Huyu jamaa ni mshikaji wetu sana,Watanzania tusiombee hata kidogo aondolewe kwa maslahi mapana ya nchi yetu..
Tanzania na Afrika ya Kusini zimekuwa na uhusiano mzuri wa kihistoria uliojengwa katika mapambano dhidi ya utawala wa makaburu.Hapa ndio napasubiri
Zuma kaharibu mambo mengi na anazotuhuma nyingi tena zenye ushahidi wa wazi za ufisadi zinazotishia ustawi wa kisiasa na wa kiuchumi wa nchi yake.
Mambo ya Zuma yamesababisha kujengeka kwa kasi kwa chuki za kitabaka na ubaguzi wa rangi unaorudi kwa kasi. Amani na utulivu pia viko mashakani.
Endapo Zuma atang'ang'ania kuwepo madarakani itaharibu sana uchumi na ustawi wa Afrika Kusini. Na kuharibika huko hakutakuwa katika maslahi ya nchi yetu. Hatutafaidika nako bali kutatuathiri hata sisi pia.