Ninaomba niwe mkweli katika hili. Nilikuwa ninampenda sana Jakaya Kikwete na bado nitaendelea kumpenda, japo mimi ni mtoto wa mkulima tena wa jembe la mkono niliyebahatika kusoma vizuri enzi hizo kwa sababu ya sera za Hayati Mwl. Nyerere - Baba wa Taifa.
Jakaya Mrisho Kikwete ni mtu mstaarabu na muungwana sana. Hapendi kukosana sana na watu, hususani anaowafahamu. Hilo ndilo nilomtafuna kwa kasi yeye binafsi na chama chake!
Wito wangu kwa Mh. J.K, chondechonde zinduka CHADEMA wameishaingia sebureni bado tu kuingia chumbani! Walianza pole pole na tukadhani ni kikundi cha msimu, lakini ishara na viashilia vyote vinaonyesha, CHADEMA siyo tena Chama cha Msimu. Ninaandika haya nikijua kuwa hapa jamvini wengi ni CDM, lakini sina namna yoyote ya kukutumia ujumbe wa kukushauri sababu ya itifaki yako kama Rais. Baadhi ya watu wako waliokuzunguka aidha hawakushauri vizuri au bado wana underestimate CHADEMA.
Dr. Slaa kama kamanda mkuu wa CDM ni mtu makini, jasiri, mvumilivu na mpiganaji wa kweli. Ninampenda sana na kumuombea kwa Mungu afya njema japo sipo CDM. Ninapoandika haya ninajua ninachokisema na sina ushabeki wowote ni CDM wala CCM.
J.K tafadhari, zinduka CHADEMA wameingia sebureni sasa wanajipanga kuingia master bedroom!
Please man. Kikwete ni Fisadi number moja na wizi wake wakura, uzembe, kuficha siri za wizi wa mali za watanzania na kushiriki kuwamaliza wananchi ndivyo vimechangia jk kuwa incompetent. Tafadhari sijawahi kuona kiongozi anasifa unazozisema, maybe unataka kuwadanganya tena kwa mbinu mpya kama za dairy news na tbs. Not this time ....