Jacqueline si mtoto wa Prof Ndalichako, asihukumiwe bila hatia

Kama una ujasiri wa kuandika haya uliyoandika, ungeanza kwanza kumshangaa Rais Dk John Pombe Magufuli ambaye alizunguka nchi nzima akiahidi kwamba "serikali ya Magufuli hakuna mwanafunzi atakayekosa mkopo elimu ya chuo kikuu"!
Mkuu, kama ulimwamini Magufuli aliposema "...hakuna mwanafunzi atakayekosa mkopo..." kwa nini usimwamini G. Malisa pia kwa alichokiandika..?
 
Baada ya kusambaa kwa taarifa inayoonesha wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/17 kumejitokeza mjadala mkubwa juu ya jina la binti aliyejulikana kama Jacqueline Ndalichako, akidaiwa kuwa mtoto wa Waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako.

Mimi ni miongoni mwa watu waliohamaki baada ya kupata taarifa hiyo, na nikasema IKIWA NI KWELI JACQUELINE NI MTOTO WA PROF.NDALICHAKO basi inabidi Waziri huyo ajiuzulu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mtoto wa waziri hawezi kupata mkopo hata kama anakidhi vigezo vya kitaaluma. Mwongozo wa HESLB unamtaka mwanafunzi awe anatoka familia isiyojiweza kiuchumi, lakini mtoto wa Waziri hawezi kuwa kundi la wasiojiweza kiuchumi. Wapo watanzania wengi wenye uhitaji wa mikopo ya elimu ya juu kuliko watoto wa mawaziri.

#UKWELI_KUHUSU_TAARIFA_HIYO.

Baada ya kufuatilia nimegundua mambo yafuatayo:

1. Jacqueline si mtoto, ndugu wala hana unasaba wowote na Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi. Ni ufanano tu wa majina, baina ya watu hawa wawili lakini ni watu wasiofahamiana kabisa.

2. Profesa Ndalichako hana mtoto mwenye jina Jacqueline, wala hana ndugu mwenye mtoto mwenye jina hilo.

3. Watoto wa Profesa Ndalichako walishahitimu elimu ya juu na hakuna yeyote anayejiunga na elimu ya juu kwa sasa.

4. Jacqueline amehusishwa na Prof.Ndalichako kwa sababu ya ufanano wa majina, lakini si watu wenye kufanana nasaba.

5. Jacqueline hakusoma HGL kama ilivyoelezwa. Amesoma EGM na amechaguliwa kusoma Shahada ya Uchumi na Takwimu (B.A in Economics and Statistics).

6. Jacqueline anatoka familia yenye uchumi wa kawaida hivyo anakidhi vigezo vya kupewa mkopo. Amesoma St.Mary Gorreti katika mazingira ambayo si vzr kuyaeleza hapa. (Nimefuatilia taarifa za familia ya Jacqueline inayoishi Yombo Dovya lakini nisingependa kuziweka hapa).

SWALI: Je waliosema Ndalichako awajibike wamekosea?

JIBU: Hapana. Hoja ilikuwa "Kama kweli Jacqueline ni mtoto wake basi awajibike". Hii ina maana kuwa hakukuwa na sababu ya kuwajibika kama si mwanae.

SWALI: Walioibua hoja ya Jacqueline kuwa mtoto wa Ndalichako wamekosea?

JIBU: Ndio. Walioanzisha hoja hii wamekosea kwa kuwa kuna viashiria kwamba walikusudia kupotosha. Hoja hii imepata nguvu mitandaoni na kusababisha usumbufu ambao ungeweza kuepukika.

[HASHTAG]#MyTAKE[/HASHTAG]:
Kwanza niwape pole Jacqueline pamoja na Prof.Ndalichako kwa usumbufu ambao kila mmoja ameupata.

Pili niwatake wote wanaoendelea kusambaza taarifa kuwa Jacqueline na Prof.Ndalichako ni ndugu waache kufanya hivyo maana wanaweza kupotosha wengine.

Ufanano wa majina si kigezo cha kuhukumu wasio na hatia pasipo uchunguzi. Bahati mbaya Jacqueline ameingia kwenye mijadala ya mitandao bila hatia. Amekuwa victim wa social media kwa sababu za kisiasa, ambazo yeye hahusiki nazo kabisa. Pia nimpe pole Prof.Ndalichako kwa usumbufu alioupata.

Ukweli ni kwamba kufanana majina ni jambo la kawaida katika tasnia yoyote. Wapo wanafunzi wengi waliopo vyuoni au waliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu wenye majina yanayofanana na viongozi wakubwa kisiasa lakini hawajahusishwa na viongozi hao.

Kuna mwanafunzi amechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu Dodoma mwenye jina Gideon Wassira, lakini sijasikia akihusishwa na Mzee Stephen Wassira. Kijana Nobert Mbowe amehitimu Chuo kikuu Mlimani akisomea shahada ya Uhandisi wa madini (Mining Engineering) lakini hajawahi kuhusishwa na Mhe.Freeman Mbowe. Kuna mwanafunzi anaitwa Kennedy Yusuf Ndugai amechaguliwa shahada ya elimu maalum UDOM lakini hajahusishwa unasaba wake na Spika Job Ndugai.

Kwa hiyo nitoe wito watu waache kutumia habari inayomhusu Jacqueline kwa kumhusisha na Waziri Ndalichako maana ni watu wasio na uhusiano wowote kinasaba.

Najua wengi wamehamaki kusikia Jacqueline ni mtoto wa Waziri halafu kapewa mkopo huku watoto wa maskini wakikosa mikopo. Kumbe Jacqueline naye ni mtoto wa maskini pia, ila ameponzwa na ufanano wa majina na Waziri Ndalichako.

Nihitimishe mjadala huu kwa kutoa rai kwa "bloggers &social media emperors" kutokuendelea kujadili suala la Jacqueline na Waziri Ndalichako maana ni watu wasiofahamiana kabisa, achilia mbali kuhusiana kinasaba. Tumpe nafasi Jacqueline aweze kucocentrate ktk masomo yake, asiwe frustruted na mitandao. Let us end this discussion to save this innocent poor soul.!

Malisa GJ

Malisa G J,hata waliohusisha jina la huyo binti na Waziri wa ELimu bado hawajakosea,hii inatakiwa iwaonyeshe watawala ni namna gani Watanzania wakawaida wanaumizwa na matendo ya wale tuliodhani tumewachagua kwa ajili ya Taifa.Inaonyesha ni kiasi gani Chuki imejengeka miongozi mwetu,kati ya walionacho na wasionacho!Watawala na watawaliwa.Kesho hao akina Ndugai na Wassira kuna watu watauliza na watatafiti kama wanaunasaba na watawala.

Tumeona watoto wa watawala wakipewa mikopo bila shida na kusomeshwa nje kwa full sponsorship za wafadhili,wapo wakutosha.

Ni wakati wa kujifunza kupitia Binti Jacquiline Ndalichako,ni kwa kiasi gani Chuki na ubaguzi tuliodhani hautamea sasa umemea kwa kiasi kikubwa.

Watawala mjifunze,polisi hali kadhlika mlikotupeleka sasa tumefika
 
TCRA Mungu anawaona. Huyu msambazaji wa taarifa za uwongo na uchochezi m'memwacha?
 
Naona kama kaandika hisia zaidi kuliko utafiti. Anawajuaje ndugu woooote wa prof?
Mkuu, ni kweli kwamba kuna matatizo makubwa kwenye mfumo wa uendeshaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kuanzia kwenye utaratibu wa utoaji mikopo hadi kwenye ukusanyaji wa hiyo mikopo. Lakini mimi siamini kama hayo matatizo yanaweza kuisha kwa kujadili watu waliopata mikopo kwa upendeleo au waliotoa mikopo kwa upendeleo. Nadhani tunaweza kufanya zaidi ya hapo na si kwa HESLB tu maana ubabaishaji imekuwa culture yetu. Kuna taasisi gani ya umma unayoweza kusifia utendaji wake..? Kwa nini tufanyie kazi matukio tu..? Hao watu walioweka vigezo si wanasiasa na wanaovitumia kuchuja waombaji ni baadhi yetu tulioajiriwa pale, na hivyo, tukubali ubabaishaji ni janga la kitaifa wala hakuna wa kumkasirikia. Tujitafakari kwa ujumla wetu labda tunaweza kujisahihisha.

Eng. WFM
 
Sishangai, maana yalisemwa mengi hata alipoteuliwa balozi john kijazi kuwa Katibu kiongozi wakimuhusisha na akina kijazi ambao wana nyadhifa mbalimbali serikalini kuwa ni ndugu yao.
 
Ni sawa na jina la Msuya, wenye sir name ya Msuya wote ni watoto kibaolojia wa Cleopa Msuya ?
 
Walau leo malisa umekuwa binadamu wambie na ukawa wenzako kabla ya kupost chochote wafanye tafiti kidogo.
Maana wengi huwa wanajitoa ufahamu.
 
Katika sakata hili nimegundua kuwa sisi Watanzania tunachuki kali sana kwa watu wanaofanikiwa katika jambo fulani....

Mihemko ya roho ya kwanini na chuki kali vinamfanya mtu apoteze uwezo wake wa kutafakari jambo sawa sawa.....

Sisi Watanzania tunapenda sote tuwe level moja ya maisha....nyoyo zetu zinakuwa ngumu sana kukubali mafanikio ya wenzetu hasa watu wetu wa karibu......na panapotokea tu uchochoro wa kumsilibia hata kama iwe ni kwa uzushi....hapo ndipo utakapoona wanavyohamaki kuonesha kuwa walikuwa wanalingojea jambo hilo kwa muda mrefu.........

Hatuna utaratibu wa kutiana moyo kupiga hatua bali kukatishana tamaa ili mwenzio asifike ulipofika yeye.....anapenda yeye awe kileleni ili awe anawadithia anayoyaona ya juu...lakini sio kukuleta juu ili na wewe ujionee.....
Ni aina ya watu ambao kujiweka nao karibu kunaweza kupelekea anguko lako baada ya kukuinua......

Ndio nimepata kuelewa kuwa kwanini hata huko nje ya mipaka sisi tunakwepana......kwa maana tunafahamiana hila zetu......

Mwisho....naomba Mungu mkuu aziondoe jinamizi hilo kwenye nyoyo za Watanzania.......

Tusiwe wepesi wa kuhukumu kabla hata ya kujua upande wa pili......

Tufikirie kauli zetu kabla ya kuzitoa kwani kauli zetu zinaawaumiza wengine kihisia kuliko hata mijeledi ya moto.....

NB;
Kuna watoto wengine wanasomeshwa na familia zinazojiweza kwa misaada tu...lakini sio ndugu wa damu wa familia husika.....
Utawalaumu watu bure ........ kale kamentality ka Ujamaa bado kapo damuni ndiyo maana watu hawaamini kama mwingine anaweza kupata zaidi ya mwenzake!!

Hako hako kaujamaa mentality ndiko kanawafanya pia viongozi wetu nao watake advantage kwa vitu vingi .... Naamini kabisa watoto wengi tu wa vigogo, matajiri na mawaziri watoto wao wamesomeshwa kwa mikopo kama Watanzania wengine. Inawezekana kabisa ni halali yao but I think it's not right. Ile mentality ya elimu bure iliyotolewa na utawala wa Mwalimu bado inatuandama. Kama mzazi jukumu lako ni kumsomesha mtoto wako as long as you can afford it ... lakini tofauti na nchi nyingine Tanzania wazazi wanafikiri jukumu lao la kusomesha linaishia sekondari tu unless anataka kumsomesha mtoto wake nje ya nchi!!

Kwa wenzetu mtu anajitahidi kuchukua mkopo as little as he/she can wakat hapa kwetu ni kinyume ... mtu anataka kupata mkopo as mach as he/she can!!
 
Mkuu wangu kubishana na upinzani ni kazi kubwa
Una maana gani mkuu kusema hivi?

Kwa nini ishu ya watu kutofautiana kiwazo unakuhusianisha na kuwa mpinzani (naamini una maana ya wafuasi wa vyama vya upinzani)?

Hapana bwana, ondoa hiyo dhana haifai. Ukijifunga ktk dhana hiyo utakosa fursa nyingi sana za kuelewa mambo kadha wa kadha ktk jamii.

Ni vyema penye kukubaliana, tukubaliane tu bila kujali itikadi zetu za kisiasa, vivyo hivyo penye kutofautiana, kukosoana na kushauriana.

By the way mimi wala siyo mfuasi wala mpenzi wala mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi - chama kinachoongoza serikali kwa sasa, lakini siku zote nasimama kwenye ukweli bila kumuonea mtu!!
 
Shida yote hii ni mikopo mikopo hivi mtu unazaa wa nini kama huwezi kumsomeshaa?

Watu wanaleta viumbe kwa starehe zao afu wanaishia kuvipatia shida tu, Serikali duniani zina kazi kwa kweli, haingii akilini mtu aanze la kwanza, form one hadi six mzazi hujajipanga na kujiandaa kumuwezesha mwanao kusoma.

Mungu wape maisha marefu wazazi wangu japo si katika hali ya kujikweza au elimu za ghari sana ila kwenye suala la Elimu walijipanga mapema.

Binafsi sioni hasara kuishi duniani bila ya mtoto ambaye ni wangu ili hali sijaandaa mazingira yatakayomharahishia maisha yake, Japo hatuwezi kuzuia mambo mengine yanayoweza kutokea kinyume na matarajio yetu,ni muhimu dhamira,jitihada na bidii za makusudi ziwepo ili kiumbe chako kisije kuwa tegemezi either kwa serikali au kwa mtu.

Nawaonea huruma sana wanafunzi waliofaulu na wanaoshindwa kumudu gharama za masomo hii haikuwa mipango wala si mapenzi yao ni failure ya wazazi wao, Serikali imekuwa kichaka cha kujifichia tu.
Loh, kama kuna watu wana upeo mkubwa wa akili basi wewe ni namba wani. Unafikiri beyond, hongera kwa maelezo yaliyojaa herufi nyingi, hakika unasthiki kuombewa.
 
Mimi Nimejaza Fomu Ya Mkopo Na Sijaona Kipengele Hata Kimoja Unachojaza Kuwa Uliposoma Private School Ulilipiwa na Wazi Wako au Ulifadhiliwa na NGOs...
Bali Sharti Lilisema Kuwa Mkopo utatolewa Kwa →→ "Mean Test Value" ! Kwahiyo Ni Wazi Kuwa Huyo Jacqueline Kwamujibu Wa Taratibu Za Kupata Mkopo Basi Yeye Hastahiki Kupata hata Kama Ni Fukara kwa Sababu Alisoma Shule Ya Private ya Bei Mbaya! Kwani Serikali Katika Kuomba Mkopo Haikutaka Kujua Kwa Mwanfunzi Wa Private School Analipiwa Ada na Nani!!

Na Jambo La Pili Linalomkosesha Sifa Ya Kupata Mkopo ni Fani Anayokwenda Kusomea Ni Kuwa Haimo Katika →→"Priority Cluster 1 wala 2"!! Kwahiyo Hana Sifa Ya Kupata Mkopo Katika "First Batch".. Sasa itakuaje Waachwe Watu Wa Priority Kupewa Mkopo Kwanza na Apewe Jacqueline Ambaye Ni Non-priority??

Nadhani Mtoa Mada Utakuwa Una Uhusiano Wa Kifamilia na Jacq si bure...
 
Mitandao ya kijamii imezaa tabaka la watu wajinga na wap.umbavu kupindukia.
Nyani Ngabu na wewe Malisa Godlisten sasa naona akili zinaanza kuwakaa vizuri maana sisi tukisema mnasema ni wafia chama. Mungu ibariki CCM, Mungu Mbariki sana sana sana Dkt Magufuli, Mungu mbariki 100% Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Magufuli kwa kusimamia maadili yaliyokuwa yameanza kumomonyoka. Lazima tukubali nchi hii inahitaji kurudishiwa heshima yake, watu tunatakiwa tuwe wakweli!
 
Well sa
Shida yote hii ni mikopo mikopo hivi mtu unazaa wa nini kama huwezi kumsomeshaa?

Watu wanaleta viumbe kwa starehe zao afu wanaishia kuvipatia shida tu, Serikali duniani zina kazi kwa kweli, haingii akilini mtu aanze la kwanza, form one hadi six mzazi hujajipanga na kujiandaa kumuwezesha mwanao kusoma.

Mungu wape maisha marefu wazazi wangu japo si katika hali ya kujikweza au elimu za ghari sana ila kwenye suala la Elimu walijipanga mapema.

Binafsi sioni hasara kuishi duniani bila ya mtoto ambaye ni wangu ili hali sijaandaa mazingira yatakayomharahishia maisha yake, Japo hatuwezi kuzuia mambo mengine yanayoweza kutokea kinyume na matarajio yetu,ni muhimu dhamira,jitihada na bidii za makusudi ziwepo ili kiumbe chako kisije kuwa tegemezi either kwa serikali au kwa mtu.

Nawaonea huruma sana wanafunzi waliofaulu na wanaoshindwa kumudu gharama za masomo hii haikuwa mipango wala si mapenzi yao ni failure ya wazazi wao, Serikali imekuwa kichaka cha kujifichia tu.
Well said!!!
 
Huu ubaguzi katika mikopo ndio unazalisha wafanyakazi hewa. Unamkuta Mwalimu ambae hapendi kufundisha, Daktari asiependa kutibu na Mhandisi wa barabara anayechukia jua..

Kisa, walifuata mikopo.
 
Baada ya kusambaa kwa taarifa inayoonesha wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2016/17 kumejitokeza mjadala mkubwa juu ya jina la binti aliyejulikana kama Jacqueline Ndalichako, akidaiwa kuwa mtoto wa Waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako.

Mimi ni miongoni mwa watu waliohamaki baada ya kupata taarifa hiyo, na nikasema IKIWA NI KWELI JACQUELINE NI MTOTO WA PROF.NDALICHAKO basi inabidi Waziri huyo ajiuzulu. Hii ni kutokana na ukweli kwamba mtoto wa waziri hawezi kupata mkopo hata kama anakidhi vigezo vya kitaaluma. Mwongozo wa HESLB unamtaka mwanafunzi awe anatoka familia isiyojiweza kiuchumi, lakini mtoto wa Waziri hawezi kuwa kundi la wasiojiweza kiuchumi. Wapo watanzania wengi wenye uhitaji wa mikopo ya elimu ya juu kuliko watoto wa mawaziri.

#UKWELI_KUHUSU_TAARIFA_HIYO.

Baada ya kufuatilia nimegundua mambo yafuatayo:

1. Jacqueline si mtoto, ndugu wala hana unasaba wowote na Profesa Joyce Ndalichako, Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi. Ni ufanano tu wa majina, baina ya watu hawa wawili lakini ni watu wasiofahamiana kabisa.

2. Profesa Ndalichako hana mtoto mwenye jina Jacqueline, wala hana ndugu mwenye mtoto mwenye jina hilo.

3. Watoto wa Profesa Ndalichako walishahitimu elimu ya juu na hakuna yeyote anayejiunga na elimu ya juu kwa sasa.

4. Jacqueline amehusishwa na Prof.Ndalichako kwa sababu ya ufanano wa majina, lakini si watu wenye kufanana nasaba.

5. Jacqueline hakusoma HGL kama ilivyoelezwa. Amesoma EGM na amechaguliwa kusoma Shahada ya Uchumi na Takwimu (B.A in Economics and Statistics).

6. Jacqueline anatoka familia yenye uchumi wa kawaida hivyo anakidhi vigezo vya kupewa mkopo. Amesoma St.Mary Gorreti katika mazingira ambayo si vzr kuyaeleza hapa. (Nimefuatilia taarifa za familia ya Jacqueline inayoishi Yombo Dovya lakini nisingependa kuziweka hapa).

SWALI: Je waliosema Ndalichako awajibike wamekosea?

JIBU: Hapana. Hoja ilikuwa "Kama kweli Jacqueline ni mtoto wake basi awajibike". Hii ina maana kuwa hakukuwa na sababu ya kuwajibika kama si mwanae.

SWALI: Walioibua hoja ya Jacqueline kuwa mtoto wa Ndalichako wamekosea?

JIBU: Ndio. Walioanzisha hoja hii wamekosea kwa kuwa kuna viashiria kwamba walikusudia kupotosha. Hoja hii imepata nguvu mitandaoni na kusababisha usumbufu ambao ungeweza kuepukika.

[HASHTAG]#MyTAKE[/HASHTAG]:
Kwanza niwape pole Jacqueline pamoja na Prof.Ndalichako kwa usumbufu ambao kila mmoja ameupata.

Pili niwatake wote wanaoendelea kusambaza taarifa kuwa Jacqueline na Prof.Ndalichako ni ndugu waache kufanya hivyo maana wanaweza kupotosha wengine.

Ufanano wa majina si kigezo cha kuhukumu wasio na hatia pasipo uchunguzi. Bahati mbaya Jacqueline ameingia kwenye mijadala ya mitandao bila hatia. Amekuwa victim wa social media kwa sababu za kisiasa, ambazo yeye hahusiki nazo kabisa. Pia nimpe pole Prof.Ndalichako kwa usumbufu alioupata.

Ukweli ni kwamba kufanana majina ni jambo la kawaida katika tasnia yoyote. Wapo wanafunzi wengi waliopo vyuoni au waliochaguliwa kujiunga na vyuo vikuu wenye majina yanayofanana na viongozi wakubwa kisiasa lakini hawajahusishwa na viongozi hao.

Kuna mwanafunzi amechaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu Dodoma mwenye jina Gideon Wassira, lakini sijasikia akihusishwa na Mzee Stephen Wassira. Kijana Nobert Mbowe amehitimu Chuo kikuu Mlimani akisomea shahada ya Uhandisi wa madini (Mining Engineering) lakini hajawahi kuhusishwa na Mhe.Freeman Mbowe. Kuna mwanafunzi anaitwa Kennedy Yusuf Ndugai amechaguliwa shahada ya elimu maalum UDOM lakini hajahusishwa unasaba wake na Spika Job Ndugai.

Kwa hiyo nitoe wito watu waache kutumia habari inayomhusu Jacqueline kwa kumhusisha na Waziri Ndalichako maana ni watu wasio na uhusiano wowote kinasaba.

Najua wengi wamehamaki kusikia Jacqueline ni mtoto wa Waziri halafu kapewa mkopo huku watoto wa maskini wakikosa mikopo. Kumbe Jacqueline naye ni mtoto wa maskini pia, ila ameponzwa na ufanano wa majina na Waziri Ndalichako.

Nihitimishe mjadala huu kwa kutoa rai kwa "bloggers &social media emperors" kutokuendelea kujadili suala la Jacqueline na Waziri Ndalichako maana ni watu wasiofahamiana kabisa, achilia mbali kuhusiana kinasaba. Tumpe nafasi Jacqueline aweze kucocentrate ktk masomo yake, asiwe frustruted na mitandao. Let us end this discussion to save this innocent poor soul.!

Malisa GJ
'BILA YA UTAFITI TIMILIFU HUNA HAKI YA KUANDIKA'- Tuwache hearsays na kujumuisha mambo kwani mwisho wa siku unaweza kujikuta umefunguliwa kesi ya madai ya kumvunjia mtu hadhi yake mbele ya jamii kwa kuandika uvumi ambao hauna kichwa wala miguu.
 
Mimi Nimejaza Fomu Ya Mkopo Na Sijaona Kipengele Hata Kimoja Unachojaza Kuwa Uliposoma Private School Ulilipiwa na Wazi Wako au Ulifadhiliwa na NGOs...
Bali Sharti Lilisema Kuwa Mkopo utatolewa Kwa →→ "Mean Test Value" ! Kwahiyo Ni Wazi Kuwa Huyo Jacqueline Kwamujibu Wa Taratibu Za Kupata Mkopo Basi Yeye Hastahiki Kupata hata Kama Ni Fukara kwa Sababu Alisoma Shule Ya Private ya Bei Mbaya! Kwani Serikali Katika Kuomba Mkopo Haikutaka Kujua Kwa Mwanfunzi Wa Private School Analipiwa Ada na Nani!!

Na Jambo La Pili Linalomkosesha Sifa Ya Kupata Mkopo ni Fani Anayokwenda Kusomea Ni Kuwa Haimo Katika →→"Priority Cluster 1 wala 2"!! Kwahiyo Hana Sifa Ya Kupata Mkopo Katika "First Batch".. Sasa itakuaje Waachwe Watu Wa Priority Kupewa Mkopo Kwanza na Apewe Jacqueline Ambaye Ni Non-priority??

Nadhani Mtoa Mada Utakuwa Una Uhusiano Wa Kifamilia na Jacq si bure...
Maoni haya ni zaidi ya AKILI KUBWA,

MUNGU AWASAIDIE LIVERPOOL MSHINDE LEO.
 
I never argue with weak minded people like you. Soma andiko vzr, nimesema nimefuatilia familia ya Jacqueline pale Yombo Dovya na nimegundua mengi ambayo wewe na "wapayukaji" wenzio hamuwezi kuyajua. Kuna story ndefu sana nyuma ya pazia kuhusu Jacqueline kusoma St.Mary Goreti. Fuatilia kwanza kabla hujatoa mapovu.

Sasa mbona wewe ndio unapayuka? halafu mbona umetumia nguvu nyingi sana...ungeandika paragraphs tatu zingetosha kuliko kurudia rudia maneno
 
Back
Top Bottom