Jacob sehemu ya II

Jacob sehemu ya II

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Baba yake Jacob alikuwa mfanyabiashara mwenye mafanikio makubwa. Yeye na mke wake walifanikiwa kumpata Jacob mwaka mmoja baada ya ndoa yao. Uzazi uliwaliwakimbia baada ya hapo lakini hayo hayakuwasumbua sana kwani walipendana mno na mkewe.

Jacob alikwa mtoto aliyependwa sana na wazawazi wake lakini hakudekezwa. Baba yake alimnunulia vitu gharama. Alianza kuwa na computer yake kama zawadi ya kufikisha miaka mitano. Baba yake alimnunulia baiskeli yenye gear zile zinazopanda milima kama zawadi ya kufikisha miaka kumi.

Watoto wa mtaani waliitamani sana ile baiskeli. Ingawa Jacob aliwapa nafasi ya kuiendesha lakini watoto wale walimtaka Jacob atoe baiskeli Jumamosi asubuhi washinde wakiendesha. Jacob alikuwa na majukumu ya kusafisha chumba chake na Jumamosi nyingi alishinda ofisini kwa baba yake akifundishwa kazi za kupanga ma file.

Siku moja akiwa anarudi kutoka dukani, watoto walijipanga wamnyan’ganye baiskeki yake. Jacob alikimbia huku akitetemeka na kwasababu hiyo aligonga jiwe na kuanguka kwenye barabara ya lami. Jacob alipoteza fahamu. Alipoamka alijikuta yuko hospitali akiwa amezungukwa na madaktari, manesi na wazazi wake.

Alikaa hospitali kwa miezi mitatu na ni baada ya mazoezi mengi ya mama cheza aliweza kutumia miguu yake tena. Hakutaka tena baiskeli baada ya hapo. Si muda mrefu baada ya ajali mzee aliaga dunia. Mama alinying’onyea sana kufiwa na mume.

Baada ya msiba ndugu wa karibu walimkalisha Jacob kumfahamisha kuwa yeye ndiye mwanaume wa kumtunza mama yake. Jacob alijifunza ku man-up.
Alivyokuwa kidato cha pili ndipo alipogundua matatizo ya kutopata erections, lakini aliman-up akijua hili litapita tu. Girl friend wake wa kwanza alimuacha wakiwa form four aliumia sana. Aliamua kujikita kwenye vitabu na masomo yake ili amkomoe yule msichana kwa matokeo mazuri
Jacob alifahlu vizuri na alikwenda kusoma ECA. Hakutaka kujiweka karibu na wanawake kuepuka aibu.

Mke wake alimshirikisha shost kwanza kwenye shida hii, shost alimshauri akanunue sexy nighties na perfume nzuri. Mke alijipulizia Jadore Jacob alihamaki kuwa ana allergy na perfumes. Shost akampeleka mke kwa Sangoma aliyewapa vumbi la Kongo hakukuwa na matokeo.

Ushost ulikufa pale shost alipoamua kumtafuta mwanaume wa kumkuna mke wa Jacob. Mke aliamua kusali rozari akimuomba Mungu. Jacob alimnunulia mkewe X6 mke aliikataa akisema yeye anataka sex si gari. Alimfahamisha daktari wa familia aliyewapa referral kwa neurologist.

Jacob aliambiwa matatizo yake yalitokana na ajali aliyoipata. Tiba inawezekana lakini anatakiwa awe kwenye hali ya utulivu. Alipata likizo ya miezi mitatu kazini na yeye na mke wake walikwenda kwenye resort huko milimani. Baada ya kutumia dawa kwa wiki nane aliweza ku perform his marital duties. Waliishi happily ever after.
 
Jacob kawa kidume sasa mm naona bora tukulane tu kabla ya chochote ili ijulikane mbivu na mbichi mtu anakwambia subili mpaka kwenye ndoa kumbe ana matatizo yake
 
Jacob kawa kidume sasa mm naona bora tukulane tu kabla ya chochote ili ijulikane mbivu na mbichi mtu anakwambia subili mpaka kwenye ndoa kumbe ana matatizo yake
Lakini mke wake ni shujaa, bila yeye Jacob asingepona
 
Lakini mke wake ni shujaa, bila yeye Jacob asingepona
Ni kweli mke wake kachangia kila kitu kwa mfano angemwambia ukweli toka mapema kuwa sisimamishi lakini sijui tatizo ni nini Jacob angeanza matibabu mda sana yote kwa yote ukweli jamani kuna vitu sio vya kumficha mwenzako
 
Ni kweli mke wake kachangia kila kitu kwa mfano angemwambia ukweli toka mapema kuwa sisimamishi lakini sijui tatizo ni nini Jacob angeanza matibabu mda sana yote kwa yote ukweli jamani kuna vitu sio vya kumficha mwenzako
Ninadhani ni matatizo ya kuwa mtoto wa pekee, hakuwa na mtu wa kumwambia siri zake. Hata mama yake Angeles’s kumsaidia.
 
Back
Top Bottom