Jaji Mkuu: Mahakama zisiendeshwe kwa Maelekezo

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
24,144
Reaction score
56,411

Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, George Masaju, amesema Mahakama haiwezi kuendeshwa kwa utaratibu wa kusubiri maelekezo, bali inapaswa kuongozwa na uwajibikaji na kujituma kwa kila kiongozi mwenye dhamana.

Akizungumza Februari 25, 2026 jijini Dodoma katika Kikao cha Mwaka cha Majaji Wafawidhi, Jaji Mkuu Masaju amesema viongozi wa Mahakama wanapaswa kutambua wajibu wao bila kusubiri kusukumwa na maelekezo kutoka juu.

“Hatuwezi kuishi kwa maelekezo. Sisi ni binadamu tuna akili na tunatambua wajibu wetu. Sisi ni viongozi wenye dhamana kubwa katika taifa hili, tunapaswa kuwajibika ipasavyo,” amesema.

Ameonya kuwa utamaduni wa kusubiri maagizo kabla ya kutekeleza majukumu unaweza kuharibu mahusiano ya kikazi na kushusha hadhi ya taasisi hiyo muhimu.

Aidha, Jaji Mkuu huyo amesema Mahakama inapaswa kuwa mfano wa uwajibikaji kwa taasisi nyingine, akisisitiza kuwa ndiyo kimbilio la wananchi wanapotafuta haki.

“Hii tabia ya kuzungumza kwenye vikao halafu wanaotakiwa kutekeleza wanasubiri kikao kingine, hatutakuwa na utamaduni wa namna hiyo,” amesema.

Ameongeza kuwa tangu aingie madarakani amekuwa akisisitiza suala la kujituma katika utendaji kazi, akieleza kuwa si sharti lake binafsi bali ni wajibu unaotokana na Katiba.
 
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, George Masaju, amesema Mahakama haiwezi kuendeshwa kwa utaratibu wa kusubiri maelekezo, bali inapaswa kuongozwa na uwajibikaji na kujituma kwa kila kiongozi mwenye dhamana.

“Hatuwezi kuishi kwa maelekezo. Sisi ni binadamu tuna akili na tunatambua wajibu wetu. Sisi ni viongozi wenye dhamana kubwa katika taifa hili, tunapaswa kuwajibika ipasavyo,” amesema.
Huyu naye ndiyo wale wale tu kwani hayo anayokataza ndiyo mtindo wa utendaji wa Mahakama zetu, mfano hai ni hii kesi ya ugaidi wa mchongo inayoendelea sasa hapo Mahakama Kuu laiti Majaji wanaoisikiliza wangekuea huru kesi ingeshaisha na Lissu kuachiwa huru lakini sasa hivi inaonyesha mawakakili wa Serikali ndiyo wamegeuka majaji wanachotaka ndiyo kinafanyika na majaji watatu wamekuwa wadogo kama Pirton.
 
Hili Ndio tatizo la wengi waliopewa dhamana kuongoza.
Sasa analalamika au
Badala ya kuwawajibisha wanaopokea maelekeza anatoa sijui ushauri, hata hieleweki
Woga huu wa kutupia vijembe Ndio maana wengi hutimuliwa

Kama kuna kitu unalimaliza kwa cheo chako bila kuzunguka bushes
 
Anaenda kinyume na mfumo, anaongea kama Simbachanwene aliyetumbiliwa.

Samia is outraged.

Ana hasira kali sana na huyu mtu

Kumtoa hawezi.

Samia alidhani anamjua vizuri na hatamgeuka wa saab siku za nyuma alishampaga kahongo ka kuwa Mwanasheria wa Ikulu.

Masaju ana balls za kuongea hivi kwa saab anajua Samia kaingia mkenge na kumtoa hawezi.
 
Uongozi ni ujasiri wa kufanya maamuzi magumu na sometimes hata kuingia kwenye hatari ya kupoteza cheo ulichonacho. Hongera sana mkuu umeliweka vizuri sana. Ila aungwe mkono hata kwa hilo dogo alilonalo. Kumbukumbu/Historia itambeba kwamba aliwahi kusema. Anaongoza muhimili muhimu sana kwenye maisha ya watu.
 
Hana lolote; huyu ni wale wale judge kazi maalumu!
 
Wakuielekeza mahakama kwa sasa kama siyo Samia ni nani? Yaliyotokea Oct 29 2025 pamoja na kesi aliyopewa Lissu vimeonesha udhaifu wa awamu ya sita.
Huyu Jaji anatutapeli tu. Kama yuko serious afanye kwa vitendo. Kesi ya Lissu toka Kisutu unaona kabisa inaendeshwa kwa maelekezo na hajafanya kitu. Ngoja tusubiri hiyo rufaa ya Katuga tuone itachukua muda gani.
 
Huyu Jaji anatutapeli tu. Kama yuko serious sfanye kwa vitendo. Kesi ya Lidsu toka Kisutu unaona kabisa inaendeshwa kwa maelekezo na hajafanya kitu. Ngoja tusubiri hiyo rufaa ya Katuga tuone itachukua muda gani.
Hawa watu wamejaa hadaa na ulaghai kiasi kwamba kila wanaposema jambo, tafsiri yake ni lazima iwe kinyume na wanayoyatamuka.

Maneno ni mengi sana wanayosema, lakini matendo juu ya hayo maneno huoni hata moja!

Polisi siku hizi wakitoa tangazo, kama wewe siyo mtu unayeishi nchi hii, ukisoma kilichoandikwa utatamani sana uje kuishi ndani ya nchi ambayo polisi wanafanya kazi kufuatana na maelezo ya matangazo yao.

Nadhani watawala waovu hawa wameamua kutumia mtindo huu wa kutawala kama ndiyo mbinu inayowawezesha kuendelea kukaa madarakani.
 
Hana lolote; huyu ni wale wale judge kazi maalumu!
Hivi kwani haya maneno anamweleza nani hasa; na analenga nini?

Jaji Mkuu, si ndiye yeye mkuu wa eneo hilo?

Yeye anao wasaidizi wake wanaomsaidia kupanga mahakama iendeshwe kwa misingi ipi.
Wao ndio wanaofanya mipango yao yote ya sekta yao, na kuwashirikisha wote kwenye sekta hiyo jinsi ya kufanya shughuli zao.

Sasa anamweleza nani haya maneno.

Kama kuna ukiukwaji wa taratibu katika utendaji katika ngazi yoyote hawana njia ya kurekebishana wao kwa wao?

Anatangaza hadharani kuwa hana uwezo wa kuendesha eneo lake hadi atafute njia ya kujivua lawama hadharani?

Amwajibishe yeyote aliyekiuka misingi waliyojiwekea, halafu tuone huyo anayewaingilia atafanya nini. Hapo waTanzania watakuwa na uhakika wa anayojaribu kueleza hapa.
 
Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, George Masaju, amesema Mahakama haiwezi kuendeshwa kwa utaratibu wa kusubiri maelekezo, bali inapaswa kuongozwa na uwajibikaji na kujituma kwa kila kiongozi mwenye dhamana.

“Hatuwezi kuishi kwa maelekezo. Sisi ni binadamu tuna akili na tunatambua wajibu wetu. Sisi ni viongozi wenye dhamana kubwa katika taifa hili, tunapaswa kuwajibika ipasavyo,” amesema.
Actions speaks louder than words!
 
Hivi kwani haya maneno anamweleza nani hasa; na analenga nini?

Jaji Mkuu, si ndiye yeye mkuu wa eneo hilo?

Yeye anao wasaidizi wake wanaomsaidia kupanga mahakama iendeshwe kwa misingi ipi.
Wao ndio wanaofanya mipango yao yote ya sekta yao, na kuwashirikisha wote kwenye sekta hiyo jinsi ya kufanya shughuli zao.

Sasa anamweleza nani haya maneno.

Kama kuna ukiukwaji wa taratibu katika utendaji katika ngazi yoyote hawana njia ya kurekebishana wao kwa wao?

Anatangaza hadharani kuwa hana uwezo wa kuendesha eneo lake hadi atafute njia ya kujivua lawama hadharani?

Amwajibishe yeyote aliyekiuka misingi waliyojiwekea, halafu tuone huyo anayewaingilia atafanya nini. Hapo waTanzania watakuwa na uhakika wa anayojaribu kueleza hapa.
Masaju ni mnafiki sana. Judiciary branch inayojitambua haiendeshi mambo yake kwa style hii.
 
Uongozi ni ujasiri wa kufanya maamuzi magumu na sometimes hata kuingia kwenye hatari ya kupoteza cheo ulichonacho. Hongera sana mkuu umeliweka vizuri sana. Ila aungwe mkono hata kwa hilo dogo alilonalo. Kumbukumbu/Historia itambeba kwamba aliwahi kusema. Anaongoza muhimili muhimu sana kwenye maisha ya watu.
Ni kweli kabisa ulichokiandika Mkuu.
Kwa nchi zetu ni vigumu kuwa mkweli na muwazi
Na ukifanya hivyo utakosa ajira na hata kusumbuliwa kisa Ukweli.

Ila kaweka wazi kiaina
 
Back
Top Bottom