Mbunge Kaliua, Kwezi Awataka Vijana CCM Kuwashughulikia Watu Wenye Kuwachafua Viongozi Mitandaoni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945
Akiwashukuru viongozi waliohudhuria katika tukio la usiku wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM KALIUA) na akitoa pongezi nyingi kwa DC wa Kaliua Dtk. Rashid Chuachua na Mwenyekiti UVCCM Kaliua Ndg Abubakar Kallah.

"Toka nimekuwa Mbunge hii sasa ni miaka mitatu na kwa hii miaka mitatu hili kwangu tukio la kwanza kwangu la vijana na tena limefanyika usiku na vijana mmekuja mmependeza" - Mhe. Aloyce Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua

"Mhe. Mkuu wa Wilaya uliponishilikisha katika hili nami nilikuwa tayari kulifanya nakushukuru sana kwa utayari wako tangu umefika Kaliua, Kaliua sio ile tuliyoizoea" - Mhe. Aloyce Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua

"Pia, namshukuru Mhe. Rais Mama Samia kwa kutoa fedha nyingi za maendeleo ya miradi aliyotuletea Kaliua yananifanya niweze kulala na kusubiri uchaguzi wa 2025" - Mhe. Aloyce Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua

"Rais anatupenda sana wanakaliua ametupatia shule ya wasichana "TABORA GIRLS GRAND SCHOOL iliyopo Wachawaseme yenye kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha sita ikiwa na majengo 30" - Mhe. Aloyce Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua

"Mliyoyaomba yote mimi nayapokea, tarehe 20 mwezi wa kwanza nitawapatia Tsh milioni 2 nilizowahaidi, hilo swala lenu la sare 20 (Kombat ) za Green Guard nalichukua mimi kama mlivyoomba" - Mhe. Aloyce Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua

"Vijana mna nguvu kubwa sana katika mitandao tunawaomba vijana wetu msiruhusu viongozi wenu watukanwe katika mitandao, ukiona mtu anamtukana Rais Dtk. Samia Suluhu Hassan kataa, Rais anatutendea yaliyo mazuri yanaonekana, Nyie ndio jeshi la Mama Samia na nyie ndio jeshi la Chuachua" - Mhe. Aloyce Kwezi, Mbunge wa Jimbo la Kaliua

Pia, Mbunge Aloyce Kwezi amefurahishwa na Teamwork ya Viongozi wa Kaliua chini ya Dkt. Rashid Chuachua na kuwasihi wanakaliua kuendelea kuwa na umoja na mshikamano huu.

WhatsApp Image 2023-12-20 at 15.34.22(1).jpeg
 
Usoni tu anaonyesha ni mkaanga sumu, atumie akili kidogo nayeye anakanyaga arhini.
 
mzaha mzaha huu tutajikuta tuna vikundi vya uasi sasa kujitetea na kulipana visasi..

Hao tunaowaona leo wako kwenye machafuko walianza kwenye huu huu ujinga.

Viongozi wetu wengi wanaonekana kichwani uwezo wao mdogo sana, na wengi wanakosa sana exposure ya dunia..

Hao green guard wakiendekezwa watajiona ni sehemu ya polisi, jeshi na hata tiss na matokeo yake yanaweza kuwa mabaya san, maana uonevu hauwezi kudumu milele bali huwa una mwisho na mwisho wake ni kisasi na visasi.

CCM na viongozi wake mnapaswa kusoma alama za nyakati na kubadili mtazamo na mbinu za kiutawala, kwa sasa ni akili ndio inatawala sio maguvu..
 
Back
Top Bottom