Jaji Mkuu aomba bajeti zaidi kwa Mahakama.................. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Mkuu aomba bajeti zaidi kwa Mahakama..................

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Dec 23, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 416,608
  Trophy Points: 280


  Jaji Mkuu aomba bajeti zaidi kwa Mahakama

  Imeandikwa na Hellen Mlacky, Bagamoyo; Tarehe: 22nd December 2010 @ 22:56

  JAJI Mkuu Augustino Ramadhani ameiomba Serikali kuongeza bajeti ya Mahakama ili kuiwezesha kuboresha miundombinu na shughuli za utoaji haki katika mahakama zote nchini.

  Jaji Mkuu aliyasema hayo juzi wakati akizindua Mahakama ya Mwanzo Kerege iliyopo Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani iliyogharimu Sh 203,100,000 zilizotolewa na Serikali kupitia bajeti ya Mahakama ya Tanzania.

  Alisema kwa sasa Mahakama inapata asilimia 0.5 ya Bajeti ya Serikali, kiwango alichosema ni kidogo kushinda hata bajeti ya mkoa.

  “Mahakama tunapokea bajeti ndogo sana kwa mwaka ya kuhudumia mahakama zote nchini ikilinganishwa na mkoa ambao ni mdogo unaohudumia wananchi… sisi tuna matawi katika kila wilaya na mara nyingine kata kwa hiyo bajeti hii ni ndogo sana,” alisema Jaji Mkuu.

  Alisema pamoja na hayo, lakini kwa sasa wana matumaini kwamba wataboresha mhimili huo wa Dola kwa sababu mwakani wataanzisha Mfuko wa Mahakama ambao unategemewa kutekeleza mambo mengi na kuiomba serikali kuchangia asilimia mbili ya bajeti katika mfuko huo.

  “Mahakama ya Tanzania kwa kutambua hali ya miundombinu, hususani majengo ya mahakama zetu hapa nchini, imeweka sera ya kujenga majengo yenye kukidhi mahitaji yote yanayoambatana na shughuli za utoaji haki katika mahakama zetu,” alieleza Jaji Mkuu.

  Aidha, alisema katika mwaka huu wa fedha, Mahakama ya Tanzania inakusudia kuanza kujenga majengo ya namna hiyo katika wilaya za Kibaha, Kisarawe, Kinondoni, Temeke, Bariadi, Bunda, Tabora, Nkasi, Mpanda, Ilala, Mwanga, Kilosa, Korogwe, Masasi, Simanjiro, Monduli, Mufindi, Chunya, Mwanza na Songea.

  Mapema Jaji Mfawidhi Kanda ya Dar es Salaam, Semistokes Kaijage alisema Mahakama ya Mwanzo ya Kerege ilianza kujengwa Juni 25, 2007, lakini ilishindwa kukamilika mapema kutokana na changamoto mbalimbali ikiwamo majambazi waliovamia eneo la mradi huo na kumuua mlinzi na kuiba vifaa vya ujenzi.

  Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Absalom Mwakyoma, alisema kujengwa kwa Mahakama hiyo kutapunguza gharama ya kusafirisha mahabusu zaidi ya kilometa 30 kama ilivyokuwa awali na pia itapunguza uhalifu wa wizi wa mifugo.

  Uzinduzi huo wa Mahakama ya Mwanzo Kerege ambayo ni ya mfano na pili kuzinduliwa baada ya kuzinduliwa kwa Mahakama ya Mwanzo Msoga/Lugoba, ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwamo pia Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Amina Mrisho.


   
 2. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160

  Nani atasikiliza hiyo kesi wakati aliyeibiwa ndie muamuzi wa kesi yenyewe, changamoto kwa great thinkers
   
Loading...