Jaji Manento akiri Mwangosi alipigwa risasi na askari

Jaji Manento akiri Mwangosi alipigwa risasi na askari

JipuKubwa

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2013
Posts
2,342
Reaction score
2,390
Akiongea katika viwanja vya Ikulu,Jaji Amiri Manento amekiri jambo gumu ambola Tume ya Haki za binadamu na utawala bora imesimamia kwa nguvu ni sakata la kifo cha Mwangosi.

Na amekiri serikali haijafanyia kazi mapendekezo ya tume hadi leo.

Jaji akumbusha machungu kifo cha Daudi Mwangosi

kaka1-550x280.jpg
MWENYEKITI wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) aliyemaliza muda wake, Jaji Amir Manento, ameonyesha kutofurahishwa na Serikali kushindwa kutekeleza ripoti iliyotolewa na tume hiyo kuhusu mauaji ya mwandishi wa kituo cha Channel Ten mkoani Iringa, Daudi Mwangosi.

Jaji Maneto aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana, wakati wa hafla ya kuapishwa kwa mwenyekiti mpya wa tume hiyo, Bahame Nyanduga na makamishna wake.
"Pamoja na kustaafu, jambo ambalo sitalisahau ambalo linaumiza kichwa changu ni namna ambavyo Serikali imeshindwa kutelekeza ripoti ya mauaji ya Mwangosi.

"Wananchi walipokea vizuri ripoti yetu, lakini nasikitishwa ambavyo viongozi wa Serikali walivyoshindwa kulichukulia hatua jambo hili, wakiona ni mwiba kwao," alisema.

Alisema ripoti hiyo kwa sehemu kubwa ilionyesha namna ambavyo watendaji wa Serikali walionyesha uzembe uliochangia kuuawa kwa Mwangosi.

"Kucheleweshwa kwa haki ya Mwangosi, kisheria ni sawa na kumnyima haki yake, katika sheria tunatambua suala la kucheleweshewa haki ni sawa na kunyimwa haki kwa mhusika," alisema.

Pamoja na haki hiyo kucheleweshwa, Jaji Manento anaamini huenda Mwenyekiti mpya Nyanduga, atasimamia pale walipokuwa wamelifikisha wao ili haki ipatikane.
Mwangosi, aliyekuwa mwandishi wa habari wa Chanel Ten Mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa mkoa huo, aliuawa Septemba 2, 2012 kwa kitu ambacho kinasaidikiwa kuwa ni bomu.

Katika tukio hilo, Mwangosi alikamatwa na zaidi ya polisi watano, huku mmoja akionekana kumnyoshea bunduki sehemu za tumbo lake.
Tukio hilo, lilitokea katika Kijiji cha Nyololo wakati alipokuwa akitimiza wajibu wake kwenye uzinduzi wa tawi la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Tume iliwahusisha maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Said Mwema.

Katika ripoti ya tume hiyo iliyokuwa chini ya Jaji Manento, ilionyesha kulikuwa na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora na kushauri kwamba ili kuwapo kwa utawala bora mamlaka zote za Serikali ni lazima zifuate utawala wa sheria.

Katika taarifa yao ilibaini aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda, Septemba 2, 2012 katika utekelezaji wa majukumu yake alikiuka Sheria ya vyama vya siasa (Cap 258 RE. 2002) kifungu cha 11(a) na (b) na sheria ya Polisi (Sura ya 322) kwa kuingilia kazi za OCD wa Mufindi na kutoa amri ya kuzuia shughuli za Chadema wakati hakuwa "Officer In-charge" wa polisi wa eneo husika.

"Kwa maana hiyo, amri aliyoitoa haikuwa halali kwa kuwa ilitolewa na mtu ambaye hakuwa na mamlaka kisheria wa kuitoa. Haya ni matumizi mabaya ya mamlaka, hivyo ni ukiukwaji wa misingi ya utawala bora," ilisema sehemu ya taarifa yao.

Wengine walioapishwa na Rais Kikwete jana ni Iddi Ramadhani Mapuri anayekuwa Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo.

Vile vile aliwateua makamishna ambao ni Rehema Ntimizi, Mohamed Hamadi, Salma Ali Hassan na Dk. Kevin Mandopi.

Kabla ya kuwaapisha, Rais Kikwete alianza kumuapisha Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Katarina Revocati.

Chanzo: Mtanzania
 
Hawa nao wanatuchanganya tu!! Siku zote hizo alikuwa wapi??japo hata kupaza sauti kuwa mapendekezo ya tume yake juu ya suala hilo hayajatekelezwa, anasubiri hadi muda wake uishe ndio anaibuka!!! Au ni kulinda mafao, hapo ndipo tofauti ya wasomi wetu na wengine hata kenya tu!!
 
Siku zote ukweli Lazima uwe hadharani,hata kama uchelewe.......aibu kwa SERIKALI.
 
Mchange akamatwe na polis!!!!....
 
Hayo ya Mwangosi yameshapita. Tugange yajayo
 
Damu ya mtu haipotei bure..

Ukiua hata ukijificha miaka kibao ipo siku ukiwa usingizini utaota na kupaza sauti kuusema ukweli
Kama si usingizini basi ulevini na kama si ulevini basi uchizini!! Utaokota makopo na kinywa chako kitanena uovu
Mtaufunika ukweli lakini roho zitawasuta

Hongera Judge Ameir Manento kwa kuutua mzigo lakini hiyo ndio serikali uliyokuwa ukiitumikia

Nathubutu kusema kuwa CCM ni kama kutangaza kuwa wewe si Muislamu ni KAFIRI na pia sio Mristo na MPAGANI

Maana hakuna muislamu wala mkristo anasimamia maovu kama mauaji ya mtu asiye na hatia na kuyatetea na kukanusha....yule mjane..wale watoto...hebu jiwekeni nafasi hiyo mngekuwa nyinyi!

Hivi kweli maisha ya mtu kisa siasa zenu za dhulumati na eskelewuu(escrow)?????
 
Hayo ya Mwangosi yameshapita. Tugange yajayo
hebu ficha utupu wa kichwa chako wewe mpinga EL, kumbuka ni maisha ya mtu hayo yamepotea,jaji anaongea vitu vya msingi,unajidai tugange yajayo, waliohusika wachukuliwe hatua,wapi Kamuhanda???
 
Hayo ya Mwangosi yameshapita. Tugange yajayo

Hata baada ya miezi yote hii bado mtu huyu hajapata uwezo wa kuamua ya kuandika. Hajui ni yapi yenye kuinufaisha jamii.
nahisi hata akilawitiwa, atasema tugange yajayo ili aendelee kulawitiwa.
 
Kwa kauli hiyo ya Jaji Manento, tafsiri yake ni kuwa kiongozi wa operesheni ya 'ondoa uhai wa Mwangosi' kamanda Kamuhanda, aliyekuwa RPC wa İringa wakati huo wa mauaji ya Mwangosi, pamoja na vijana wale mapolisi waliomlipua Mwangosi, kwa kutii amri hiyo ya 'kiuendawazimu' ya kamanda wao wanapaswa kupandishwa kizimbani haraka iwezekanavyo.
 
Tusivunje sheria kwa ahadi hewa tunazopeana na kudanganyana tutalindana. Mambo yanabadilika...na yanabadilika kwa kasi. Tujifunze kufanya mambo kama watu tunaojua tunataka kwenda wapi. Pole zao waliohusika....hata kama itachukua miaka kadhaa...it is in the record!
 
Siku zote penye ukweli, uongo hujitenga.

Wanajisikiaje sasa akina Chagonja, ambao mara tu baada ya mauaji yale, walijitahidi sana kuihadaa dunia, kuwa eti waliosababisha kifo cha Mwangosi, ni mashabiki wa Chadema, waliorusha kitu chenye ncha kali, kilichoyaondoa maisha ya Mwanahabari Daudi Mwangosi!
 
Back
Top Bottom