Jamaa atengeneza sufuria mbili kwa moja

Wasiojua kupika nawatambua hapa..

Haiwezekani
 
NAKUPINGGA...kiongozi unaonaje kuwa kama mboga ikiiva ukihihifadhi kwenye vyombo maalum vya kuhifadhia mboga kama hotpot...ama countainer....? nadhani sio lazima mboga ibaki kwenye sufuria
 
Inayoiva unaichota unahamishia kwenye chombo kingine
 
Inarahisisha kwenye upande wa mboga pia unaeza kupika wali afu hapo hapo ukachemsha chai,

Unapika mboga huku upande wa pili anachemsha maji ya kukoga watoto
Heheh
 
Unapika chai afu pembeni unapika mchuzi wa samaki afu unafunikia ili vichemke.Badae unakunywa chai yenye ladha ya samaki hadi raha.
 
Inayoiva unaichota unahamishia kwenye chombo kingine
Ni kweli mkuu kwa hivyo inakuwa rahisi sana ila kwa hiko chombo kilivyo mfano mchuzi ukiiva hapo huwezi kuhamishia kwenye chombo kingine alafu kile kisehemu kikabaki hakina mchuzi,kuna mchuzi utabaki ambao huo mchuzi utaanza kuungua na kusababisha kuharibu sufuria.

Otherwise akimaliza atie maji mengi kusafisha sufuria.

Ila kiupande fulani hii sufuria kutumia ni kuongeza ugumu sana.
 
Wazo zuri kwa wazee wa geto,ila angeweka kona pande zote za ndani.
 
Yapo ya kuzingatia kwenye upishi huo kama ilivyoandikwa na mtoa mada pale.
Huwezi pika Maharage na Chai
Huwezi Kaanga samaki na ugali
Utaangalia vyakula vinavyoshabihiana hasa wale wazee wa mboga saba wanaelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…