Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 376,417
- 872,010
Afrika kusini imepoteza mvuto wake.. Rushwa uzembe na kulindana vimezidi... Zuma amelemewa na hana namna tena... Kikundi kinachoongoza hizo harakati kinamtaka Zuma afanye haraka kuondoka madarakani kabla hali haijawa mbaya zaidi
Akiwa kwenye Kilele cha kashfa za rushwa mwaka jana mwishoni aliponea kura ya kutokuwa na imani naye... Kura chache mno bungeni zilimuokoa.. Lakini safari hii ndio bai bai....
Kashfa maarufu zaidi ni
1. Kutumia mamilioni ya pesa za uma kujenga na kuboresha makazi yake binafsi... Hii kesi alishindwa na sasa analipa pesa yote aliyotumia KINYUME NA KATIBA YA NCHI
2. Mahusiano yake ya karibu mno na FAMILIA tajiri na yenye nguvu Afrika kusini, familia ya GUPTA... kwenye kashfa kubwa kubwa za mabilioni ya rand za serikali na miradi iliyopitishwa BILA RIDHAA YA BUNGE NA KWA MUJIBU WA KATIBA YA NCHI.. familia hii imekuwa ikihusishwa moja kwa moja, na imekuwa ikitumia ukaribu wake na rais hata kuathiri mipango mbalimbali yafisadi kwa manufaa binafsi...
Mwisho wake umefika na anayetarajiwa kuchukua mikoba yake ni mwasiasa na mfanyabiashara tajiri bwana Ramaphosa ambaye inasemekana ndio alikuwa chaguo la Mzee Madiba... Ramaphosa ameshaanza kuonesha kuwa anajitenga na fisadi Zuma... Na hivi karibuni akiwa kwenye kongamano la kimataifa akasema mwanzo mpya wa Afrika kusini unakuja
Je ninini kinaweza kumpata Zhuma kama akiondolewa madarani?
Labda tu kuwe na huruma na msamaha nje ya katiba lakini wakifuata taratibu Zhuma hatakuwa na kinga ya kutoshtakiwa... Jambo la kupandiswa kizimbani limeshaanza kujadiliwa kila kona.. Na hii itakuwa pigo kwake na washirika wake.... FAMILIA ya Gupta ikiwa mwathirika number moja
Jana ilikuwa siku ya rais Zhuma kuhutubia bunge lakini spika akatoa tangazo kuwa.. Imeahirishwa mpaka hapo itakapotangazwa tena... Haya yanatafsiriwa kama ni maandalizi ya mwisho ya kumtoa Zhuma madarakani
Je Tanzania tutaathirika kama Zhuma akipigwa chini? Itajulikana the soonest Lakini kwa sasa tuwe tayari kwa breaking news