MC44
JF-Expert Member
- Mar 1, 2019
- 2,169
- 3,310
Nawasalimu kwa nguvu ya utafutaji. Na kamwe mtafutaji hachoki.
2016
Nipo jirani na mgodi wa dhahabu ila haifanyi kazi kwa kigezo cha wapo kwenye hatua za utafiti. Vijana wa mtaani wakawa na tabia ya kwenda kuchimba kwa kuiba. Ikafika mahali ikawa ni kama ka miradi fulani. Tunazungumza na askari wa kituo cha polisi cha mgodi pamoja na walinzi wa mgodi wanatupa maeneo ya kuchimba.
Hapa tunachimba vikole. Shimo ni futi 15 hivi tayari umepata vitu. Tukafanya kazi tukawa tunagawana 400 mara 100 mara 200. Shift ikatoka.
Siku ya balaa.
Tuliitwa kuingia shift, za usiku. Tukapanga maeneo ya kazi na kazi ikaanza. Asubuhi tukiwa tunatoka tukapata taarifa ya kusitisha kazi kwamba kuna ukaguzi kutoka juu. Tukaacha mashimo yakiwa hayajafika kwenye ulaji. Siku ya kwanza ikapita.
Siku ya pili tukafanya mchongo na wale walinzi (hawaijui dhahabu) tukawapa 30 elfu tufanye kazi kwenye mashimo waliyoacha wengine. Siku ya kwanza tukafanya kazi hatujafika, siku ya 2 tukafanya kazi tukauza tukagawana 150. Siku ya tatu tukagawana kama 200
Tukawa hoi tukasema tupumzike halafu tukamalizie. Siku ya kwenda kumalizia sasa kumbe wale jamaa wenye mashimo yao walishtukia, wakasubiri tumefika kule wakaenda polisi, wakachukua askari wawili na bunduki.
Dhamira yao niuawe au nijeruhiwe vibaya kwa kuwa nimefanya mpango huo. Kweli askari wakaja, ila tukashtuliwa, aisee tulikimbia ni balaa, hadi nikafika home salama.
Nyumbani mke wangu hajui kama tunafanya ya wizi. Akajua tumeruhusiwa. Nikafika saa 6 nikalala, asubuhi nikaingia job, baadaye mtaani. Wale wenye mashimo wakaja wakasema MC44 NITAKUCHOMA KISU LAIVU UMEHARIBU HELA YANGU.
Aisee niliishi bila amani kipindi hicho, nikaitwa na OCS alikuwa jamaa yangu, wala haikuwa noma.
Akaja ofisini kapiga biti tusiende kule.
All in all, ni katika harakati za utafutaji.
Mgodi bado haujafunguliwa naangalia kama itawezekana kupeleka tena kikosi.