Jacob Zuma asema Mugabe yuko kizuizini Zimbabwe

Jacob Zuma asema Mugabe yuko kizuizini Zimbabwe

kirerenya

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2013
Posts
1,699
Reaction score
2,261
zuma.jpg

Johannesburg, Afrika Kusini. Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe amewekwa kizuizini na Jeshi la Ulinzi usiku wa kuamkia jana katika mji mkuu wa Harare, Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amethibitisha.

Zuma alisema jana kwamba alipigiwa simu na Mugabe mwenyewe. Taarifa kutoka ofisi ya Zuma ilisema: "Rais Zuma alizungumza na Rais Robert Mugabe mapema leo na amedokeza kwamba anazuiliwa nyumbani kwake lakini alisema yuko salama."

Kuanzia Jumanne wanajeshi walionekana wakivinjari na kupiga doria katikati ya Harare, baada ya kuteka kituo cha televisheni cha Shirika la Utangazaji la Zimbabwe (ZBC) kwa kile kilichoelezwa wanawalenga “wahalifu”.

Hatua hiyo ya jeshi inaweza kuwa ni mpango wa kumwondoa Mugabe na kumweka katika nafasi hiyo makamu wake aliyefukuzwa kazi wiki iliyopita Emmerson Mnangagwa, shirika la BBC limeripoti.

Ofisa mmoja wa jeshi, Meja Jenerali Sibusiso Moyo alionekana kwenye televisheni baada ya kukiteka kituo hicho akisema Mugabe na familia yake wako “salama na afya njema na ulinzi wao ni wa uhakika ".

Meja Jenerali Moyo alisema, “Sisi tunawatafuta wahalifu waliomzunguka yeye (Mugabe) ambao wanafanya uhalifu na kusababisha machungu ya kijamii na kiuchumi nchini.”

"Mara tutakapokuwa tumekamilisha operesheni hii, tunatarajia kwamba hali itarudi kuwa ya kawaida."

Kufukuzwa kazi kwa Mnangagwa wiki iliyopita kutengeneza njia kwa mke wa Rais Mugabe, Grace kuteuliwa katika nafasi hiyo hivyo kuwa na matumaini ya kuteuliwa kuwa mrithi wa kiti cha mumewe.

Milio mizito ya bunduki ilisikika kaskazini mwa mji wa Harare hadi jana alfajiri.

Chanzo: Mwananchi
 
The People's Army aka Jeshi la Wananchi; hii ndio maana sahihi ya chombo hiki na sio kulinda watawala walioshindwa au wanaoharibu nchi.

CDF wa Zimbabwe na jeshi lake jinsi walivyoendesha hii operation bila kujeruhi hata sisimizi wamenipa raha sana; zaidi kibabu kimehifadhiwa pahala salama. We are fighting criminals sorrounding him causing social and economic difficulties in our country! So professional indeed.
 
Back
Top Bottom