Mmoja wa mawakili wao, John Mapinduzi, waliiambia mahakama kuwa wateja wae, hawana imani na jaji hasa baada ya kesi yao kuchukua muda mrefu.Pia walidai kuwa hakuna ushahidi kuwa wakipewa dhamana watatoroka kama ilivyoelezwa na jaji.
Awali Jaji Sheikh, alisema madai ya washtakiwa kumtaka ajitoe yalikuwa hayana msingi wowote na kwamba yalikuwa ya nia mbaya dhidi yake kufuatia uamuzi wa kuwanyima dhamana.Jaji Sheikh alisema sababu za kumtaka ajitoe walizozitoa hazikidhi viwango vya kisheria vilivyowekwa na Mahakama Rufani.