Jakaya Mrisho Kikwete ni Amiri Jeshi Mkuu!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jakaya Mrisho Kikwete ni Amiri Jeshi Mkuu!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kigarama, Nov 10, 2011.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wakati wanajeshi wanakula kiapo cha utii mbele ya Rais, tafsiri yake ni kwamba wanasema hawatafanya jambo lolote lile lililo kinyume na matakwa ya Rais ambaye ndiye Amiri Jeshi Mkuu. Amiri jeshi Mkuu ndiye "Bosi" wa majeshi yote ya ulinzi na usalama na ikiwa majeshi hayo yatakwenda kinyume cha matakwa ya Amiri Jeshi Mkuu basi majeshi hayo yatakuwa yameasi. Kwa hiyo uasi siku zote huwa ni dhidi ya Amiri Jeshi Mkuu na wala si dhidi ya nchi anayotawala Amiri Jeshi Mkuu.

  Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Kama ukikuta Polisi mitaani wanakong'ota watu au kutaka rushwa, basi juwa hayo ni matakwa ya Amiri jeshi Mkuu, Kama Polisi wanazuia Maandamano au "mikesha" ya wanasiasa juwa kabisa wasingefanya hivyo kama si matakwa ya Amiri Jeshi Mkuu. Kama unasikia Polisi wanasema Al shababu wataingilia maandamano ya wanaharakati, basi juwa Amiri Jeshi Mkuu naye anaamini Hivyo!!

  Hoja yangu hapa tusiwachukie maaskari kwani nao pia wapo kazini na wako kwenye kutimiza kiapo chao cha kumtii Amiri Jeshi Mkuu.

  Kwa nini tusishughulike na Amiri Jeshi Mkuu ambaye hawa Askari wanaotupiga virungu wanamtii yeye??
   
 2. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  nchi haina kiongozi by the way
   
 3. dhahabuinang'aa

  dhahabuinang'aa Senior Member

  #3
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hii nchi ina miaka 6 hatuna rais tunaongozwa kichwa nazi kichwa viroboto watanzania tuamke.
   
 4. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,996
  Likes Received: 2,651
  Trophy Points: 280
  Product za Msoga hazifai kabisa.
   
Loading...