barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Kamishna wa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma Jaji mstaafu Salome Kaganda amewaasa viongozi wapya waliokula kiapo leo ambao ni baashi ya wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi zaidi ya 180 kuwa na maadili mazuri nje na ndani ya ofisi zao.
Jaji Kaganda anasema asilimia zaidi ya 90 ya wateule hao wa Rais ni vijana wadogo ambao wameaminiwa na Rais kuchukuwa kipindi hiki cha mpito, kutoka "Serikali ya Wazee kwenda Serikali ya Vijana" hivyo ni wajibu wao kuthibitisha kuwa sio kweli kuwa ngoma ya vijana haikeshi.
Amesisitiza kuwa Wakurugenzi wanawake wanatakiwa kuwa makini sana huko wanakooenda, isije ikafikia kila mtaa akipita basi watu wanajuwa aina ya sidiria alizonazo. Wanatakiwa kuwa na nidhamu ya mavazi na muonekano nje na ndani ya ofisi, amewataka viongozi hao wa kike kuweka mipaka kati ya mambo ya ofisi na kifamilia kwani kumekuwa na malalamiko ya waume wengi wa wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi kutumia magari ya serikali kwa mambo binafsi na pengine kuwaamrisha madereva wa serikali kuwapeleka sehemu kwa mambo yao binafsi. Jaji Mstaafu Kaganda amewasisitiza kuacha tabia hiyo kwani ni kinyume cha maadili ya utumishi wa umma.
Mama Kaganda pia amewakumbusha vijana wa kiume kujiheshimu, kuepuka rushwa za ngono ili kupandisha vyeo na wakati mwingine uhamisho au kupitisha likizo, kufanya hivyo ni kuvunja sheria na ni kosa la kifungo. Tabia ya kuwa kiongozi halafu ukipita mtaani unasikia mabinti wanasema "Yule DED anakoroma sana", maanake kuna siku ulikesha nae ndio maana anajuwa hata jinsi unavyokoroma. Watumie vizuri nafasi hizo kuwatumikia wananchi na si kuwanyanyasa.