TANZIA Jaji Haji Omar Haji afariki dunia

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,246
24,108
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mh. Dr. Hussein Ali Mwinyi leo ameongoza mazishi ya Jaji Haji Omar Haji huko mkoa wa Mjini Magharib Unguja Zanzibar.


Jaji Omar Haji​

Mazishi yalihudhuria halaiki kubwa ya watu pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali, mahakama na vyama vya siasa. Marehemu alifariki ghafla baada ya kuumwa kwa muda mfupi.



Marehemu Jaji Haji Omar Haji pia aliwahi kuwa Mtendaji wa Mkuu Mahakama ya Africa Mashariki ( EACJ administrator) kati ya mwaka 2018 mpaka 2021 kabla ya kuteuliwa na Mh. Rais Hussein Mwinyi kuwa jaji Zanzibar.

Marehemu Jaji Haji Omar Haji aliteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar mnamo Februari 01, 2021 na kuapishwa mnamo Februari 08, 2021.

Marehemu alizaliwa 4 June 1967 katika kisiwa cha Mafia mkoani Pwani kabla ya kuhamia Zanzibar 1985 kwa masomo ktk skuli ya sekondari Lumumba, kisha kuendelea na masomo ya juu katika Chuo cha Mzumbe Morogoro kusomea sheria. Baadaye alisomea shahada ya sheria kati vyuo vikuu vya Zanzibar na Afrika ya Kusini. Marehemu ameacha kizuka na watoto wanne.

Source : Zbc Zanzibar
 
Corona itatumaliza tupate chanjo jamani. Halafu inachagua wasomi na matajiri tu, makapuku inawaruka
 
Corona itatumaliza tupate chanjo jamani. Halafu inachagua wasomi na matajiri tu, makapuku inawaruka
Kapuku atakusikia nani wewe? Wanakufa kama panzi but who cares? Halafu ndio wabishi wa chanjo sumu waliyolishwa ni hatari sana.
 
Poleni mno kwa wafiwa ALLAH awapeni unafuu kwenye kipindi hiki kigumu kwenu,je kuna yeyote mwenye baadhi ya cases alizoamua marehemu ili tuweze kuenzi legacy yake aliyotuachia
 
Back
Top Bottom