Jaji Zenji awajibu wanasheria | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Zenji awajibu wanasheria

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Mar 21, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  Jaji Zenji awajibu wanasheria Send to a friend Sunday, 20 March 2011 21:01

  Salma Said, Zanzibar
  JAJI Mkuu Zanzibar, Hamid Mahmoud amesema katiba ya Zanzibar inamruhusu kuendelea na wadhifa huo, baada ya kuongezewa mkataba na Rais, licha ya kustaafu kwa hiari na kulipwa mafao yake.

  Jaji Mkuu alisema hayo katika barua yake kwenda kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, kujibu hoja za chama cha wanasheria Zanzibar ambao walisema watafungua kesi kupinga uhalali Jaji huyo kuendelea kuwa katika nafasi hiyo.

  Jaji Mahmoud katika barua barua hiyo ambayo gazeti hili imeiona nakala yake, alisema baada ya kustaafu kuna kazi ambazo alikuwa hajazikamilisha na kwa kutumia kifungu cha 95(3) cha Katiba ya Zanzibar aliongezewa muda ili kukamilisha kazi hizo.

  Jaji Mahmoud katiba baru yake hiyo ya Machi 17, mwaka huu yenye kurasa saba alikikariri kifungu hicho cha Katiba kwamba: “Licha ya kuwa Jaji amefikia umri ulioainishwa katika kifungu cha 95 (1), Jaji wa Mahakama Kuu ataendelea katika wadhifa wake huo mpaka pale atakapomaliza shughuli zote zilizomfikia kabla ya kutimiza umri huo.

  Kwa msingi huo jaji Mahmoud alisema kuendelea kwake na kazi katika wadhifa huo ni halali kisheria na hajakiuka kifungu chochote cha katiba na hakukuwa na haja ya kuteuliwa Jaji wa Mahakama Kuu na baadaye kupendekezwa tena kuwa Jaji Mkuu kama inavyodaiwa na chama cha wanasheria.

  Alisema katika mkataba wake huo mpya inaelezwa wazi utaratibu utakaoumia kuhusu malipo baada ya kustaafu na analipwa pencheni katika muda wa miaka miwili hadi Aprili 30 mwaka huu.

  “Mkataba huu umeeleza kuwa nilipwe kile tu ambacho silipwi katika malipo yangu ya pencheni, mengine yaliyomo ni kama yalivyo katika utumishi wangu katika nafasi hiyo, kama vile haki ya kupata likizo na malipo ya muda wa ziada nitakaokuwa nimefanya kazi baada ya kustaafu,” alisema.

  Alisema kwamba hakuna msingi wowote kwa chama cha wanasheria Zanzibar kuitaka mahakama imtake Rais wa Zanzibar kuunda tume ya kuchunguza uhalali wa kuendelea kushika wadhifa wa Jaji Mkuu.

  Alisema mahakama haina uwezo wa kisheria kumpa Rais amri yoyote ile hasa kwa kuzingatia uamuzi wa mahakama unatolewa kwa mtu ambaye amefikishwa mahakamani na kupewa nafasi ya kujitetea.

  Jaji mkuu alieleza kwa vile hakuna sheria ya kumfikisha mahakamani Rais awapo madarakani na kwa maana hiyo hakuna uwezekano kwa mahakama kumuamuru Rais aunde tume.

  Akizungumzia hoja za Jaji mkuu, Rais wa chama cha wanasheria Zanzibar, Yahya Hamad alisema hoja za chama hicho ni kwamba utaratibu mzima wa kumuongezea mkataba ulifanyika kinyume na ibara ya 94(1) ya Katiba ya Zanzibar.

  Alisema baada ya Jaji Mkuu kustaafu kwa hiari hakuna kikao cha Tume ya Utumishi wa Mahakama ambayo kiliwahi kujadili mkataba wake wa kazi na kuupitisha licha ya tume ya utumishi wa mahakama, kwa mujibu wa katiba kuwa na jukumu la kujadili na kupitisha mkataba huo.

  Yahya alisema kwamba baada ya kustaafu kwa hiari alitakiwa ateuliwe tena kuwa jaji wa mahakama kuu na ndipo aongezewe tena mkataba wa kuwa Jaji Mkuu, jambo ambalo halikufanyika na ni kinyume na katiba ya Zanzibar.

  Rais huyo alisema kwakuwa uteuzi wake umekiuka katiba na ndio mana wanaiomba mahakama itangaze kuwa kuwapo kwake kwenye wadhifa huo ni batili kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar na serikali ikubaliane na hoja zao.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Mar 21, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,613
  Likes Received: 419,253
  Trophy Points: 280
  PHP:
  Jaji Mahmoud katika barua barua hiyo ambayo gazeti hili  imeiona nakala  yakealisema baada ya kustaafu kuna kazi ambazo alikuwa   hajazikamilisha na kwa kutumia kifungu cha 95(3cha Katiba ya Zanzibar   aliongezewa muda ili kukamilisha kazi hizo.
  a piece of rubbish reasoning..........................huwezi ukapewa kibali cha kumalizia kazi na hapo hapo ukapemwa promotion kama vile bado ajira yako ni endelevu.........................Shein is a big disgrace............................hivi hajui soko la ajira linadaia mabadiliko makubwa ya wazee kuachia ngazi vijana ambao wanasaga lami mtaani?
   
Loading...