Jaji Lubuva Asema Sheria Inawaruhusu Raia Mita 200

Jaji Lubuva Asema Sheria Inawaruhusu Raia Mita 200

Kukaa mita 200 lazma hata kama mahakama itanyonga haki,maccm kama yanaibiana kura wao kwa wao yanashindwaje kuiba za ukawa??!!
 
Bahati nzuri kutoka kituo cha kupiga kura mita 200 zimegota barazani kwangu,kwahiyo nitakaa bila bughuza nikiwa na ndugu jamaa na marafiki tukisubiri matokeo ya kituo changu cha uchaguzi.
 
Mimi kituo kiko maeneo ya jeshi nikimaliza naenda lala tu
 
Halafu kampuni za uwakili ziko kibao, na ndiyo fani pakee wanatembea wameniga tai na suti hata kama jua linawaka vipi.
 
Wanasheria wetu wote wameshindwa kuitafsiri sheria yetu wenyewe ya uchaguzi inayohusu mita 200 baada ya kupiga kura, hiki ni kichekesho kikubwa kwa taifa. Kila mtu anasema kivyake utadhani hii sheria tuliirithi kutoka kwa wakoloni.

Sio mwenyekiti wa tume, msajili, Jaji mkuu, mwanasheria mkuu, majaji wala mawakili asiye mung'unja maneno kuhusu sheria hii. Ombwe la wanasheria kwenye sheria hii linasababisha wanasiasa na raia kuingia kwenye mkanganyiko. Hii inaleta mashaka makubwa juu ya TUME kama iko huru au haiko huru, ina weledi au haina.

Tusisababishe ICC kuja kututafsiria sheria yetu wenyewe iliyotungwa na bunge letu wenyewe na kutiwa saini na Rais wetu wenyewe
Tofauti ya ukoloni wa babu zetu ni kuwa haukuwa wa hiari kama ilivyo leo watu wanakwenda na barua za maombi ili wawatumikie WAKOLONI
 
Sheria iko wazi kuwa ni mita 100 .... kwa usalama zaidi wanasema mita 200 ... CCM hawataki kuwaona Raia wamekusanyika kwani idadi yao itaashiria jinsi ambavyo mshindi atapatikana ..
 
Nyumba yangu ipo ndani ya mita 10 tu toka kituo kilipo, naomba ufafanuzi kwa kutumia sheria hii ya mita 100 na kanuni ndogo ya mita 200 tafadhali.
 
Sasa ubishi uishe, tunayo kazi moja tu watanzania kwa sasa nayo ni kuiondoa ccm madarakani, uwezo wa kuiondoà tunao, sababu ya kuindoa tunayo na nia ya kuindoa tunayo pipoooooooooooz

Powereeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeerrrrrrrr
 
Baada ya zoezi la kulinda kura kugonga ukuta. Tusishangae kuambiwa kura Milioni Tatu zimeharibika kuruhusu bao
la mkono. Njia hii itatumika kufanya goli la mkono. Kura zilizopigiwa Ukawa zitatikiwa mara mbili kuonyesha kuwa
zimeharibika au kura zingine kutohesabiwa kuonyesha kuwa wapigaji hawajajitokeza. Jamani Ukawa hakikisheni mawakala wenu hawanunuliwi..!! Nawakilisha..!
 
Kwani mahakamani imekuwaje au bado? Lakini lugha ya KULINDA kura naamini itakuwa kikwazo. Tungeshtuka mapema tukatumia neno lingine, lakini hili la KULINDA halijakaa sawa. Bora tungesema TUKAE mita .... Hii isingekuwa na ukali ( Kulinda ) linaweza kutukosesha penalty
 
Hali imekua tofauti vitisho vinavyotolewa na serikali ya CCM kuhusu kulinda kura nje ya mita 200 vimeingia sura mpya, kwani imezuka hofu kubwa wengine wakianza kurudi vijijini wengine sidhani hata kama watakwenda kupiga kura.

Uchaguzi huu utapigwa kura na vijana wengi na wanaume wengi, haya magari ya washa washa wanayoyaonyesha yanawatia hofu wakina mama na wazee na sijui kama watajitokeza kwa hali hii inayotokea sasa.
 
Sauti ya wengi ni sauti ya mungu, sauti ya mungu hapa bongo Mwaka huu inataka mabadiliko. CCM hoi.........
 
Hilo suala nililiona mapema,Wazee wengi wameingiwa na hofu,baada ya kuona hizi purukushani za polis.Sasa tutabaki vijana tu.Huu ni mbaraka mkubwa sana
 
Mkuu ni kweli kuna familia moja hapa jijin mwanza iko karibu na shule...wamesema watasafiri kwenda kijini baada ya kupiga kura jumapili asubuhi
 
Hali imekua tofauti vitisho vinavyotolewa na serikali ya CCM kuhusu kulinda kura nje ya mita 200 vimeingia sura mpya, kwani imezuka hofu kubwa wengine wakianza kurudi vijijini wengine sidhani hata kama watakwenda kupiga kura.

Uchaguzi huu utapigwa kura na vijana wengi na wanaume wengi, haya magari ya washa washa wanayoyaonyesha yanawatia hofu wakina mama na wazee na sijui kama watajitokeza kwa hali hii inayotokea sasa.
Nadhani imethibika wazi wameshajua wameshindwa!
 
Back
Top Bottom