Jaji Sinde Warioba kanishangaza

Jaji Sinde Warioba kanishangaza

Njema kabisa

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
699
Reaction score
238
Ikumbukwe kuwa Jaji Warioba alikuwa akizunguka kutoa elimu ya uraia pamoja na kueleza wananchi jinsi maoni yao yalivyotupwa kwenye rasimu ya katiba jambo ambalo lilifanya atukanwe, adhihakiwe, adharauliwe na hata kudaiwa kupigwa.

Kilichonishangaza ni yeye kusimama jana na kupiga kampeni kwa wagombea, wakati kwanza chama hicho ndo kilihusika kusigina maoni ya wananchi, pili mmoja wa wagombea alikuwa makamu mwenyekiti bunge la katiba sasa Mh. Warioba ulikuwa unazunguka kufanya nini kwa wananchi ikiwa leo una wanadi waliosigina maoni ya wananchi?

Sikutegemea kwa kweli, sasa vipi ile rasimu ya wananchi ndo huitetei tena? Nimewaza kwa sauti wajamaeni.

Uwepo wa Jaji Warioba Jangwani wagongelea msumari wa ubatili wa UKAWA

Sote ni mashuhuda, kilichotokea siku ya Tarehe 23, katika viwanja vya jangwani kulipofanyika uzinduzi wa kampeni ya CCM kuelekea Uchaguzi wa oktoba 25.

Walikuwepo manguli wote wa siasa za Tanzania, akiwemo Jaji Mstaafu Warioba, ambaye alikua mwenyekiti wa Tume ya kuratibu maoni ya wananchi katika mchakato wa kupata katiba mpya.

Uwepo wake umekua wa faraja na umehitimisha safari ya uhalali wa vyama vinne vya upinzani vilivyounda umoja wao na kuuita UKAWA.

Dhana nzima ya Muunganiko huo kama wanavyotaka tuwaamini ilikua ni kupigania matakwa ya wananchi yaliyoratibiwa na tume, kabla ya kufanyiwa marekebisho na bunge na kutoa rasimu ambayo itapigiwa kura na kuamuliwa na wananchi.

Jaji mstaafu warioba, pamoja na kuzungumzia mengine, aliutaarifu uma kwamba atakuwepo kuipigia kampeni CCM katika uchaguzi wa oktoba 25.

Kauli hiyo ni nzito, na inamaana kubwa katika uhalali wa muunganiko wa Ukawa, kauli ya muasisi wa madai ya Ukawa, inatoa picha moja kubwa kwamba, watu hao hawaaminiki, na si watu sahihi katika kuhakikisha wananchi wanapata wanachokihitaji.

Ukawa ingepata Uhalali kama ingepata support ya nguli huyu wa siasa,lakini kwa kua amewakataa kwa kutojihusisha nao, sidhani kwanini sisi wananchi wa kawaida ambao hatupo karibu na hao watu tuwakubali.

Kifupi ni kwamba UKAWA imekufa na imepoteza uhalali wake kimantiki tokea siku ile ilipoanza kukumbatia watu wenye tuhuma mbali mbali kama watu wake wa karibu. Jambo hili si dogo na limemfanya mwasisi wa madai yao kuwakana hadharani.

Ni jambo la heri mno kwa Mh. jaji Mstaafu kuona kua kikundi hicho ni cha wababaishaji, na watumiaji wa uelewa mdogo wa wananchi katika mambo flani kujinufaisha kisiasa kwa malengo binafsi.

Ukawa haina pakusimamia, imekufa kabla hata ya Oktoba kufikia, tunashukuru kuona wazee kama hawa wakijitokeza na kuwaumbua hadharani hawa watu.
 
huyu si ndio maana alipigwa na makonda, asipoangalia atadundwa tena
 
Ikumbukwe kuwa Jaji Warioba alikuwa akizunguka kutoa elimu ya uraia pamoja na kueleza wananchi jinsi maoni yao yalivyotupwa kwenye rasimu ya katiba jambo ambalo lilifanya atukanwe, adhihakiwe, adharauliwe na hata kudaiwa kupigwa. Kilichonishangaza ni yeye kusimama jana na kupiga kampeni kwa wagombea, wakati kwanza chama hicho ndo kilihusika kusigina maoni ya wananchi, pili mmoja wa wagombea alikuwa makam mwenyekit bunge la katiba sasa Mh. Warioba ulikuwa unazunguka kufanya nn kwa wananchi ikiwa leo una wanadi waliosigina maoni ya wananchi???? Sikutegemea kwa kweli, sasa vipi ile rasimu ya wananchi ndo huitetei tena? Nimewaza kwa sauti wajamaen.

Amefnya hivyo kwa sababu gamba tayari limevuka, Fisadi hayupo tena CCM, Nachama kimebaki salama
 
Wallah walioba ni miongoni mwa Wa tz wasaliti.nashangaa nanazid kushangaa hili taiga Mzee kamahuyu nae!!!
 
Huyu Huyu Mzee Warioba Ndiye Alipigwa Na MaCCM Wenzake Kwa Sababu ya Kushaabikia rasimu yake ya Katiba. Leo Ni

Kimbembele wa Kuishaabikia CCM. Kweli CCM Ni Ile Ile..Do Hata Dr. Magufuli Hawezi Lolote Kwa MiCCM.
 
Njema kabisa
Hapo ndo utaona watanzania tuko tofauti duniani yule ni mwanasheria yuko vile je sie darasa hakuna tuko vipi ila huo ndo mfumo tuliojengewa watanzania ndo mana kenyatta alimwambia nyerere kuwa unaongoza maiti tanzania
 
Namuheshimu sana Jaji Warioba, lakini kwa hili la kukubali kutumika pamoja na kutukanwa sana na kupigwa kwa baraka ya chama hicho hicho, na bado akasimama nao jana linampunguzia sana heshima kwangu.. Nakumbuka Bulembo alivyomtukana huyu mzee and yet jana wakawa jukwaa moja..!
 
Uzee unachangia mambo mengi Warioba keshazeeka jamani Tumuache.
 
mtoto wake atapewa viti maalumu ni ahadi ... kazi zimekuwa issue now days
 
Msichoelewa ni nini katika huu wimbo? "CCM ni ile ilee, oo ni ile ile ileee... "
 
Nimepata jibu kelele za Humphrey Polepole hawa ndo waliokuwa wanamtuma!
 
Sikujua kama huyu mzee ni mnafki kiasi hiki; anaamua kusimamia masilahi ya chama anaacha masilahi ya Taifa!!!!? Hata hana uchungu wowote wa zile pesa za walipakodi alizozunguka nazo Tanzania nzima kukusanya maoni ya wananchi, duuuuuuh We are so foolish.!
 
Back
Top Bottom