Nilikuwa naamini ccm ilitakiwa kujiamini kwa kuwa ni chama dola ila nimegundua kiukweli kabisa ccm imefikia mahali inaogopa hadi kivuli chake! Iweje mtu kama jackline Wolper kurudi ccm iwe habari inayovumishwa kuliko Magufuli kuteuliwa kuwa mwenyekiti? CCM chama changu naona kimepoteza mwelekeo, mpendazoe anarudi inakuwa habari, tena wanaipa uzito, sasa chama dola badala ya kuhangaika na kutekeleza sera zake kimebaki na mipasho na kuhangaika na habari za kurudi kwa watu ambao hata kadi za chama haijulikani kama wanazo.