Jacqueline Kainja akubali kasi ya maendeleo Jimbo la Kaliua

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MBUNGE JACQUELINE KAINJA AKUBALI KASI YA MAENDELEO JIMBO LA KALIUA

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora Mhe. Jacqueline Kainja akiwa Kata ya Kamsekwa Wilaya ya Kaliua katika Uzinduzi wa Jukwaa la Wanawake amesema kuwa Kaliua imebadirika, siyo kama zamani kwani imepiga hatua kubwa kimaendeleo

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Tabora Mhe. Jacqueline Kainja amesifu na kupongeza utendaji kazi mzuri wa Mbunge wa Jimbo la Kaliua Mhe. Aloyce Andrew Kwezi kwa kuanisha mambo mbalimbali ambayo yameshafanyika katika Jimbo la Kaliua.

"WanaKaliua mna bahati sana, kupata Mbunge kijana, mchapakazi, mahiri, Aloyce Andrew Kwezi anafanya kazi zake vizuri. Kaliua ilikuwa na vumbi lakini leo hii Kaliua ni Lami na taa za barabarani" - Mhe. Jacqueline Kainja

"Mhe. Aloyce Andrew Kwezi anapambana kwenda kwenye Wizara za Ujenzi, Nishati kuongea na Mawaziri na watendaji wa Serikali ili kuhakikisha maendeleo ya wanaKaliua wenzake yanaenda vizuri. Vitu haviji vyenyewe, kwanini miaka mingine iliyopita havikuja?" - Mhe. Jacqueline Kainja

"Sasa hivi tunajionea kwa macho, tumshike mkono kijana wetu mkono. Wanaojipitisha msiwasikilize. Kuna mambo ya madarasa, Milioni 180 zimetengwa kwa ajili ya madarasa ya Sekondari Kata ya Kamsekwa na Mhe. Kwezi ameongeza Milioni 12" - Mhe. Jacqueline Kainja

"Kuna Milioni 400 kutoka Kazaroho hadi hapa Kamsekwa kwa ajili ya Barabara. Mhe. Kwezi kwa mahusiano yake mazuri, kijana mnyenyekevu na aliyejishusha hana makuu anaongea na Mawaziri vizuri kama Waziri Bashe. Mmeona wenyewe masoko ya Tumbaku mwaka huu mnauza bei ya juu haijawahi kutokea" - Mhe. Jacqueline Kainja


WhatsApp Image 2023-05-22 at 10.40.38.jpeg
 
Back
Top Bottom