Jaji Ramadhani: Nitatema nyongo baada ya Uchaguzi

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
48,776
102,136
Aliyekuwa mgombea urais CCM na kukatwa kwa madai kuwa hana maadili(Alikatwa na Kamati ya Maadili) amenukuliwa kuwa atasema ya moyoni baada ya uchaguzi.Hofu yake ni kuwa akisema leo atabadilisha upepo wa urais kabisa.Ikumbukwe kuwa Mh.Kinana alisisitiza kuwa waliokatwa ni makapi,hivyo hawatishiki nao.Hii ni wazi kuwa hakuridhika kwa maana angeridhika isingekuwa tabu kufagilia mchakato wa chama chake.
 
Kapi ni lowasa mwenye record ya kukataliwa ndani ya ccm, hana maadili ya kuendelea kubaki huko. Chama cha mapinduzi hakikuwa na muda wa kushughulika na wauuni. Kama mtu ni muhuni ataondoka wale ambao watakubaliana na mambo kwa maana ya kujua uongozi ni nini watabaki ccm nao ndio hakina Jaji Augustino
 
haa haa wale wote waliokatwa na ccm kule dodoma ni makapi. by kinanan
 
Aliyekuwa mgombea urais CCM na kukatwa kwa madai kuwa hana maadili(Alikatwa na Kamati ya Maadili) amenukuliwa kuwa atasema ya moyoni baada ya uchaguzi.Hofu yake ni kuwa akisema leo atabadilisha upepo wa urais kabisa.Ikumbukwe kuwa Mh.Kinana alisisitiza kuwa waliokatwa ni makapi,hivyo hawatishiki nao.Hii ni wazi kuwa hakuridhika kwa maana angeridhika isingekuwa tabu kufagilia mchakato wa chama chake.
Maliza kumsafisha fisadi lowassa ndo uhamie kwa ccm
 
Ni kweli ni kapi tu. Angelikuwa na lolote la maana ansingesema eti anaogopa kusema ili asibadilishe upepo w auraisi. Huyu ni kapi tena halifai. Hajitambui na hana uchungu na nataifa. Asingekuwa kapi, asinge sita kusema kweli yoyote anayoijua ambayo ingewafanya Watanzania waamue kuchagua kiongozi kwa busara kwa kutumia taarifa sahihi ili kujenga nchi.

Huyu ni kapi tu linaloenda na upepo, hana uchungu na nchi, hana ujasiri wa kufanya maamuzi na hana uwezo hata mdogo wa kuikomboa nchi. Kajaa unafisi na ubendera fuata upepo.

Kweli ni kapi tena lisilokomaa, na ambalo halifai. kusema baada a uchaguzi ni kuwazomea Watanzania na hila za kusababisha machafuko

M.baffu kabisa na kama nasemi sasa na anyamaze hata milele. Hatutegemei lolote jema kutoka ccm. Yote ni majambazi tu yamezoea rushwa na ku black mail.
 
Wasingeweza kupitishwa kugombea urais wote 40. Ilikuwa lazima apatikane mmoja wao katika wale wote. Hili lazima alijue na kila Mtanzania alijue
 
CCM imemdhalilisha sana huyu Jaji, yaani Makamba na Membe waliofungiwa kufanya siasa kwa mwaka mmoja ndio wenye maadili kumshinda huyu Jaji? Kweli CCM kiboko!

Sawa na fisadi Lowassa alivyowadhalilisha Slaa na Lipumba
 
Huyo naye ni mnafiki tu.Kama anajiamini na ana nyongo kwanini asiitoe kabla ya uchaguzi? Kwani yeye alikatwa lini na kuitwa makapi lini?
Ndio maana namheshimu Lowassa maana ni jasiri...ana uthubutu hamuogopi yeyote.
 
Kapi ni lowasa mwenye record ya kukataliwa ndani ya ccm, hana maadili ya kuendelea kubaki huko. Chama cha mapinduzi hakikuwa na muda wa kushughulika na wauuni. Kama mtu ni muhuni ataondoka wale ambao watakubaliana na mambo kwa maana ya kujua uongozi ni nini watabaki ccm nao ndio hakina Jaji Augustino
wewe nawe kapi lililosalia ccm,iko siku utachujwa na kutupwa ktk mtaro wa maji machafu kwa kuwa hata akili huna
 
Masikini Jaji Augustine Ramadhan, mwanzo alikataa kabisa kuchukua form kuwania urais, baadae wakamuomba sana wakimhakikishia ushindi
Leo hii anaishia kutukanwa kwa lugha mbaya na kuitwa kapi?!

This is too bad!
 
Achaneni nae huyo kwanza 'saizi yake tu' kuitwa. Yeye akubali tu kuwa kuwa hakuna jipya...Ameobwa (kwa staili ya kuingizwa mkenge 'kuhadaiwa' au kutumiwa bila ya kujitambua) kutumika kama mgombea...Kama alivyokuwa akitumiwa huku akijitambua kutumika kwa kutulea 'judgements' sizizo na mashiko na za hovyo before ikiwemo mgombea binafsi.

Kwanza alishajivua nguo siku nyingiii huyu wala si kumuonea huruma huyu....Waswahili husema "Muonsha Huoshwa" hivyo mwacheni aonje uchungu wa shubiri kama na yeye alivyokuwa akiwaonjesha watu kwa staili ya kutumiwa.
 
Kapi ni lowasa mwenye record ya kukataliwa ndani ya ccm, hana maadili ya kuendelea kubaki huko. Chama cha mapinduzi hakikuwa na muda wa kushughulika na wauuni. Kama mtu ni muhuni ataondoka wale ambao watakubaliana na mambo kwa maana ya kujua uongozi ni nini watabaki ccm nao ndio hakina Jaji Augustino

Mtashangaa mwaka huu..yaani tunawatahiri bila ganzi oktoba
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom