Jaji wa Mahakama Kuu, Biswalo Mganga, tembea kifua mbele

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
3,082
2,000
Mhe. Biswalo Mganga,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa mamlaka aliyonayo wewe Mkurugenzi wa Mashitaka nchini, pamoja na Naibu wako, na kukuteua kuwa Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania.

Mhe. Biswalo Mganga,
Ninachotaka kukwambia, kwa niaba ya wananchi wa Tanzania, hususani Wazalendo kwa taifa letu ni kwamba, baada ya utawala wa hayati Baba wa taifa mwl. Julius Kambarage Nyerere, hakujawahi kutokea Mkurugenzi wa Mashitaka aliyefanya kazi kwa viwango vyako wewe.

Wewe ni Mkurugenzi wa Mashitaka mzalendo kuwahi kutokea, uliyeipenda nchi yako, uliyepambana na wahujumu uchumi, wala rushwa, wakwepaji kodi, mafisadi, majangiri, majambazi, waporaji wa rasilimali za nchi hii, na viongozi waliotumia madaraka yao vibaya kujinufaisha. Umeifanya kazi yako usiku na mchana bila kuchoka wala kuhofia usalama wa maisha yako.

Mhe. Biswalo Mganga,
Wananchi tunatambua jinsi ulivyosimamia uendeshaji wa kesi mbali mbali za uhujumu uchumi ikiwemo ya wazungu wa kampuni ya Barrick pamoja jangiri mashuhuri muuwaji wa tembo ambaye alishindikana kukamatwa tangu alipoanza ujangiri mwaka 1986 kufikia hatua ya kujiita Malikia wa Tembo, lakini kupitia uongozi wako mahiri, leo jangiri huyu yupo gerezani, tembo wamezaliana, wanazurula hadi kwenye makazi ya watu kwa amani na raha mustarehe.

Hata kama mamlaka ya uteuzi wako imeona hufai kuendelea kuhudumu kama Mkurugenzi wa Mashitaka, nataka nikutie moyo kwamba, wananchi tunatambua mchango wa utumishi wako ulioleta matokeo chanya kwenye uchumi hadi nchi kufikia uchumi wa kipato cha kati kabla ya makadirio ya muda uliowekwa 2025.

Ni kupitia wewe, ofisi yako iliweza kurudisha fedha mabilioni yaliyokuwa yakiibwa na wafanya biashara walioigeuza nchi hii kuwa shamba la bibi, akiwemo aliyekuwa akiiba milioni 7 kwa kila dakika kwa njia ya kukwepa kodi kwa kutumia mfumo wa mashine za EFD.

Wewe ndiye Mkurugenzi wa Mashitaka uliyekomesha tabia sugu ya Wana siasa hususani wa upinzani iliyokuwa imeota mizizi ya kutoheshimu sheria, kanuni na taratibu za nchi. Hukuangalia cheo cha mtu wala nafasi aliyonayo katika jamii. Ni nani kama Biswaro Eutropius Mganga?

Mhe. Biswalo Mganga,
Uzalendo wako kwa nchi si tu kwamba ulibakia kulinda rasilimali za ndani bali ulivuka mipaka kwa kufuatilia rasilimali zilizoporwa na kutoroshewa nje ya nchi, ambapo ulifanikisha kurejeshwa kwa madini ya dhahabu na mamilioni ya fedha zikiwemo dola za Marekani zilizoporwa na majambazi nchini mwaka 2013 na kukamatiwa Kenya. Hongera sana kwa hilo.

Kwangu mimi wewe ni shujaa miongoni mwa mashujaa waliowahi kutokea katika kuitetea nchi na rasilimali zake. Wewe ni kiongozi uliyehakikisha kila mkosaji anashitakiwa, bila kujali anayo nafasi gani kwenye jamii au ni maarufu. Ulikomesha majigambo ya waliokuwa wakisema, UNANIJUA MIMI NANI. Uonevu ulikoma kama siyo kumalizika. Hakuna DPP kama wewe. Mungu akutunze.

Nataka nikuhakikishie kwamba, historia ya nchi hii kuhusu ujenzi wa uchumi, ulinzi wa rasilimali za nchi, mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi, matumizi mabaya ya madaraka, haiwezi kuandikwa na kukamilika bila jina lako kutajwa, na kwa msingi huo, historia italiandika jina lako kwa wino wa dhahabu.

Mhe. Biswalo Mganga,
Naomba nihitimishe hoja yangu kwako kwa kusema kwamba, ustawi wa kiuchumi wa taifa lolote duniani, unategemeana kwa kiasi kikubwa na uimara wa ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka katika nchi husika.

Mafanikio ya kiuchumi yaliyopatikana kwa nchi yetu ikiwemo ufanisi katika kukusanya kodi, ujenzi wa miradi mikubwa ya kimkakati kama vile Bwawa la Mwl. Nyerere, Ujenzi wa reli ya Standard Gauge, Ujenzi wa Vituo vya afya, Zahanati, Hospitali za Wilaya, Mkoa na Kanda, Usambazaji wa maji mijini na vijijini, usambazaji wa umeme vijijini, utoaji elimu bure, mikopo ya elimu ya juu, yote haya yamewezekana kutokana na ushupavu wa uongozi wako ukiwa Mkurugenzi wa Mashitaka.

Kwenye nchi yoyote ambayo Mkurugenzi wa Mashitaka anakuwa upande wa wahalifu, haya yasingewezekana kufanyika. Nikuombe nenda kachape kazi kwenye nafasi yako mpya, huku ukimtanguliza Mungu mbele. Tembea kifua mbele, wananchi wazalendo tupo nyuma yako. Usisikilize kelele za maadui wa kazi yako wala kunyong'onyea bali endelea kusimama kwenye nafasi yako ya kulitetea taifa. Hakika uongozi wako umeacha alama isiyofutika..

Lema na Chadema kwa ujumla mkome kumwandama jaji Biswaro Mganga, kesi zenu za uhujumu uchumi ataziamua yeye.
 

Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
2,334
2,000
Tumekusikia Mh. Biswalo

Ila yale machozi ya wale walioporwa yale mahela yao kwa kisingizio cha plea bargain bado hayajakauka
 

Nyange

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
3,479
2,000
Yale machozi ya waliosingiziwa kesi kamwe hayatawaacha salama, damu ya Yesu inanena mema, ilishaanza kulipiza kisasi, subiri zamu zenu.
 

tzkwanza

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
1,576
2,000
Arudishe pesa za kina Kitilya na Kabendera kwanza.

Huyo ni mhalifu kuliko unavyodhani.

Time will tell!
 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
3,845
2,000
Ifike mahala sasa, tusikubali viongozi wetu ambao wanajitoa kufanya kazi kwa moyo mmoja wachafuliwe kirahisi rahisi hivi.

tumeshuhudia tabia hii imeshamiri kwa kasi kubwa sana mara baada ya hayati JPM kuaga dunia!! hili halikubaliki na wala lisifumbiwe macho, tumeona maneno na kashifa nyingi zikitolewa kwa viongozi wetu wajuu, tuhuma za kizushi, majungu na fitina, hii si sawa.

mamlaka zinazo husika chukueni hatua, kwa nini mnaachilia watu wanachafuliwa tu, kutokana na chuki binafsi!!

kazi aliyo ifanya DPP ni ngumu sana ambayo hata angekuwa mtu yoyote yule lazima upate maadui wengi tu, ni sawa na kazi ya Ujaji au Uhakimu kamwe huwezi kupendwa na watu wote lazima wapo wengi watakuchukia kutokana na aina ya kazi yako kuwa huwezi kuwaridhisha watu wote na haswa kama unamsimamo na unasimamia sheria kikamilifu.

Biswalo ni mtu alijitolea kufanya kazi zake kwa uaminifu wa hali ya juu na kutokana na uadilifu wake wapo ambao walitaka kumtoa kwenye msimamo na walishindwa, sasa nadhani ndio wakati wao wa kupiga majungu na kumfitini ilimradi achafuke ili wapate ushindi.

kamwe Rais wetu asiingie kwenye mtengo na kuwasikiliza watu wenye chuki zao binafsi.
 

Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
12,836
2,000
Ifike mahala sasa, tusikubali viongozi wetu ambao wanajitoa kufanya kazi kwa moyo mmoja wachafuliwe kirahisi rahisi hivi.

tumeshuhudia tabia hii imeshamiri kwa kasi kubwa sana mara baada ya hayati JPM kuaga dunia!! hili halikubaliki na wala lisifumbiwe macho, tumeona maneno na kashifa nyingi zikitolewa kwa viongozi wetu wajuu, tuhuma za kizushi, majungu na fitina, hii si sawa.

mamlaka zinazo husika chukueni hatua, kwa nini mnaachilia watu wanachafuliwa tu, kutokana na chuki binafsi!!

kazi aliyo ifanya DPP ni ngumu sana ambayo hata angekuwa mtu yoyote yule lazima upate maadui wengi tu, ni sawa na kazi ya Ujaji au Uhakimu kamwe huwezi kupendwa na watu wote lazima wapo wengi watakuchukia kutokana na aina ya kazi yako kuwa huwezi kuwaridhisha watu wote na haswa kama unamsimamo na unasimamia sheria kikamilifu.

Biswalo ni mtu alijitolea kufanya kazi zake kwa uaminifu wa hali ya juu na kutokana na uadilifu wake wapo ambao walitaka kumtoa kwenye msimamo na walishindwa, sasa nadhani ndio wakati wao wa kupiga majungu na kumfitini ilimradi achafuke ili wapate ushindi.

kamwe Rais wetu asiingie kwenye mtengo na kuwasikiliza watu wenye chuki zao binafsi.
Hakuna mtu mbaya na atakayebeba laana za watu km huyo jamaa, kesi alizibeba vibaya mpaka anatamka anaweza kumsamehe mshtakiwa saa yoyote au kumweka ndani mtu yoyote. licha ya kuzuia mabilioni 60 bila serikali kujua
  1. Rugemalila ana kosa gani mpaka sasa
  2. Habinder Sigh wa PAP
  3. Kabendera mpaka kafiwa na Mama yake, kwenda kuzika tu kakataliwa ili tu afilisiwe
  4. Kachungulia a/c za matajiri wote na kuchomoa pesa zao
  5. kwenye siasa wameshtakiwa watu kibao bila ya ushahidi tu basi kuminya sauti zao
  6. kakataa ushindi wa hukumu ya uminyaji wa waandishi wa habari iliyotolewa na Afrika mashariki
  7. Majura Makamu wa Klabu ya Simba mpaka alipoamua kutoa kitu akaachiwa
  8. Kamtoa mshtakiwa mahabusu na kumpa Ubunge viti maalum
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom