Kampuni ya PR inayodaiwa kutumiwa kupitisha fedha "za" Jairo itajwe...

Game Theory

Platinum Member
Sep 5, 2006
8,545
835
Barua ya Jairo hii hapa:

Contribution towards finalisation of preparations and tabling of the ministry's 2011/12 budget in Parliament in Dodoma.

The ministry has successfully prepared the 2011/12 budget estimates, which have already been approved by Parliament's Energy and Minerals Committee. In finalising the process, the budget speech is expected to be tabled on July 15 and 18. As has been the case during the presentation of the budget speech in Dodoma, officials from the ministry and institutions under it accompany senior leaders to assist them in making clarifications during debate.

In order to facilitate the smooth tabling of the budget you are requested to contribute a total of Sh50,000,000. The money should be deposited in the Geological Survey of Tanzania (GST) account No. 5051000068 NMB, Dodoma Branch. After the cash is deposited, the ministry should be informed through the DP (director of personnel) for coordination.

Thank you for your cooperation.

jairo.jpg


Latest ni kuwa pesa zimeondolewa tayari from the bank .....stay tuned for the name of the PR company iliyopewa tenda ya kuzikusanya hizo 1 billion.
 
Kumbe Geological Survey ndio akaunti chaka ya kufanyia ufisadi,jambo hili linaumiza,yaani wanapora walipa kodi na walipa bili za umeme na kuwapelekea waheshimiwa wasishiba posho.

Tena ikiwa ni itaratibu wa kila mwaka, hawa Geo Survey watuambie pesa hizo zipo wapi na kama walizitoa ni kwa matumizi gani na PCCB wanasubiri CDM wapelekewe ushahidi na CDM?
 
Geological Survey of Tanzania, nao wanapaswa kuwajibishwa, kwanini wakubali akaunti yao itumike kwa ajili ya deals zisizo na kichwa wala miguu. Inawezekana ndio maana wiki moja kabla ya bajeti ya wizara, na siku bajeti iliposomwa na ilipojadiliwa, GST palikua pako busy mpaka usiku!! Inawezekana walikua wanashughulikia masuala mbalimbali ikiwa pamoja na kutoa hizo pesa za uwezeshaji ​ili bajeti ipitishwe bila kupingwa!
 
Hivi ni PR company gani iliyokuwa inakusanya hizi 1billion za Jairo? Imekuwa procured kwa taratibu zipi na wao wanachukua kamisheni ya kiasi gani?
 
Pinda: Hatima ya Jairo iko kwa Rais

Thursday, 21 July 2011

AWEKA WAZI MAAGIZO MAPYA, KAAMBIWA ATULIE HADI MWENYEWE ATOKE AFRIKA KUSINI

Leon Bahati, Dodoma

WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda ameyaweka hadharani maagizo aliyopewa na Rais Jakaya Kikwete kuhusu tuhuma za rushwa zinazomkabili Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo akisema amemwambia kwamba atashughulikia suala hilo yeye mwenyewe atakapotoka ziarani Afrika Kusini.

Juzi, Waziri Mkuu ambaye ni kiongozi wa shughuli za kila siku za Serikali bungeni, aliliambia gazeti hili kwamba alipewa maagizo na Rais juu ya kushughulikia tuhuma za kutenga zaidi ya Sh moja bilioni, kwa ajili ya kufanikisha kupitishwa kwa bajeti ya wizara yake.

Hata hivyo, jana alipoulizwa nje ya ukumbi wa Bunge kuhusu maelekezo hayo ya Rais, Pinda, alijibu: "Mheshimiwa Rais amesema atakuja kulishughulikia akirudi."

Pinda ambaye siku ya tukio hilo alionekana kuhamaki bungeni na kusema kwamba kama angekuwa na mamlaka angemfukuza kazi Jairo, jana alionekana mwenye subira huku akisisitiza kuwa: "suala hilo halina uharaka."

Tuhuma dhidi ya Jairo ziliibuliwa na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo ambaye alisema mtendaji huyo mkuu wa wizara alitoa dokezo kwa taasisi zote zilizo chini ya wizara hiyo kutoa Sh50 milioni ili kufanikisha bajeti kupita bungeni hatua ambayo iliibua hasira miongoni mwa wabunge hasa ikizingatiwa hali ya nishati ya umeme ilivyo kwa sasa nchini.

Shellukindo katika tuhuma zake alisema, Jairo aliziandikia barua idara na taasisi hizo akiziagiza ziweke fedha hizo kwenye akaunti namba 5051000068 inayomilikiwa na Geological Survey of Tanzania (GST) kwenye Benki ya NMB, Tawi la Dodoma.

Kabla ya ufafanuzi huo wa Pinda, jana mchana kulikuwa na tetesi zilizozagaa katika jiji la Dar es Salaam na baadhi ya mitandao ya intaneti zikidai kwamba Jairo ameandika barua ya kuomba kujiuzulu. Akizungumzia tetesi hizo Pinda alisema: "Sina taarifa hizo," na kuongeza Pinda na kukiri kwamba hata yeye amezipata lakini haelewi chochote kuhusiana na hilo.

Jumatatu wiki hii, baada ya Shellukindo kuibua tuhuma hizo bungeni, Pinda aliahidi kuwa angewasiliana na Rais siku hiyo baada ya kutua kutoka kwenye ndege kwa ajili ya kumchukulia hatua za kinidhamu... "Kwa jinsi jambo hili lilivyokaa, hakuna jinsi mtu unavyoweza kulitetea hata kidogo, nilitamani sana kwamba nije hapa niseme kwamba uamuzi wangu mimi ni huu, lakini haikuwezekana.

Kwa dhati kabisa naomba wabunge tuwe na subira, mara tu mheshimiwa Rais atakapotua South Africa (Afrika Kusini) jioni ya leo (juzi), nitamwarifu na ninaamini tutaelewana kuhusu hatua za kuchukua.

Hata hivyo, Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, imesema haijui chochote kuhusu mawasiliano hayo ya Rais Kikwete na Waziri Mkuu Pinda, kuhusu hatua za kushughulikia jambo hilo. Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais, Premi Kibanga alisema hadi jana mchana, kurugenzi hiyo haikuwa na taarifa yoyote juu ya tuhuma zinazomhusu Jairo wala mawasiliano baina ya Waziri Mkuu na Rais."Kama (Waziri Mkuu Pinda kumpigia Rais Kikwete), atakuwa amempigia siyo lazima sisi tujue," alifafanua Kibanga.
 
Well...evidence of threads asking name of this company seem to disappear bila sababu.

Makes you wonder kama JF sio part of the Jairo conspiracy. I mean seriously why would JF (owners/mods) have special interest kwenye kuondoa haya maswali?

Maswali yenyewe ni:

Jina hii kampuni

Name of directors

Walipewa tenda hii na wizara ya nishati lini

Kazi hii ilitangazwa lini

Ina worth how much

Je how much did they get kwa kusanya hizi pesa

Je wao wanajitetea vipi?
Kama tunakosea kuulizia jina la hii PR company basi tunaomba tuambiwe , we might be asking the wrong questions

well...
 
Well...evidence of threads asking name of this company seem to disappear bila sababu.

Makes you wonder kama JF sio part of the Jairo conspiracy. I mean seriously why would JF (owners/mods) have special interest kwenye kuondoa haya maswali?

Maswali yenyewe ni:

Jina hii kampuni

Name of directors

Walipewa tenda hii na wizara ya nishati lini

Kazi hii ilitangazwa lini

Ina worth how much

Je how much did they get kwa kusanya hizi pesa

Je wao wanajitetea vipi?
Kama tunakosea kuulizia jina la hii PR company basi tunaomba tuambiwe , we might be asking the wrong questions

well...
??????...............................
 
Mkuu unazungumzia nini hii GST au? Anyways nilikua naangalia kwa ukaribu kuhusu hii GST na inafanya vitu gani. Nimeshtuka nilipoona imeanzishwa mwaka 2005 wakati wenzetu wanaingia Ikulu. I believe CEO wake bado ni Dr. Mruma ambaye yuko Geology Univ. of DSM. Lakini kinachotia shaka zaidi ni web site yao ambayo ina very few info na kwingine kunasema "under construction" Mmh! I am smelling something bad about this GST. Mwenye info zaidi tusaidiane.
 
Jamani kama hiyo kampuni ya PR inajulikana si itajwe tu! Lakini mimi nina hofu moja kuwa haiwezekani kampuni ipewe tenda ya kutoa rushwa. Kama hii itakuwa kweli basi ufisadi utakuwa umefikia kiwango kingine; kama signature yangu inavyosema; wakati wengine wanatumia ulazima kubuni vitu vya kusaidia maisha yao, sisi tunatumia ulazima kuvumbua namna na mbinu za kulifisadi taifa letu sana.

So, hiyo kampuni ni kampuni gani...?
 
Hizi kampuni zinazoanzishwa vipindi vya uchaguzi mara nyingi huwa zina walakini, kinachotakiwa baada ya 'kampuni ya kugawa rushwa' GST kujulikana watuambie hizo pesa ziko wapi hadi sasa, nasikia kuna baadhi zilikwisha chukuliwa tunataka tujue ni nani ali zi draw kutoka kwenye ile akaunti na kuzigawa kwa akina nani kama ni wabunge watajwe.
 
Of course JF is part of the conspiracy. Nakushangaeni it took you so long kugundua hilo

The game is gigged & as we speak its a dog eat dog situation
 
PR ni kampuni nyingine tofauti na GST ilipokopea huo mlungula? tujuzeni kidogo.
 
haya makampuni itabidi brela wajieleze vizuri wamefuatilia vizuri hii kitu inaitwa KYC(know your customer) au ndo mlungula mbele..
 
brela unatoa laki mbili wanakupatia certificate hawasomi doc wanakugongea muhuri unachapa lapa hawana muda wa kumchunguza/kumjua mteja.
 
Tusubiri hizo siku kumi tuone sharia inapochukua mkondo wake. Kwani huo ndio utawala wa sheria.

Hongera tanzania kwa kuwa muumini wa kweli wa Rules of law.
 
Tunamtaka aliyemtuma Jairo kufanya huu upuuzi.....
Je rushwa za aina hii ziko wizara moja tu?
 
Jamani kama hiyo kampuni ya PR inajulikana si itajwe tu! Lakini mimi nina hofu moja kuwa haiwezekani kampuni ipewe tenda ya kutoa rushwa. Kama hii itakuwa kweli basi ufisadi utakuwa umefikia kiwango kingine; kama signature yangu inavyosema; wakati wengine wanatumia ulazima kubuni vitu vya kusaidia maisha yao, sisi tunatumia ulazima kuvumbua namna na mbinu za kulifisadi taifa letu sana. So, hiyo kampuni ni kampuni gani...?
Mzee Mwanakijiji, members wote Wa jf ambao ni journalist wanaijua ila nao hawaisemi kwa vile nao ni Beneficiaries na hako kamgao vile vibahasha vyao "little Brown envelopes" vilituna sana!. Kampuni ya PR ya Nishati na Madini ni ...
 
Sorry, nasita kuitaja kwa vile hizi ni ti tuhuma sio Busara kutaja majina ya ya kampuni za watu bila uthibitisho huku Kutakuwa ni kuchafuana.
 
Back
Top Bottom