Jaji Sinde Warioba kanishangaza

Jaji Sinde Warioba kanishangaza

Hujajibu swali lililoulizwa.

Somo la ufahamu unalifahamu?

Mara hii umesha sahau haya hapa chini kwenye nyekundu siyo?
Jibu gani unataka zaidi ya hilo?

Unajua aina nyingine ya Binadamu asili yao-kuuma na kupuliza na waoga wa maisha hasa masilahi Binafsi yanapoingia katikati yake.
Kwamba huamini mpaka sasa kuwa ni mtu cheap siyo?.
Endelea kuamini hivyo na ni haki yako !
 
Mara hii umesha sahau haya hapa chini kwenye nyekundu siyo?
Jibu gani unataka zaidi ya hilo?

Niendelee kuamini nini?

Hivi una uwezo wa kuweka hoja iliyokuwa sophisticated kichwani mwako?
 
Ikumbukwe kuwa Jaji Warioba alikuwa akizunguka kutoa elimu ya uraia pamoja na kueleza wananchi jinsi maoni yao yalivyotupwa kwenye rasimu ya katiba jambo ambalo lilifanya atukanwe, adhihakiwe, adharauliwe na hata kudaiwa kupigwa.

Kilichonishangaza ni yeye kusimama jana na kupiga kampeni kwa wagombea, wakati kwanza chama hicho ndo kilihusika kusigina maoni ya wananchi, pili mmoja wa wagombea alikuwa makamu mwenyekiti bunge la katiba sasa Mh. Warioba ulikuwa unazunguka kufanya nini kwa wananchi ikiwa leo una wanadi waliosigina maoni ya wananchi?

Sikutegemea kwa kweli, sasa vipi ile rasimu ya wananchi ndo huitetei tena? Nimewaza kwa sauti wajamaeni.

Weweee, huwezi kumtumia Jaji Warioba kuingiza mafisadi ikulu, watu kama Lowasa,Rostam na akina Karamagi. Mambo ya katiba chadema mmeyatumia kwa hila za kupata madaraka tu.
 
Niendelee kuamini nini?

Hivi una uwezo wa kuweka hoja iliyokuwa sophisticated kichwani mwako?

Fanya marudio labda utaelewa nilicho maanisha kinachokustahili kuendelea kukiamini!
Sijalelewa sana na hiyo lugha ya kimalkia na kwa uwezo wa shule yangu ya kata umeniacha pembeni kidogo.Unaamaanisha nini vile?

Tatizo umeishia shule ya kata halafu unataka kuchambua data.
 
Tatizo umeishia shule ya kata halafu unataka kuchambua data.
Hili nimelipenda .

Na kama hicho sijui Data ndiyo kama hizi hapa chini ahaaaaaaaaaa! Shule yangu ya Kata inaweza kuwa imenikomboa na pengine ndoto ya Elimu Elimu Elimu ya Lowassa ikanikwamua muda siyo mrefu!

  • Kiranga #214

    Unatoa conclusion ambayo ni ignorant.

    Unajua anachojua Warioba mpaka useme hajiamini na ni mwoga ndiyo maana kakataa kuwa mgombea wa UKAWA?

    Akikwambia UKAWA hakijakomaa kuongoza nchi na hakina organization, na hiyo ndiyo sababu hajakikubali itamlazimisha akione kimekomaa?

    Ni lazima kila mtu aone sawa na wewe?

    Warioba kapewa nafasi ya kugombea urais UKAWA. Warioba angekuwa na credibility zaidi ya Lowassa kama mgombea wa irais wa UKAWA.

    Kama kweli anaweka maslahi binafsi mbele, mbona kakataa kugombea urais?
    [*]
    quote_icon.png
    By Kiranga

    Watanzania wana kazi ngumu uchaguzi huu.

    Kwa upande mmoja wameshaichoka CCM na mfumo wake.

    Kwa upande mwingine, hata huko UKAWA hawa makapi wa CCM washakuteka.

    Hapo ni sawa na mlinzi wa kimakonde kakufuma anakwambia "ukichimama nchale, ukikimbia nchale".

    [*]
    quote_icon.png
    By Kiranga
    Lowassa angekuwa convincing zaidi kama angetoka CCM kabla ya kukatwa.

    Sasa hivi anaonekana kama anataka urais tu.

    Kama Lowassa asingekatwa na angechaguliwa kuwa mgombea wa CCM angekuwa na ujasiri wa kuikana CCM?

    Au anaikana CCM sasa tu kwa sababu kakatwa?

    Bado naamini Warioba yuko motivated by principle than machinations. Anaona wakati huu wa kuingia kwa rais mpya kuna an opportunity of reshuffling the cards na yeye anataka kuji position kama mtu influential. There is nothing wrong with that, especially if haamini kama UKAWA wako tayari kuendesha nchi.
 
Ana haki ya kuonyesha mahaba yake juu ya mtu anaemtaka, kwa hiyo ulitaka ahamie ukawa, siasa maji taka,wew ndo maiti wa tanzania uliebaki,kwa akili yako unafikili watanzania watamchagua huyo lowasa wako ambae hana chembe ya uwadilifu,tusubili tu act ikue ndo kitakuwa chama mbadala wa upinzani maana ukawa wamepoteza dira
 
Hili nimelipenda .

Na kama hicho sijui Data ndiyo kama hizi hapa chini ahaaaaaaaaaa! Shule yangu ya Kata inaweza kuwa imenikomboa na pengine ndoto ya Elimu Elimu Elimu ya Lowassa ikanikwamua muda siyo mrefu!

That is neither here nor there but gibberish and gobedlygook.

Endelea kuota.
 
That is neither here nor there but gibberish and gobedlygook.

Endelea kuota.

Kweli wengine mna matatizo tena yanayohitaji mtaalamu wa afya ya akili. Hivi unadhani kuandika kimalkia ndiyo kuonekana kuwa unachamaana ulichoandika.
Unadhani kusifiwa kuwa lugha ya kimalki kidogo unakifahamu ndiyo ufahamu wa mambo?

Kipi hicho cha kwako chenye maana na ambayo siyo ndoto kuendana na hoja hii ya -Jaji Sinde Warioba kanishangaza!
Tena naona unandoto mbaya ya mchana kama ya Mkapa na matusi yake Jangwani kwa wapinzani!

quote_icon.png
By Kiranga

Lowassa angekuwa convincing zaidi kama angetoka CCM kabla ya kukatwa.

Sasa hivi anaonekana kama anataka urais tu.

Kama Lowassa asingekatwa na angechaguliwa kuwa mgombea wa CCM angekuwa na ujasiri wa kuikana CCM?

Au anaikana CCM sasa tu kwa sababu kakatwa?

Bado naamini Warioba yuko motivated by principle than machinations. Anaona wakati huu wa kuingia kwa rais mpya kuna an opportunity of reshuffling the cards na yeye anataka kuji position kama mtu influential. There is nothing wrong with that, especially if haamini kama UKAWA wako tayari kuendesha nchi.

Kweli wengine mna matatizo tena yanayohitaji mtaalamu wa afya ya akili. Hivi unadhani kuandika kimalkia ndiyo kuonekana kuwa unachamaana ulichoandika.
Unadhani kusifiwa kuwa lugha ya kimalki kidogo unakifahamu ndiyo ufahamu wa mambo?

Kipi hicho cha kwako chenye maana na ambayo siyo ndoto kuendana na hoja hii ya -Jaji Sinde Warioba kanishangaza!
Tena naona unandoto mbaya ya mchana kama ya Mkapa na matusi yake Jangwani kwa wapinzani!

Tofauti kati yangu mimi na wewe ni kwamba wewe unaamini kila mtu anatakiwa kufikiri sawa na wewe.

Mimi naamini kila mtu ana uhuru wa kujiamulia mambo yake mwenyewe kwa mujibu wa anavyoona yeye inafaa.
 
..kuna mambo ambayo nadhani ni ya msingi Jenerali Ulimwengu ameyazungumzia ktk makala yake.

..jisomee kipande kidogo nilichoweka hapa. pia unaweza kusoma makala nzima ktk gazeti la raia mwema.

..off course mada ya Jenerali ni pana kuliko heading ya uzi huu. naamini wengine pia mtatoka na conclusions zenu tofauti.

TAFAKURI JUU YA JK NYERERE, WARIOBA, CCM NA WAPINZANI -- JENERALI ULIMWENGU

NILIMALIZIA makala yangu iliyopita kwa kutoa mawazo yangu kuhusu misimamo ya Jaji Joseph Sinde Warioba kama kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na kumueleza kama mtu muungwana ambaye anaamini kwamba na wale walio karibu yake ni waungwana, ambalo ni kosa kubwa. Nilisema vile vile kwamba hata angetendewa vibaya namna gani na chama hicho, hawezi kukihama kama walivyohama wengine waliohisi kwamba hawakutendewa haki.

Vitendo vya kihuni alivyofanyiwa vinajieleza, na hao waliopewa zawadi kwa kumtendea hivyo wanafahamika. Kwa silika yake ya uungwana, Warioba hawezi kujishusha kufikia ngazi ya siasa za maji-taka wanamoogelea hao waliokuwa wakimtukana wakati akifanya kazi aliyokabidhiwa na Rais wa Jamhuri. Hayo yote ni heko kwa Warioba, kwani yanadhihirisha kwamba katika jamii iliyofikia hatua ya kutokuwa na haya, bado tunao miongoni mwetu waungwana wachache waliobakia na haya, na wanaojizuia kujibu matusi ya wendawazimu kwa matusi mengine ya kiuendawazimu.

Hata hivyo, naamini kada huyu wa CCM amekosea pale anapowaambia wapinzani wasilitumie vibaya jina la muasisi wa nchi hii, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa kufanya kampeni zao. Nawakosoa wapinzani kwa matamko yao yanayoashiria kwamba CCM haijafanya lolote katika miaka hamsini iliyopita, kwani miaka hiyo inajumuisha pia kipindi cha utawala wa Mwalimu. Nakubaliana na Warioba katika mantiki hiyo: Yeyote anayemuenzi Nyerere hawezi papo hapo kusema kwamba hata yeye hakuna alilolifanya katika kipindi chake. Atakayesema hivyo atakuwa ama amepitiwa ama hajui asemalo, kwa kuwa sababu ya kumuenzi muasisi huyo ni kwamba kuna mambo mema na makubwa aliyoyatenda katika kipindi cha uhai wake, ikiwa ni pamoja na kipindi cha utawala wake.

- See more at: Raia Mwema - Tafakuri juu ya JK Nyerere, Warioba, CCM na Wapinzani

cc Pasco, Sikonge, MwanaDiwani, ZeMarcopolo, Adharusi, Zakumi, Mag3, Nyani Ngabu, Bukyanagandi, Kiranga, Alinda, Mwalimu, msemakweli
 
Last edited by a moderator:
warioba anajitambua
wakati wa kanda ya ziwa
tumeshaamua rais hawezi tokea kaskazini
 
Yeye na Polepole walewale tu. Mtu unashindwa kusimamia mabadiliko uliyoyataka kwa mbwembwe! Ni wachumia tumbo hatari kabisa kwa usalama wa nchi.
 
Yeye na Polepole walewale tu. Mtu unashindwa kusimamia mabadiliko uliyoyataka kwa mbwembwe! Ni wachumia tumbo hatari kabisa kwa usalama wa nchi.

..sidhani kama huyu mzee ni mchumia tumbo.

..huyu ana uungwana uliopitiliza. Sasa ccm wana-take advantage of him na kumfanyia mambo ya ajabu-ajabu.

..angekuwa siyo muungwana basi ungeona akichakachua maoni ya wananchi kuhusu katiba mpya.

..samuel sitta na sinde warioba ni wazee wa rika moja. Nadhani wamesoma pamoja, na wote walitumikia ktk serikali ya awamu ya kwanza.

..Sasa hebu linganisha mwenendo wao wakati wa mchakato wa katiba mpya. Definetely utakubaliana na mimi kwamba Mzee Warioba ni muungwana.
 
Warioba ana faidika na system ndio maana hawezi kutoka huko kirais. Unless astaafu kabisa kujishugulisha na mambo ya serikali.
 
Good loooking out son.

Kuna mambo fulani kayasema Ulimwengu nilikuwa nayasema all along humu. Labda kwa kuwa kayasema Ulimwengu sasa watu wanaweza kukubali zaidi.

Warioba is a bonafide old school gentleman.

Ndiyo maana mimi nasikitika sana nikiona watu wanamkosea heshima hiyu mzee kwa sababu tu kaamua kubaki CCM.
 
Warioba ana faidika na system ndio maana hawezi kutoka huko kirais. Unless astaafu kabisa kujishugulisha na mambo ya serikali.

Warioba kama angekuwa na motivation ya kufaidika binafsi, angegombea urais kwa tiketi ya UKAWA na watu tungempigia kuta kwa wingi bila matatizo wala maswali anayoyapata Lowassa sasa ambaye wengine hatuna imani naye.
 
JokaKuu, kiukweli Jaji Joseph Sinde Warioba amejitahidi kwa nafsi yake kusimamia anachoamini lakini naomba tusisahau kitu kimoja, sisi sote ni binadamu. Kama binadamu tunayo mapungufu ila tunachozidiana ni kiwango tu cha uvumilivu na ustahimilivu katika kuyasimamia yale tunayoamini ndiyo sahihi. Ni wachache ambao kwa hivi sasa wanapitia wakati mgumu kama Warioba kwani kajikuta kama wasemavyo wazungu; torn between a rock and a hard place.

Hii si mara ya kwanza huyu mheshimiwa anajikuta katika hali hiyo...hii inanirudisha miaka zaidi ya ishirini nyuma, 1995 wakati William Benjamin Mkapa anatangaza nia yake ya kuchukua fomu kugombea Uraisi mbele ya waandishi wa habari. Kushoto kwake alikaa Jenerali Ulimwengu na kulia kwake alikaa Joseph Sinde Warioba. Hebi jaribu kufikiria Warioba alijisikiaje ile siku Jenerali Ulimwengu ananyang'anywa uraia na serikali chini ya Benjamin William Mkapa.

Jaji Warioba alikaa kimya na hakutoa neno. Tuje 2015, wakati Jaji Joseoh Sinde Warioba anasulubiwa na vijana na wazee ndani ya CCM kwa kisa tu cha kujaribu kutetea alichoamini ni rasimu iliyowakilisha maoni ya wananchi aliyoitayarisha yeye. Watu alioamini wangejitokeza kumtetea na kusimama naye kidete katika jukumu alilojipa la kuzunguka mikoani kama alivyofanya wakati anakusanya maoni ya wananchi hawakujitokeza, walibana wakakaa kimya.

Tururdi tena nyuma kidogo hadi wakati kashfa zilizohusisha akaunti za Benki Kuu import/support na baadaye EPA, KAGODA na MEREMETA n.k. zimepamba moto. Jina la Warioba lilijitokeza kwa njia ya kampuni moja iliyoitwa Mwananchi Gold na ingawa moto wake ulikuja kutulia, yawezekana majivu yake yalihifadhiwa kuja kutumiwa muda muafaka ukifika. Hakuna kiongozi yeyote wa juu ambaye hakuwa na doa ndani ya CCM na hii silaha imetumika sama kuwaziba mdomo wengi.

Tunapofika hapa ndipo kwangu watu kama Lowassa na Sumaye nawaita wajasiri...serikali ina mkono mrefu na hakuna sababu yoyote kwa nini mtu anayedaiwa kuwa fisadi wa mafisadi hadi leo yuko huru mtaani akitafuta kura aweze kupata ridhaa ya kuliongoza taifa hili! Watu wanakwenda mbali hadi kudai kuwa maadam kwa sasa kahamia upinzani, dhambi zote za viongozi wa taifa hili, wa zamani na wa sasa hivi, kupitia CCM zimetakasika na sasa CCM ni safi! Hapana iko namna.

Mpaka dakika hii nakaa najiuliza kilichomsibu Dr. W. P. Slaa lakini pamoja na kushangaa natambua kwamba hakuna binadamu aliye safi kwa asilimia 100%, hapana, huyo ni Mungu tu. Ndiyo maana mimi naunga mkono kwa asilimia 100% mabadiliko ikiwa na maana ya kuuondoa huu mfumo na kuingia mfumo mpya...mabadiliko ni mabadiliko na tukubali tusikubali Watanzania hivi sasa wanataka na wako tayari kwa mabadiliko na wengi wanapoamua, hakuna wa kuzuia.

Jaji Warioba alikuwa raw model wangu kama alivyokuwa Dr. Slaa lakini kama wahenga walivyosema kukubaliana kwa watu wawili au zaidi kwa kila kitu muda wote, lazima kutie shaka. Niliafiki misimamo yao katika nyakati fulani fulani lakini kwa hapa tulipo kama taifa naamini wamepotoka ama kwa hiari au kwa kulazimishwa na hali halisi. Jenerali Ulimwengu kama anapita humu bila shaka anakumbuka yaliyompata alipoanza kutofautiana na serikali ya Mkapa.

Kwa waliocheza mchezo wa draft, kuna kuingizwa king kwa nguvu.
 
Back
Top Bottom