Jaji ajitoa kesi ya samaki 'wa Magufuli'

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Jaji ajitoa kesi ya samaki 'wa Magufuli' Send to a friend Thursday, 03 March 2011 20:43

James Magai na Tausi Ally

JAJI Razia Sheikh aliyekuwa akisikiliza kesi kuhusu uvuvi haramu katika Bahari Kuu ya Tanzania, amejitoa katika kesi hiyo, ili ipangiwe jaji mwingine.Jaji Sheikh alitangaza hatua hiyo jana wakati akitoa uamuzi juu ya maombi ya washtakiwa waliomtaka ajitoe katika kusikiliza kesi hiyo, kwa madai kuwa hawana imani naye.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni 36 na ni raia wa mataifa ya China, Ufilipino, Vietnam na Kenya.Kwa pamoja, watu hao wanakabiliwa na mashtaka ya kuvua samaki katika Ukanda wa Kichumi wa Tanzania bila kibali cha kuwaruhusu kufanua hivyo.Pia wanakabiliwa na shataka la kuchafua mazingira ya bahari katika eneo hilo.

Februari 25 mwaka huu, washtakiwa hao walimtaka jaji Sheikh ajitoe baada jaji huyo, kuwanyima dhamana kwa madai kuwa mazingira ya kesi hiyo hayaruhusu.Uamuzi huo uliwafanya baadhi ya washtakiwa. kumwaga machozi baada ya wakalimani wao kuwatafisiriwa kuhusu uamuzi wa jaji juu ya maombi yao ya dhamana.

Baada ya tafsiri hiyo, washtakiwa kupitia kwa mawakili wao,walimtaka jaji ajitoe katika kesi yao.

Mmoja wa mawakili wao, John Mapinduzi, waliiambia mahakama kuwa wateja wae, hawana imani na jaji hasa baada ya kesi yao kuchukua muda mrefu.Pia walidai kuwa hakuna ushahidi kuwa wakipewa dhamana watatoroka kama ilivyoelezwa na jaji.

Awali Jaji Sheikh, alisema madai ya washtakiwa kumtaka ajitoe yalikuwa hayana msingi wowote na kwamba yalikuwa ya nia mbaya dhidi yake kufuatia uamuzi wa kuwanyima dhamana.Jaji Sheikh alisema sababu za kumtaka ajitoe walizozitoa hazikidhi viwango vya kisheria vilivyowekwa na Mahakama Rufani.
 
PHP:

DPP alifute hili shauri na hawa jamaa waruhusiwe kwenda makwao......................very difficult to prove the ellgations levelled against them................hivi tunayo tekinolojia ya kupima walikuwa ndani ya mipaka yetu au nje wakati walipokuwa wanavua???????????

Jibu ni hatuna hiyo tekinolojia...then why waste more resources over a FAILED CASE..............................
 
Back
Top Bottom