Jaji Augustino Ramadhani ni Msafi, hachafuki hata kama akimwagiwa tope, tafuteni sababu nyingine

shikulaushinye

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
828
456
Watanzania wenzangu tunapita katika kipindi kigumu kupata mtu sahihi anayefaa kuwa rais wetu. Katika kipindi hiki kuna makundi yamepewa pesa kuwachafua baadi ya wagombea.

Makundi haya yanatafuta kila sababu ya kumchafua Jaji Augustino Ramadhani, kwa kuwa hawana hoja, kwani Jaji Ramadhani hachafuki, wanatafuta visababu visivyo na kichwa wala mkia.

Hoja ya kwanza ilikuwa eti majaji na wanajeshi hawaruhusiwi kuwa wanachama wa vyama vya siasa. Mzee wa watu kawajibu mara moja tu hoja hiyo inaonekana nyepesi, majibu yake yalikuwa kama ifuatavyo:-

Alipohitaji kujiunga na jeshi akiwa anasoma UDSM, alijiunga na TANU na kusitisha uanachama mwaka 1992 ili kukidhi mahitaji ya katiba.

Swali: Je, Jaji Ramadhani ni yeye pekee ambaye aliwahi kugombea nafasi ya rais huku akiwa mwanajeshi au jaji? Rais Kikwete ni mwanajeshi mstaafu na aligombea mwaka 2005 na sasa ni rais wetu anayemaliza muda wake. Hata jaji Ramadhani alikuwa mwanajeshi na jaji, sasa ni mstaafu kama Kikwete. Tafuteni hoja nyingine hii imeshindwa.

Wakora wametafuta hoja nyinge, eti Jaji Ramadhani amevunja kiapo cha kanisa la Anglican Tanzania. Kanisa la Tanzania siyo kanisa la Anglo Catholic Church kama baadhi wanavyodai, kanisa la Anglican limesajiliwa Tanzania kama Anglican Church of Tanzania na sio Anglo Catholic Church.

Pia ya MUNGU mpeni MUNGU na ya Kaisari mpeni Kaisari. Pia Biblia inatambua kuwa mamlaka zote zinatoka kwa MUNGU" Warumi 13:1-7 "Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu". Haiwezekani MUNGU atambue Mamalaka za juu harafu watumishi wa MUNGU wasiruhusiwe kuwa viongozi.

List of Anglo-Catholic churches From Wikipedia, the free encyclopedia
This is a list of Anglo-Catholic parishes and missions within the Anglican Communion that are considered notable.

Set by Contents
1 Australia
2 Brazil
3 Canada
4 New Zealand
5 United Kingdom
6 United States

Katika orodha hiyo hapo juu, hakuna hata nchi moja ambayo ipo chini ya Anglo-Catholic churches ambayo canon law ya 1734 ac number 4559 imekuwa quoted na baadhi ya team za wa wagombea.

Tafuteni sababu nyingine hii imeshindwa.
 
Swala la uanajeshi halipo,lilopo kwa sasa yeye ni KASISI wa kanisa aka kiongozi wa kanisa na sheria inataka moja either aache UKASISI ili awe mwanasiasa au aache Siasa ili aendelee kuwa KASISI achunge kondoo zake vyema.
 
Mkuu ni kweli lakini mbona jamaa amekueleza hapo juu chini hiyo jamaa waliquote siyo law kanisa la ANGLICAN Tanzania halipo kwenye hiyi CANON LAW? Pia hatuwezi fahamu mpaka kufikia uamzi huu kama kapata baraka za uongozi wa wa juu wa Kanisa. Lakini pia sisi kama Watanzania linatuzuia nini au linatuhusu nini akiwa rais wetu?

Hayo ni mambo ya ndani ya Kanisa, watayatatua wenyewe. Hayo ni mayowe ya wapambanaji tu, lakini hayana madhara. Wapo wachungaji wengi waliopo kwenye siasa, kuna mchungaji Lwakatare, mchungaji Msigwa na wengine. Mbona watu hawakupiga kelele kwa hao?
 
Kwa sasa ni Rais wa mahakama ya Afrika ya haki za binadamu Arusha, Jaji Ramadhani alikuwa na mpango wa kutumikia kanisa kama kasisi baada ya kustaafu lkn akateuliwa kwa nafasi hiyo, mpaka sasa hana hajakabidhiwa kanisa la kuhudumia, ukassisi aliopewa na daraja la ukasisi na siyo kuteuliwa kusimamia kanisa fulani kama ilivyo kwa PENGO AU RWAKATALE. kwa wale wasio fahamu KASISI ni daraja ndani ya kanisa nyingine ni KATEKISTA, SHEMASI ASKOFU NA NK.
 
Tukitaka pure clean ni; 1. Makongoro Nyerere 2. Prof Mark Mwandosya 3. Jaji Ramadhani 4. Dr. Asha Rose Migiro 5. Dr Gharib Bilal kwisha wengine wote ni reject.
 
Kasisi ni nani? Nadhani ulikuwa unajaribu kusema hajapewa bado majukumu ya kulea kanisa/parish (yaani pastoral responsibilities) ... Ila ukanichanganya kwenye kujaribu kuelezea kasisi ...
 
kwa huyu - Popularity yake itakuwa low!! na huu ni mtaji mwingine kwa UKAWA + hasira za wale team lowassa iwapo watakata jina itakuwa ni mtaji mwingine mkubwa!!

CCM ina kibarua kigumu sana, bila uangalifu mkubwa basi tunaweza kuweka matanga!!
 
Mimi naamini sana kuwa Judge Augutine Ramadhani ni mwadiluf paseee lakijni Taifa na hasa Tanzania bara linahitaji Mtanzania Bara mwenye damu ya asilia upande wa bara kupambambana na magugu maji mazito yenye kila aina ya nguvu kuhakikisha Taifa hili linatoka kweye mkwamo ambao limekua likiishi kwa muda mlefu...Taifa linataka Mbara kwa kuwa katiba ya Zenj ina mambo yaliyojili 2010 ambayo kama yakizingatiwa donge la mamlaka ambayo CCM wameyamilki kitambo litaondoka kwa kura za gadhahabu na hatimae baadhi hata ya Wanaccm wapelekee kupiga kura za HASIRA dhidii ya chama chao.Kwa kumsimamisha mtu kama Makongoro ambae ana uwezo na upeo mkubwa na bado anaback up ya baba yake ambae vizazi vyote vya zamani na sasa vinamkubali kama Baba wa Taifa ni turufu nyepesi na isiyo na mawaa..Lakini kwa kuwa Makongoro anasimamia ITIKADI ASILIA basi kunatengenezeka mazingira ambayo UFISADI nao uancheza rafuz ake ili uweze kukwaa kiti hicho.
 
Hakuna binadamu msafi chini ya jua.Tuombe Mungu tupate mtu sahihi wa kutuinulia uchumi wetu.Wapo walioingia wasafi na wakatoka kama tope
 
Watanzania wenzangu tunapita katika kipindi kigumu kupata mtu sahihi anayefaa kuwa rais wetu. Katika kipindi hiki kuna makundi yamepewa pesa kuwachafua baadi ya wagombea.

Makundi haya yanatafuta kila sababu ya kumchafua Jaji Augustino Ramadhani, kwa kuwa hawana hoja, kwani Jaji Ramadhani hachafuki, wanatafuta visababu visivyo na kichwa wala mkia.

Hoja ya kwanza ilikuwa eti majaji na wanajeshi hawaruhusiwi kuwa wanachama wa vyama vya siasa. Mzee wa watu kawajibu mara moja tu hoja hiyo inaonekana nyepesi, majibu yake yalikuwa kama ifuatavyo:-

Alipohitaji kujiunga na jeshi akiwa anasoma UDSM, alijiunga na TANU na kusitisha uanachama mwaka 1992 ili kukidhi mahitaji ya katiba.

Swali: Je, Jaji Ramadhani ni yeye pekee ambaye aliwahi kugombea nafasi ya rais huku akiwa mwanajeshi au jaji? Rais Kikwete ni mwanajeshi mstaafu na aligombea mwaka 2005 na sasa ni rais wetu anayemaliza muda wake. Hata jaji Ramadhani alikuwa mwanajeshi na jaji, sasa ni mstaafu kama Kikwete. Tafuteni hoja nyingine hii imeshindwa.

Wakora wametafuta hoja nyinge, eti Jaji Ramadhani amevunja kiapo cha kanisa la Anglican Tanzania. Kanisa la Tanzania siyo kanisa la Anglo Catholic Church kama baadhi wanavyodai, kanisa la Anglican limesajiliwa Tanzania kama Anglican Church of Tanzania na sio Anglo Catholic Church.

Pia ya MUNGU mpeni MUNGU na ya Kaisari mpeni Kaisari. Pia Biblia inatambua kuwa mamlaka zote zinatoka kwa MUNGU” Warumi 13:1-7 “Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu”. Haiwezekani MUNGU atambue Mamalaka za juu harafu watumishi wa MUNGU wasiruhusiwe kuwa viongozi.

List of Anglo-Catholic churches From Wikipedia, the free encyclopedia
This is a list of Anglo-Catholic parishes and missions within the Anglican Communion that are considered notable.

Set by Contents
1 Australia
2 Brazil
3 Canada
4 New Zealand
5 United Kingdom
6 United States

Katika orodha hiyo hapo juu, hakuna hata nchi moja ambayo ipo chini ya Anglo-Catholic churches ambayo canon law ya 1734 ac number 4559 imekuwa quoted na baadhi ya team za wa wagombea.

Tafuteni sababu nyingine hii imeshindwa.

Wewe mzembe sana umekimbia Exlusive thread kule umekuja kujibanza huku? Kule unaogopa nini? Lete hoja zako kule kwenye thread mama.
Invisible Moderator huyu anajaza server bure iunganisheni hii thread ya kiuwogawoga na ile exclusive tupambane kwa hoja kule.
 
Last edited by a moderator:
Watanzania wenzangu tunapita katika kipindi kigumu kupata mtu sahihi anayefaa kuwa rais wetu. Katika kipindi hiki kuna makundi yamepewa pesa kuwachafua baadi ya wagombea.

Makundi haya yanatafuta kila sababu ya kumchafua Jaji Augustino Ramadhani, kwa kuwa hawana hoja, kwani Jaji Ramadhani hachafuki, wanatafuta visababu visivyo na kichwa wala mkia.

Hoja ya kwanza ilikuwa eti majaji na wanajeshi hawaruhusiwi kuwa wanachama wa vyama vya siasa. Mzee wa watu kawajibu mara moja tu hoja hiyo inaonekana nyepesi, majibu yake yalikuwa kama ifuatavyo:-

Alipohitaji kujiunga na jeshi akiwa anasoma UDSM, alijiunga na TANU na kusitisha uanachama mwaka 1992 ili kukidhi mahitaji ya katiba.

Swali: Je, Jaji Ramadhani ni yeye pekee ambaye aliwahi kugombea nafasi ya rais huku akiwa mwanajeshi au jaji? Rais Kikwete ni mwanajeshi mstaafu na aligombea mwaka 2005 na sasa ni rais wetu anayemaliza muda wake. Hata jaji Ramadhani alikuwa mwanajeshi na jaji, sasa ni mstaafu kama Kikwete. Tafuteni hoja nyingine hii imeshindwa.

Wakora wametafuta hoja nyinge, eti Jaji Ramadhani amevunja kiapo cha kanisa la Anglican Tanzania. Kanisa la Tanzania siyo kanisa la Anglo Catholic Church kama baadhi wanavyodai, kanisa la Anglican limesajiliwa Tanzania kama Anglican Church of Tanzania na sio Anglo Catholic Church.

Pia ya MUNGU mpeni MUNGU na ya Kaisari mpeni Kaisari. Pia Biblia inatambua kuwa mamlaka zote zinatoka kwa MUNGU” Warumi 13:1-7 “Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu; kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo umeamriwa na Mungu”. Haiwezekani MUNGU atambue Mamalaka za juu harafu watumishi wa MUNGU wasiruhusiwe kuwa viongozi.

List of Anglo-Catholic churches From Wikipedia, the free encyclopedia
This is a list of Anglo-Catholic parishes and missions within the Anglican Communion that are considered notable.

Set by Contents
1 Australia
2 Brazil
3 Canada
4 New Zealand
5 United Kingdom
6 United States

Katika orodha hiyo hapo juu, hakuna hata nchi moja ambayo ipo chini ya Anglo-Catholic churches ambayo canon law ya 1734 ac number 4559 imekuwa quoted na baadhi ya team za wa wagombea.

Tafuteni sababu nyingine hii imeshindwa.

Hakuna asemae n mchafu ila hafai kuwa rais,kwanza lazma rais awamu hii atoke mikoa ya bara tumechoka kuwa na waswahili,pili hana ubavu wa kufanya maamuzi.mdebwedo tunasema niooiooooio
 
Swala la uanajeshi halipo,lilopo kwa sasa yeye ni KASISI wa kanisa aka kiongozi wa kanisa na sheria inataka moja either aache UKASISI ili awe mwanasiasa au aache Siasa ili aendelee kuwa KASISI achunge kondoo zake vyema.

Na alikuwa jaji huku akiwa na mapenzi na ccm nina mashaka na kesi alizoziendesha kisheria kakiuka maadili ya uongozi hembu tuwe wakweli ulikuwa jaji leo hii uje ugombee urais:what::banghead:
 
Tukitaka pure clean ni; 1. Makongoro Nyerere 2. Prof Mark Mwandosya 3. Jaji Ramadhani 4. Dr. Asha Rose Migiro 5. Dr Gharib Bilal kwisha wengine wote ni reject.
Wa kwanza katika hao ni Jaji Agustino Ramadhani. Hana makundi ndani ya chama, na ametumikia taifa hadi kustaafu akiwa hana kashifa yoyote. Ni Mzamnzibari safi! Kwamba ni Kasisi hilo si juu yetu kujadili. Ni juu ya Uongozi wa Kanisa la Kianglikana Tanzania. Na kwao Jaji Agustino kugombea ni rukhsa!
 
Mkuu ni kweli lakini mbona jamaa amekueleza hapo juu chini hiyo jamaa waliquote siyo law kanisa la ANGLICAN Tanzania halipo kwenye hiyi CANON LAW? Pia hatuwezi fahamu mpaka kufikia uamzi huu kama kapata baraka za uongozi wa wa juu wa Kanisa. Lakini pia sisi kama Watanzania linatuzuia nini au linatuhusu nini akiwa rais wetu?

Hayo ni mambo ya ndani ya Kanisa, watayatatua wenyewe. Hayo ni mayowe ya wapambanaji tu, lakini hayana madhara. Wapo wachungaji wengi waliopo kwenye siasa, kuna mchungaji Lwakatare, mchungaji Msigwa na wengine. Mbona watu hawakupiga kelele kwa hao?

TUnapoongelea Kanisa kubwa kama Anglican High Church,Anglican Low Church,Catholics,Lutherans,Senventh day,hatuongelei makanisa yanyoanzishwa na watu binafsi leo naanzisha kanisa langu lipo machame tu kwingine halijulikani hili halina impact wala sheria zozote,sheria mimi ni askofu wa kanisa mchungaji nk nk ninajitungia sheria kulingana ninavyotaka lie.

Lakini haya mengine yanasheria zinazotambulika ulimwenguni na si lazima ziwe Canon Law,inawezecana wanasheria zao kabisa na kama amekuwa Ordained as a Priest maana yake dunia nzima kwa kanisa la Anglican High Church analotoka Judge wanajua.

Na pia ipo sheria yetu mama inayokataza kiongozi wa dini kuwa mwanasiasa.Kiongozi wa dini anatakiwa avae kofia moja tu,either mwanasiasa au kiongozi wa dini.Hii nitakupa sababu kubwa moja,Judge Ramadhani Augustino ni mwanaCCM je,unadhani tukiwa kanisani na mimi ni mwanachama wa Upinzania atanitendea HAKI?Je tukifika mahali tukakwaruzana na anajua mimi ni mpinzani HAKI itandeka?Je Kiongozi ambaye si MwanaCCM ambaye yawezekana kicheo ni mdogo kanisani kakosa unadhani atatendewa HAKI?

La pili huoni kwamba kwa kuwa ni RAIS wamuungano ni rahisi zaidi kupendelea Kanisa lake atokako sababu ni Kiongozi wa kanisa,akifanya hayo mtamlaumu?

Ninajua kwa CCM ni sawa lakini hili lingekuwa kwa UPINZANI moto wake sijui kama kungetokea mtu wa kuuzima.Ifike mahali sheria ikate pande zote mbili na siyo iwe upande mmoja ni sawa na upande wa pili ni jinai.Sheria zetu Judge anajua zinasemaje.Amtendee HAKI Mt Augustino wajina wake hilo ndilo ninalomuomba.

Awe mkweli kwa nafsi yake mwenyewe na nafsi zetu watanzania.Aamue moja kuukana uongozi wa Kanisa na kuuchukua Uongozi wa kidunia.Tusikwepe UKWELI kwa upofu wa UADILIFU wa mtu.....

Yawezekana pia alikuwa hayuko fair kwenye kesi zinazokabili CCM sababu alikuwa na interest na CCM aka KADA wa CCM.

Tujitahidi kuita CHEPEO CHEPEO na si KIJIKO KIKUBWA.
 
Binafsi ingizo jipya katika list ya watangaza nia, kwa Jaji Ramadhani kuchukua fomu za kugombea nafasi ya Urais, limenipa faraja na matumaini ya kupata uongozi thabiti na wenye manufaa kwa Watanzania.

Kipindi fulani, niliona na nikaandika kwamba kama Jaji Akiteuliwa, na CCM basi litakua jambo jema kwa Chama na chaguo sahihi kwa Tanzania salama.

Mantiki ya angalizo langu liligusia sifa alizonazo Mh. Jaji ukilinganisha na mahitaji halisi kwa sasa. Mtazamo wangu ni kwamba anafit katika kila hitaji.

Sioni ni mgombea gani aliyepo kwa sasa mwenye vigezo sahihi kama vyake, sio kwamba waliopo hawafai, ila je sifa walizonazo zinakidhi mahitaji ya sasa, ukitazama kwa haraka, na ukitulia pia na kuangalia kwa umakini utagundua kwamba jaji anawapiku na kuwaacha kwa mbali wagombea wake.

Rekodi yake ya utuimishi kwa uma ni safi, na imejipambanua yenyewe, viashiria vya ziada vinampa upendeleo zaidi, ni makosa, na si sahihi, kutumia mihemko katika kufanya maamuzi, huyu ndiye mtu sahihi kwa sasa, tunahitaji atumike.

Ni imani yangu kwamba uzoefu wake katika utumishi wa uma, na weledi wake utatufikisha mahali salama na sahihi kama taifa.

Ni rai yangu kwa wependa maendeleo na amani kwa taifa hili, kujumuika wote na kumpa sappoti Jaji Ramadhani katika nia yake hii ya kuongoza taifa letu.

Amani kwenu.
 
Kwa sasa ni Rais wa mahakama ya Afrika ya haki za binadamu Arusha, Jaji Ramadhani alikuwa na mpango wa kutumikia kanisa kama kasisi baada ya kustaafu lkn akateuliwa kwa nafasi hiyo, mpaka sasa hana hajakabidhiwa kanisa la kuhudumia, ukassisi aliopewa na daraja la ukasisi na siyo kuteuliwa kusimamia kanisa fulani kama ilivyo kwa PENGO AU RWAKATALE. kwa wale wasio fahamu KASISI ni daraja ndani ya kanisa nyingine ni KATEKISTA, SHEMASI ASKOFU NA NK.

Nafasi hiyo sidhani kama ni ya kisiasa na ndiyo maana kuna Mapadre,masister,mashehe ambao ni Ma-leacturer chuo kikuu zaidi sana nafasi ya RAIS WA MAHAKAMA YA AFRIKA YA HAKI ZA BINAADAMU ni kazi na si siasa.

Na sidhani kama ameitendea HAKI nafasi hiyo hasa ukizingatia namna DAFTARI la WAPIGA KURA linavyofanywa na JUDGE mwenzie.Ndiyo maana bado sina IMANI na Judge Ramadhani kama atatusaidia tuendako,kama ameshindwa leo kukemea maovu sidhani akiwa ndani ya CCM ataweza.
 
Na alikuwa jaji huku akiwa na mapenzi na ccm nina mashaka na kesi alizoziendesha kisheria kakiuka maadili ya uongozi hembu tuwe wakweli ulikuwa jaji leo hii uje ugombee urais:what::banghead:

Kwa sisi wanaCCM hatulioni hilo.Ila lingekuwa upinzani cha moto mngekiona.
 
Back
Top Bottom