GE2025 Jaji Asina: Watendaji wa uchaguzi muithamini dhamana mliyopewa

GE2025 Jaji Asina: Watendaji wa uchaguzi muithamini dhamana mliyopewa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,436
Reaction score
5,231
Watendaji wa Uchaguzi ngazi ya Kata wametakiwa kuitambua na kuithamini dhamana waliyopewa ya kusimamia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 kwenye ngazi hiyo.

Wito huo umetolewa na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama Kuu Asina Omari leo Agosti 06, 2025 alipotembelea na kukagua mafunzo kwa watendaji hao katika Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino na Manispaa ya Jiji la Dodoma ambapo amewasisitiza kuwa Tume inatarajia watatekeleza majukumu hayo kwa kuzingatia uadilifu, uaminifu, uzalendo na weledi

"Mtambue na mthamini dhamana mliyopewa, mmepewa dhamana ya kwenda kusimamia uchaguzi ngazi ya Kata kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 hivyo tunatarajia ya kwamba mtatekeleza majukumu yenu kwa uadilifu na kwa uzalendo...kuna aspect pia ya uweledi" Ameeleza Jaji Asina.

Mafunzo hayo ya siku tatu ambayo yalianza mapema Agosti 04, 2025 yamehitimishwa leo Agosti 06, 2025 ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo watendaji hao kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu.

snapins-ai_3693356431428658398.jpg
snapins-ai_3693356430891727061.jpg
snapins-ai_3693356431294507913.jpg
 
Back
Top Bottom