Nimewataja TAKUKURU kwa kuwa jana wametamba kwamba wameanza uchunguzi na halafu ndiyo chombo pekee kilichopitishwa na bunge kufanya kazi kama hizi. Au washauri tumuombe DCI Manumba ashupalie hili suala, lakini looh nanongonezwa na kuwa kumbe Hosea wa TAKUKURU na Manumba wanatoka wilaya moja, sijui hiyo itaathiri utendaji wao!!! Kuhusu swali lako, miimi ni Mtanzania, naishi muda nusu kwa nusu Bongo na nje ya nchi katika kuhangaikia maisha. Kumbuka maneno ya Mwalimu Nyerere alipokuwa anaongea kuhusu uchaguaji wa candidate mzuri wa uraisi: 'Mimi siyo kuku sitagi mayai, lakini ukinipa yai bovu nitaligundua!!', hivyo nchi yangu naifahamu, ondoa shaka.
Hivi kwani mtu akijiuzulu hawezi fikishwa katika vyombo vya sheria kama step ya kwanza huku uchunguzi ukiwa unaendelea???
Mkuu, unaamini kabisa Ngereja na naibu wake walikuwa hawajui habari hii....hahahahaAmesema ni kwa nini anajiuzulu? Yawezekana ni bangusilo na 'wakuu' wanataka kufunika kombe! Hii habari ya kulobby (kuhonga!) ili bajeti zipite imeanza kusikika muda mrefu tu.
Atakuwa ameonyesha njia ila isiishie hapa lazima mtandao mzima uwe tracked ikiwemo list ya wabunge waliokula hizo hela. Ni rahisi kuwapata kwani benki wana jina la mtu aliye draw hizo hela na tarehe aliyochukua. Pia wizara nyingine zifuatiliwe maana najua huo ndio utamaduni wa serikali inayopinga rushwa lakini yenyewe inatoa rushwa kwa wabunge.
Hapa ndo napata picha kwamba siyo rahisi TAKUKURU ifanikiwe kufanya kazi kama autonomous institution kwani nao pia kama idara kuna jinsi nao walitakiwa watoe mchango wa rushwa kwa wabunge ili bajeti YA WIZARA yao ipite na kwa kufanya hivyo wataweza kupambana na rushwa vizuri zaidi. "WHAT A JOKE"
maadam chenge ni safi machoni mwa takukuru, jueni ya kuwa imeshafeli kabla haijaanza takukuru-puka, mimi binafsi sina imani na serikali hii ya ccm-jk.Kama TAKUKURU wako serious, waongeze wigo wa uchunguzi, wapitie akaunti zote za Idara za serikali zilizoko hapo Dodoma yaani hiyo Geological Survey (Madini), Msalato na Bihawana Secondary (Elimu), Isanga Prisons (Mambo ya Ndani), Mirembe Nursing School (Afya), Makutupora JKT (Ulinzi) nk; hizi zote inawezekana ziunatumiwa kupitisha mafungu ili zitumike kuhonga wabunge. Na hasa wachunguze zile transfer kubwa kubwa za funds katika kipindi cha March hadi August. Naamini kwa kuwa wao ni wataalamu, basi watajua technic nzuri zaidi ya mapendekezo yangu. Lakini nikikumbuka uchakachuaji wa uchunguzi wa awali wa Richmond, basi na-reserve my comments kama hawa TAKUKURU wanaweza chukua maamuzi magumu!!!
Hivi TAKUKURU iko chini ya Wizara ipi, Wizara ya Sheria na Katiba au Ofisi ya Rais? Kama iko Ofisi ya Rais nachelea kushauri kwamba na wao wachunguzwe akaunti yao hapo Ofisi za TAKUKURU Dodoma kama inapitisha fedha za kulaininsha wabunge ili bajeti ya Ofisi ya Rais ipite. Halafu kila mara huwa tunasikia kuwa kila bajeti ikipitishwa, Wizara husika hjuangusha bonge la party (millions of sdhillings) kusherehekea bajeti yao kupitishwa. Kuna mwaka Wizara ya Mali Asili ilitayarisha party kubwa pale Dodoma baada ya bajeti yao kupita, na wanyama pori kibao walichinjwa na kuliwa. Hii ni dalili ya kitu gani?
Nimeipenda...Kumbuka maneno ya Mwalimu Nyerere alipokuwa anaongea kuhusu uchaguaji wa candidate mzuri wa uraisi: 'Mimi siyo kuku sitagi mayai, lakini ukinipa yai bovu nitaligundua!!', .