Jaji Mstaafu Kissanga asema rushwa inatisha mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Mstaafu Kissanga asema rushwa inatisha mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Oxlade-Chamberlain, Aug 5, 2010.

 1. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Jaji mstaafu, Dk. Robert Kissanga, ameelezea kukerwa na kukithiri kwa rushwa mahakamani na kusema kuwa baadhi ya mahakimu wamekuwa wakiandaa hukumu mbili kwa ajili ya kupendelea upande utakaotoa fedha nyingi wakati wa kusoma hukumu.
  Aliyasema hayo wakati akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalum nyumbani kwake Oysterbay jijini Dar es Salaam.
  Alisema baadhi ya mahakimu wasiofuata maadili wamekuwa wakiidhalilisha Idara ya Mahakama kwa kujihusisha na vitendo vya kuuza haki za watu.
  Alidai kuwa baadhi ya mahakimu hao wamekuwa wakiandaa hukumu mbili zote zikipendelea, hivyo yule ambaye anatoa fedha ndiyo hukumu inayombeba inasomwa mahakamani wakati wa hukumu.
  “Allegations (tuhuma) hizi ni za kweli kabisa ushahidi upo na ingawa kuzithibitisha ni vigumu lakini zipo, wapo mahakimu wasio waaminifu kabisa unakuta anaandaa hukumu mbili kisha anatoa 'signal' kuwa yuko tayari kutoa upendeleo kwa yeyote atakayetoa fedha na kweli yule anayetoa fedha ndiye inatolewa hukumu ya kumpendelea,” alisema.
  Alisema hakimu kuzungumza na upande wa mshitakiwa na mlalamikaji nje ya mahakama ni jambo linalojenga taswira ya rushwa na ni jambo lisilotakiwa katika maadili ya taaluma hiyo.
  Jaji Kissanga, alieleza kuwa kumeota tabia ya wenye fedha kununua haki za watu kwa kuhonga mahakama ili wapate upendeleo wanapokuwa na kesi mahakamani.
  Aliongeza kusema kuwa hata baadhi ya askari polisi wamekuwa wakati mwingine wakiuza haki za raia kwa kuwatoza fedha ili wapate dhamana vituo vya polisi wakati ni haki yao ya msingi.
  Alifafanua kuwa dhamana ni haki ya msingi ya kila mtuhumiwa, hivyo haoni sababu inayowafanya polisi kuwatoza fedha watu kwa ajili ya kitu ambacho ni haki yao.
  “Mtu akikamatwa na kufikishwa mahakamani kule anakuta mtandao wa rushwa, baadhi ya makarani, waendesha mashtaka na mahakimu wanahusika, mtu anaambiwa kabisa kwa kesi hii hapa hutoki labda tuzungumze vizuri ujinusuru. Huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za watu na lazima kifanyike kitu kuvikomesha,” alisema Jaji Kissanga na kuongeza kuwa wakati mwingine majaji ama mahakimu hawahusiki na vitendo hivyo ila wajanja wanatumia majina yao kujipatia rushwa.
  Jaji Kissanga hivi karibuni alitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Sheria na Chuo Kikuu cha Birmingham cha Uingereza, chuo ambacho alisoma miaka ya 1960.

  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Kazi hipo kwa tusiokuwa na uwezo wa kutoa rushwa nchi hii.
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Enzi za majaji marehemu Rugakingila, Mwalusanya na Jaji Kissanga pamoja na jaji mkuu mstaafu Samatta hadhi ya mahakama hasa High court ilikuwa juu sana; the court was not politicised because the appointments were by merit. Sio siku hizi inaelekea mahakama ni extension ya CCM.
   
 4. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hadhi na position ya mahakama iko juu siku zote. Ndio maana serikali haipendi kutoa mkono wake. Hata majaji wa sasa wengi wanachaguliwa by merit ila .tatizo ni wengi hawana ujasiri wa kukataa kuambiwa nini cha kufanya na inapokuja issue yenye maslahi ya serikali.

  Unaona wewe mwenyewe umetaja majaji watau tu. hao ilikuwa ni % ya majaji wakati huo. So utaona hataka kama kipindi cha kina rugakingira walikuwa wanachaguliwa on merit mbona hatukuwasikia wengine.Serikali iliwabana na inawabana hawa jamaa ni wachache wanaoamua liwalo na liwe.
   
Loading...