GE2025 Jaji: Hakuna amri ya Polisi kufukuza wafuasi wa CHADEMA Mahakamani katika Kesi ya Tundu Lissu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,498
Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala ndogo ya Dar es Salaam imetupilia mbali hoja iliyokuwa umewasilishwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uhaini, ambaye alidai kuwa Polisi kupitia amri ya ZCO waliwatoa watu (viongozi na wafuasi wa CHADEMA) waliofika Mahakamani hapo kusikiliza mwenendo wa kesi inayomkabili

1758014214802.png

Hoja hiyo ambayo ilipelekea jopo la Majaji watatu wanaosikiliza kesi hiyo wakiongozwa na Jaji Danstan Ndunguru kuhairisha kesi kwa muda ili kutolea uamuzi/ muongozo, sasa Mahakama imerejea na Majaji wanasema hakuna amri yoyote ya aina hiyo iliyotolewa Mahakamani hapo

Soma > Wafuasi wa CHADEMA wasusa kusikiliza kesi ya Lissu baada ya wenzao kuzuiwa kuingia ndani ya Mahakamani

Katika maelezo yake Jaji Ndunguru amesema katika ufuatiliaji wake Mahakama imebaini hakuna amri yoyote iliyotolewa inayotaka watu watoke kwenye chumba cha Mahakama

Sambamba na hilo Jaji Ndunguru amesema wakati Majaji wanaingia waliona baadhi ya watu wakitoka kwenye chumba cha Mahakama na kwamba kwa wakati huo hawakuona mtu/ watu waliokuwa wakitoa amri ya kuwafukuza

Mahakama pia imetoa wito kwa wadau wake wote kutambua kuwa chumba cha Mahakama kina idadi ya watu inayotosheleza, na si kweli kwamba wote watakaofika Mahakamani wanaweza kutosheleza kuingia kwenye chumba cha Mahakama

Lakini pia, Mahakama imetoa wito kwa wadau wote kutumia utaratibu uliotumika juma lililopita ambao ulikuwa rafiki kwa watu wote kufuatilia bila kikwazo chochote,

Aidha, Mahakama imetaka pande zote/ wadau kutafuta suluhu ya mapema pale inapotokea sintofahamu kama hiyo au ya aina yoyote ile, itafutwe suluhu kabla Majaji hawajaingia kwenye chumba cha Mahakama

Baada ya uamuzi huo, sasa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu inaendelea.

Watanzania mtatafuta ushahidi ganj zaidi kujua kuwa MAHAKAMA ni sehemu kandamizi kwa kushirikiana na Executives?
 
Kwa hiyo yule polisi aliyekuwa anazuia watu kwa nguvu zake zote hana kazi kwa leo!
 
Inawezekana awatumwi ila wanajiongeza kufurahisha watawala
 
Back
Top Bottom