Jaji amuonya Waziri Maua Daftari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji amuonya Waziri Maua Daftari

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, May 7, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  JAJI wa Mahakama Kuu, Fredrica Mugaya amemtahadharisha Naibu Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Dk Maua Daftari kuwa hata kama akifanya mbinu ya ucheleweshaji, hukumu ya kesi dhidi yake na Fatma Salim Said iko palepale na haitabadilika.

  Jaji Mugaya alitoa tahadhari hiyo baada ya Dk. Daftari kuomba hukumu hiyo iahirishwe kusomwa kwa madai kuwa anataka kuwasilisha kiapo, ombi lililowasilishwa na wakili wake, Kalori Tarimo.

  Katika kesi hiyo ya madai, Fatma ambaye ni mke wa zamani wa rais mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), Dk Salmin Amour, anamdai naibu waziri huyo Sh400 milioni. Hata hivyo, baada ya kusikiliza kesi hiyo, Mahakama Kuu iliamuru Dk.

  Daftari amlipe mlalamikaji huyo kiasi cha Sh. 107milioni, pamoja na gharama nyinginezo za kesi kama zitakavyoainishwa.

  Hukumu hiyo, ilitarajiwa kusomwa jana na Jaji Mugaya lakini kutokana na ombi hilo la Dk. Daftari, haikuweza kusomwa ili kutoa nafasi ya kuwasilisha na kusikiliza kiapo chake. Alipohojiwa na Jaji Mugaya kuhusu umuhimu wa maombi hayo, Wakili Tarimo alidai kuwa yeye anatekeleza matakwa ya mteja wake.

  Licha ya kukubaliana na maombi hayo, Jaji Mugaya alimtahadharisha mlalamikiwa huyo kuwa kiapo hicho hakitabadili chochote katika hukumu hiyo ambayo tayari imeshakamilika na kwamba huko ni kutaka kuchelewesha tu kusomwa kwa hukumu hiyo.

  Kutokana na maombi hayo ya kutaka kuwasiliha kiapo, Wakili Tarimo aliomba kesi hiyo iahirishwe hadi mwezi Juni. Hata hivyo, Jaji Mugaya alikataa ombi hilo na kutoa siku saba kwa mlalamikiwa kuwasilisha kiapo hicho mahakamani hapo na kupanga siku ya kusikiliza kiapo hicho kuwa Mei 27.

  “Upande wa mlalamikaji mkipenda mnaweza kujibu lakini haina ulazima,” alisema Jaji Mugaya akimweleza wakili wa mlalamikaji, Dominick Kashumbugu.

  Kwa mara ya kwanza hukumu hiyo ambayo iliandaliwa na Jaji Laurean Kalegeya ilisomwa Novemba 14, 2007 na naibu msajili wa Mahakama Kuu, Mwakibanila na mahakama ikamwamuru mlalamikiwa amlipe kiasi cha Sh107milioni pamoja na gharama za kuendesha kesi kesi hiyo. Hata hivyo, DK.

  Daftari hakuridhika hivyo akakata rufaa kupinga hukumu hiyo, lakini ikatupiliwa mbali na jopo la majaji watatu mwaka 2009. Jopo hilo lililoongozwa na Jaji Harold Nsekela, pamoja na mambo mengine liliiagiza Mahakama Kuu hukumu hiyo isomwe upya na jaji na si msajili ambaye kisheria hana mamlaka ya kusoma hukumu.

  Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo, Fatma alikuwa akimdai Dk Daftari Sh.210,092, 400 alizompa ili amnunulie vifaa mbalimbali kati ya mwaka 1994 na 1997, lakini mlalamikiwa hakufanya hivyo.

  Vitu hivyo ni pamoja mashine ya kusindika matunda kutoka nchini Afrika Kusini, ungo (dish) la satellite, kutoka Uingereza, gari pamoja na vito vya dhahabu.

  Mbali na pesa hizo taslimu, pia mlalamikaji alikuwa akimdai Dk.
  Daftari pesa za vitu mbalimbali alivyovichukua kwake kama vito vya dhahabu, mabati ya kujengea nyumba na milango ambavyo pia hakurudisha.

  Mlalamikaji pia alikuwa akimdai mlalamikiwa pesa kiasi cha Sh200 milioni kama fidia kwa kuvunja makubaliano hayo, ambazo kwa jumla zilikuwa takribani Sh410milioni, ikiwa ni pamoja na gharama uendeshaji wa kesi hiyo.

  Katika hukumu yake Jaji Kalegeya alieleza kuwa licha ya mlalamikiwa pamoja na mumewe kukataa madai hayo katika utetezi, walionekana kuwa ni matapeli.

  http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-habari-za-kitaifa/1411-jaji-amuonya-waziri-maua-daftari
   
 2. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,758
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  Too strange! Does Maua want to re-open the case? Pls make a follow up na utujuze the kind of application will Maua file.
   
 3. E

  Estmeed Reader Senior Member

  #3
  May 8, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Huu ni mfano wa ufisadi mwingine wa kila siku unaofanywa na vigogo wenye "diplomatic immunity". Maua Daftari kamfuata rafiki yake ili yeye (Maua) amnunulie vifaa kutoka Afrika Kusini.

  ü Vifaa hivyo vingenunuliwa bila kulipa kodi huko Afrika Kusini.
  ü Vifaa hivyo vingesafirishwa bila malipo ya kodi za kuvisafisha kutoka Afrika Kusini had Tanzania.
  ü Vifaa hivyo vingeingia Tanzania bila kutozwa kodi ya malipo.

  Afrika Kusini na tanzania zinapoteza baadhi ya kodi zinazostahili kulipwa kwa manufaa ya wananchi! Na hii haiwaumi watu kama Waziri Maua Daftari, anayeonekana kwenye picha ya habari akichekelea!

  Hii kesi hii ya ufisadi, kutokana na "conflicts of interests" imechukua muda mrefu! Na Rais kaifumbia macho tu bila ya kumwachisha kazi huyo Waziri wake, kama ilivyo kwa Chenge! Zaidi, rais kaifumbia macho bila hata ya kumtimua Waziri wake!

  Wengine huongwa na wakala, kama ilivyokuwa kesi ua BAE na rada. Mawakala hao hudai % zao. Na kama mwuzaji akisema kuwa % ni juu sana, basi mawakala wanamwambia aongeze bei ya manunuzi. Mnunuzi atakubali kufanya hivyo; na huwagawia mawakala hamsini zao. Mwishoni, anayewalipa mawakala hao huwa ni Tanzania.
   
 4. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  duh, kumbe tunao mawazili matapeli...au nakosea, na hivi huyo fatma alikuwa anataka kupitia mgongo wa waziri kununua vitu ili asilipe baadhi ya kodi nini? kwani maua ni mfanyabiashara wa magari, ungo na mashine? dili ziliungua wakaamua watoboe siri maji yakiwa shingoni. hii ndo tz bwana...
   
Loading...