Jaji Werema hatufai

Jaji Werema hatufai

Tatizo lenu washabiki wa Chadema kila mtu mnafikiri mnaweza kumfanya kama mlivyomfanya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wenu wa BAVICHA.Huyu ni chaguo la Rais wa Tanzania na yuko kwa maslahi ya watanzania siyo ya wana chadema kama wanavyotaka.

Ccm hapo ndipo mnapokosea mnadhani kila anayekosoa madude yanayofanywa na hao wajinga wenu ni chadema,nchi hii si ya chadema wala ccm,kila mtu anauchungu nayo kwa hiyo unapokuwa na kiumbe dhaifu ktk kutekeleza mambo ya msingi mfano kutenda haki ni lazima azodolewe na hasa anayelipwa na kuishi kwa kodi zetu
 
Hingi kweli hapa kuna dalili za u-chadema wala u-ccm? Mwanasheria Mkuu wa Serikali anatoa majibu ambayo hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria hawezi kutoa, then unasema mashabiki wa chadema. Hapa tumeongelea kama alichojibu kilistahili nje ya siasa kumbuka kumfanya Mwanasheria Mkuu sio kua ndio tiketi ya kua mwanasiasa.
 
Huyu AG kutokana n'a utendaji wake wa kazi kwa mtindo wa mtumikie kafiti upate mradi wako, ameitukanisha sana taaluma ya sheria, mfano mmojawapo ni namna alivyotaka kuizima hoja ya Zito Kabwe, kuhusu mabilioni ya pesa yaliyofichwa Uswisi, ambapo benki kuu ya uswisi mwaka jana ilitoa taarifa kuwa vigogo 6 kwenye serikali ya CCM wameficha kwenye mabenki ya uswisi pesa kiasi cha dola za kimarekani milioni 197, sasa badala ya mxanasheria mkuu kufanya juhudi ya kuzirejesha pesa hizo yeye anawakingia kifua mabosi wake walioficha mapesa yetu huko!!!
 
Exactly, akili zao kama za LEMA tu.

akili za magamba uuuwii lusinde style. Yaani mwanasheria wa serikali ya magamba ananashindwa kutolea ufafanuzi suala lililowazi mpaka asubiri utafiti? Utafiti gani huo? Mahakama si imeshatoa hukumu sasa rais wa serikali ya magamba anapoingilia kazi za mhimili mwingine na mwanasheria mkuu wa serikali ya magamba anashindwa kutolea ufafanuzi! Pathetic!
 
Kwa tanzania ya sasa na katiba hii ni vigumu kwa wanasheria kufanya kazi zao kitaaluma kwa kuwa wanalinda matakwa ya waliowaweka kwenye madaraka. Ona kenya katiba yao ilivyowapa uhuru, kama leo mwanasheria mkuu wa kenya anatamka waziwazi kuhusu muswada wa kuongeza marupurupu ya rais kibaki kuwa si sahihi, kwetu hapa haiwezekani.
 
Huyu mtu haeleweki. Alishasema Zanzibar ni nchi lakini hakusema ilipo Tanganyika! Wenzie wanaongea mambo kisiasa, yeye anaropoka .
 
Back
Top Bottom