Jaji warioba akimbizwa bondeni

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,778
WAZIRI Mkuu na Makamu wa Rais mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba (69), amepelekwa Afrika Kusini kwa matibabu baada ya afya yake kuzorota; Tanzania Daima imebaini.

Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata kutoka vyanzo vilivyo karibu na familia ya Jaji Warioba zinaeleza kuwa mwanasiasa huyo anayeheshimika, alisafirishwa kwenda Afrika Kusini jana alfajiri.

Kwa mujibu wa habari hizo ambazo hata hivyo hazikueleza kiongozi huyo mstaafu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa gani, zilizothibitishwa na mwanafamilia mmoja, zilisema kuwa hali yake haikuwa ya kukatisha tamaa.

Pamoja na kukiri kupelekwa Afrika Kusini kwa mwanasiasa huyo, mwanafamilia huyo alilielezea tukio la mzee wake kusafirishwa kuwa ni la kuchunguzwa afya zaidi kuliko matibabu.

"Ni kweli baba anaumwa, leo (jana asubuhi) amepelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya ‘check up' (matibabu) ili kubaini chanzo cha ugonjwa unaomsumbua," alisema mtoto huyo.

Alisema baba yake alikuwa imara hadi Jumamosi iliyopita, ambako alihudhuria mazishi ya aliyekuwa Balozi wa Kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Daudi Mwakawago.

"Jumamosi alikwenda kwenye mazishi ya Balozi Mwakawago akiwa mzima… lakini tangu juzi (Jumatatu) alionekena kudhoofika na mpaka sasa hatujajua nini kinachomsumbua zaidi," alisema mtoto huyo.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Seif Alli Idd, alipoulizwa kuhusiana na suala hilo, alijibu: "Niko Arusha kikazi, nawaomba muwasiliane na Ikulu, inaweza kuwa kwenye nafasi nzuri ya kutoa ufafanuzi."

Juhudi za gazeti hili kuwasiliana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Salvatory Rweyemamu, ziligonga mwamba baada ya simu yake ya mkononi kuita bila kupokewa kwa muda wote jana.

Kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu Novemba 5, 1985 na Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi, mwanasiasa huyo aliyezaliwa Septemba 3, 1940 amepata kushika nyadhifa mbalimbali kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Waziri wa Sheria.

Alikuwa Waziri Mkuu hadi Novemba 9, 1990 wakati Mwinyi alipovunja baraza la mawaziri na nafasi yake ikachukuliwa na John Samuel Malecela na yeye akateuliwa kuwa Waziri wa Nchi Tawala wa Mikoa na Serikali za Mitaa. Januari 17, 1996 wakati wa Serikali ya Rais wa Awamu ya Tatu, Jaji Warioba aliteuliwa na rais wa wakati huo, Benjamin Mkapa kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Rais ya Kuchunguza Mianya ya Rushwa, ambayo ripoti yake ilimjengea umaarufu na heshima kubwa katika jamii.
 
mbiu ya mgambo ikilia kunajambo (stei chuni)

mbona wantisha mie mwenzio

au ndio balali style tuambiane jamani tuwaweke wakina maezeki sby,..siku hizi wako full mpaka mwezi wa sita embu chunguza chunguza hiyo dawa inaishia lini kama ni style ya "balali""""
 
Sijui watakuwa wamempatia wapi yule jamaa yuko fit

kuanzia
biblia-quran- mpaka bagamoyo...sasa sijui wamepitia wapi hao
 
Nilishawahi kumwambia miaka fulani kuwa apunguze uvutaji wa sigara, akasema kapunguza lakini alionekana kama bado ni mvutaji asiyetaka kubandua sigara mdomoni,sigara ina madhara mabaya sana.
 
...Jaji warioba ni mmoja kati ya watanzania wachache ambaye anaweza kuweka wazi anacho amini, hata kama atapingana na dola kwa mtazamo wake huo.

Get well soon, mzee!!
 
Wapo wa kukutibu wewe sio 'wao'.
Na kenda check tu, sijui huko wanacheki nini cha ajabu ambacho Muhimbili hakiwezekani. TZ imekua corrupt mpaka inanuka. Mtu mmoja aliwahi sema hapa kua hao madaktari wao na ndio msitari wa mbele kupendekeza mgonjwa wao apelekwe nje ili tu nae apate posho, ni aibu wanadhalilisha udaktari wao kwa ubinafsi wao au ndio yale yale 'ndivyo tulivyo'.
Lakini pia hutashangaa nesi tu wa 'Kitengo Cha Ukimwi', ana RV4 mbili mpyaaa...lakini wala hafugi kuku ama nini.
 
Pole Mzee Warioba. Tunakuombea upone haraka tuendelee na mapambano.

mbona wantisha mie mwenzio

au ndio balali style tuambiane jamani tuwaweke wakina maezeki sby,..siku hizi wako full mpaka mwezi wa sita embu chunguza chunguza hiyo dawa inaishia lini kama ni style ya "balali""""

Hapo hata sina la kusema. Kuna mambo ya Mkutano wa taasisi ya Nyerere, kuna CCJ....n.k. Hii ni Bongo..... ingawa wakati mwingine yanakuwa magonjwa ya kawaida tu!
 
Acha uchuro............... Naona kama unafurahi vile !!!!

Get well soon Mzee Warioba.
 
Na kenda check tu, sijui huko wanacheki nini cha ajabu ambacho Muhimbili hakiwezekani. TZ imekua corrupt mpaka inanuka. Mtu mmoja aliwahi sema hapa kua hao madaktari wao na ndio msitari wa mbele kupendekeza mgonjwa wao apelekwe nje ili tu nae apate posho, ni aibu wanadhalilisha udaktari wao kwa ubinafsi wao au ndio yale yale 'ndivyo tulivyo'.
Lakini pia hutashangaa nesi tu wa 'Kitengo Cha Ukimwi', ana RV4 mbili mpyaaa...lakini wala hafugi kuku ama nini.

Ndiyo maana ikaitwa BONGOLAND.......... Akili mu kichwa
 
.......

Habari za uhakika ambazo gazeti hili limezipata kutoka vyanzo vilivyo karibu na familia ya Jaji Warioba zinaeleza kuwa mwanasiasa huyo anayeheshimika, alisafirishwa kwenda Afrika Kusini jana alfajiri.

.......

Pamoja na kukiri kupelekwa Afrika Kusini kwa mwanasiasa huyo, mwanafamilia huyo alilielezea tukio la mzee wake kusafirishwa kuwa ni la kuchunguzwa afya zaidi kuliko matibabu.

"Ni kweli baba anaumwa, leo (jana asubuhi) amepelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya ‘check up' (matibabu) ili kubaini chanzo cha ugonjwa unaomsumbua," alisema mtoto huyo.

..........

Kwa uelewa wangu mdogo wa lugha ya kiswahili, kusafirishwa ni neno linalotumika kuondoa kitu kisichojiweza kutoka sehemu moja hadi nyingine, e.g mzigo, magogo, mtu asiye na uhai etc.

Mtu mwenye afya anapopanda chombo cha usafiri kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa sababu yeyote ile iwayo, anasafiri.

Nipo tayari kusahihishwa.
 
Hapo hata sina la kusema. Kuna mambo ya Mkutano wa taasisi ya Nyerere, kuna CCJ....n.k. Hii ni Bongo..... ingawa wakati mwingine yanakuwa magonjwa ya kawaida tu!

Head on. It seems kaanza kuumwa KWIKWI kitambo kidogo. It is SAID, right after that TAASISI kongamano thing. Even the late, Amb. Mwakawago participated. I dont have to repeat what THEY DECLARED.

Msiunganishe na ya yule Shehe Hayahaya! Tumuombee heri apate nafuu na apone.
 
Back
Top Bottom