Jaji Warioba na tume yake kushitakiwa

Jaji Warioba na tume yake kushitakiwa

Mkuu pole kwa kutofikiwa na tume.Wako mamilioni ya watanzania ambao hawakufikiwa na tume ambao walikuwa na maoni ya maana sana ambayo tume haijaweka kwenye rasimu kwa sababu hawakuwafikia.
Lakini wote ambao hawakufikiwa wasihofu kuna wabunge wao ambao wako kwenye bunge la katiba wawape tu hayo maoni.Kuna wengne ni wafugaji nakumbuka walienda bungeni kupeleka maoni yao kwa kuwa tume haikuwafikia ili wanapojadili hiyo rasimu bungeni na hayo maoni yao wayajadili pia kama wawakilishi wao.

Tume ya warioba iliandika kwenye rasimu maoni ya hao wachache waliojaliwa kukutana na tume.Walio wengi mawazo yao yanabebwa na wabunge na wawakilishi wa zanzibar.

Ndio maana tunalaani kwa nguvu zote kitendo cha wabunge wa katiba wa kundi la UKAWA kususia kuingia bungeni huku wakijua kuwa kuna watu wengi ambao hawakufikiwa na tume ambao wao wabunge ndio inabidi wawakilishe maoni yao katika bunge la katiba wakati mijadala inaendelea.Kitendo cha wabunge wa UKAWA kususa wanawakosesha watu wa aina ya hao wa Rombo maoni yao kujadiliwa bungeni.

UKAWA wamejipambanua kuwa wao ni wabunge wa wale tu waliotoa maoni na kufika mbele tume ya warioba tu.
Hao wengine ambao hawakupata hiyo nafasi UKAWA si wabunge wao.Kwa hiyo wao na maoni yao wafilie mbali.Ni kama wanawachukulia kuwa kama si watanzania.Nawasihi UKAWA warudi bungeni kuna makundi wana maoni tena mazuri tu ambayo hayamo kwenye rasimu lakini hayakuwekwa kwa kuwa hawakufikiwa.

Wanarombo msiende mahakamani pelekeni maoni yenu kwa mbunge yeyote wa bunge la katiba anayehudhuria vikao au tumeni wawakilishi fungeni safari nendeni dodoma muwakilishe maoni yenu kwa spika mueleze wazi kuwa hamkufikiwa na tume na tume haijaweka kwenye rasimu. Atayapokea na kuyapeleka yawemo kama sehemu ya mijadala inayoendelea. Yakionekana yafaa yatawekwa kwenye katiba.Msihofu bado nafasi ya maoni yenu kufika ipo kwa kupitia wabunge wenu.Ila kama mbunge wenu ni UKAWA achaneni naye sababu kasusa hatapeleka mpeni yeyote anayeingia kwenye vikao vya bunge la katiba linaloendelea.

Noted mkuu, ila haiwapotezei haki ya kumpeleka mahakamani.
 
bado hujawashawishi kitu, uanze kuwapa darasa walioenda shule na ambao hawakuenda maana ya sampling! Wala tume haikuambiwa kusanyeni maoni kwa kutumia sampling, huo bado ni ubaguzi wa kisampling.

..... Kwahyo Hata Sis Ambao Hatukumpigia Kura Jk 2nabaguliwa Siyo? Mbna Jk Alipata Kura M6 Na Anaongoza Watu M48
 
Nahisi hakukua na elimu ya kutosha na sasa watu ndio wameanza pata elimu khs katiba mpya
 
... Mtaambiwa Na Ccm Kuwa Nyie Ni Wakenya, Si Umeona Ya Kigoma Yametiwa Kapuni Eti Ni Wakimbizi Wa Burundi, Rwanda Na Kongo

naona umebadili topic tena!
 
acha kuleta jok mkuu, raisi nani alimtuma atembee kila kijiji? Tume ya Warioba ilitumwa kukusanya maoni ya Watanzania, iweje kwingine hawakufika halafu waseme maoni ni ya Watanzania?

Mnatapatapa tu,kwani tume iliambiwa itembelee kila kijiji na kata? Kwa nini hawakutuma maoni yao kwa tume? Hata sisi tume haikufika kutokana na muda iliopewa kukusanya maoni kuwa mfupi na ndio maana sisi tulituma maoni yetu na tunashukuru kwa kiasi yamezingatiwa na kuingizwa kwenye rasimu.
 
..... Kwahyo Hata Sis Ambao Hatukumpigia Kura Jk 2nabaguliwa Siyo? Mbna Jk Alipata Kura M6 Na Anaongoza Watu M48

raisi anatokana na katiba, katiba haitokani na raisi. Lakini pia katika uchaguz wa raisi baada ya matokeo kama huridhiki na ushindi wake unakata rufaa.
 
Noted mkuu, ila haiwapotezei haki ya kumpeleka mahakamani.

Mkuu huwezi shtaki marehemu aliyekufa na kuzikwa.Tume ya katiba ilishavujwa ofisi zake zikafungwa na website ikafungwa.Kisheria haipo.Sasa ni tume ipi ya katiba wataipeleka mahakamani wakati haipo?
 
Wakazi wa Kijiji cha Letto kilichopo Wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, wamedai kuwa hawakuwahi kuiona Tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya kwenye kijiji chao na kata yao.
Wanajiuliza je wao siyo wananchi wa Tanzania? Kwanini wabaguliwe na tume hiyo iliyopo kisheria? Wanafikiria kuishitaki tume na Jaji Warioba mahakamani kwa ubaguzi huo.

Gongo inawasumbua
 
acha kuleta jok mkuu, raisi nani alimtuma atembee kila kijiji? Tume ya Warioba ilitumwa kukusanya maoni ya Watanzania, iweje kwingine hawakufika halafu waseme maoni ni ya Watanzania?

Mbona JK alichaguliwa na maccnyemu alafu leo mnasema ni Raisi wa Watanzania wote?
 
Mnatapatapa tu,kwani tume iliambiwa itembelee kila kijiji na kata? Kwa nini hawakutuma maoni yao kwa tume? Hata sisi tume haikufika kutokana na muda iliopewa kukusanya maoni kuwa mfupi na ndio maana sisi tulituma maoni yetu na tunashukuru kwa kiasi yamezingatiwa na kuingizwa kwenye rasimu.

kama maoni yalikuwa ni ya kutuma kama watu walivyotuma maombi ya kuomba nafasi za kundi la 201, basi hakukuwa na haja ya tume kuzunguka. Tume ingeambiwa kaeni msubiri wananchi watume maoni.
 
mkuu nazungumzia kata yenye zaidi ya watu laki. Ilikuwa haki yao kufikiwa na tume. Kusema maoni ni ya watanzania wakati hawakufikiwa ina maana wao ni wakenya?

Rombo nzima haizidi watu wazima laki na nusu sasa hao laki moja kwenye kata 1 wametoka wapi? By the way hiyo kata ipo katika tarafa gani? Mkuu, mashati, tarakea, Useri au Mamsera?
 
Mkuu huwezi shtaki marehemu aliyekufa na kuzikwa.Tume ya katiba ilishavujwa ofisi zake zikafungwa na website ikafungwa.Kisheria haipo.Sasa ni tume ipi ya katiba wataipeleka mahakamani wakati haipo?

inashitakiwa iliyokuwa tume. Mbona tume za chaguzi hushitakiwa baada ya uchaguzi?
 
Rombo nzima haizidi watu wazima laki na nusu sasa hao laki moja kwenye kata 1 wametoka wapi? By the way hiyo kata ipo katika tarafa gani? Mkuu, mashati, tarakea, Useri au Mamsera?

unadhani rombo ni huko ushenzini kwenu?
 
CCM wanatapatapa sana,walishauriwa waitishe kura ya maoni wakakataa na sasa wanataka kila mtanzania angehojiwa na tume. Hivi wanatumia makalio kufikikiri au? Nchi nyingi zimetunga katiba,hivi wanaweza kutupa mfano wa nchi yoyote duniani ambako wakati wa kutunga katiba kila mwananchi alihojiwa? Hivi wanawezaje kujitoa ufahamu kiasi hiki?
 
mkuu jikite kwenye mada
 
inashitakiwa iliyokuwa tume. Mbona tume za chaguzi hushitakiwa baada ya uchaguzi?

Sheria ya tume ya warioba na ya uchaguzi ni tofauti.Anyway mimi nilikuwa nadhani issue kubwa kwa hao wana kijiji si kwenda mahakani issue yao kubwa ni maoni yao.Kuzchukuliwa na kuwa sehemu ya mchakato unaoendelea wa katiba.Nadhani wafikishe tu maoni bunge linaloendelea.Wasipoteze pesa kuwalipa mawakili ubwabwa bure.Nafasi ya maoni yao kufika bado ipo.
 
raisi anatokana na katiba, katiba haitokani na raisi. Lakini pia katika uchaguz wa raisi baada ya matokeo kama huridhiki na ushindi wake unakata rufaa.

Kwa hiyo katiba ndo ilipiga kura kumchagua Kikwete?
 
Back
Top Bottom