SoC02 Jaa la mjini

Stories of Change - 2022 Competition

Shengesha

Member
Aug 31, 2022
5
0
Katika hali isiyo ya kawaida kumekuwa na wimbi kubwa la Imani potofu ambayo watu kutoka nje ya kisiwa Cha Pemba wanaifanya iendelee kuota mizizi siku hadi siku. Hiii ni kutokana na baadhi ya watu kuamini kuwa Pemba ndio kitovu au zizi la itikadi za matendo ya kishirikina hali ambayo imekuwa ikiwakereketa wapemba wenyewe baada y akuona ni kama wanadhalilishwa na kudharauliwa kwa kupandikizwa Imani za mambo ambayo ni kinyume hata na Imani ya dini yao wanayoiamini (Uislam).

Kwa dalili zilizo za wazi kuna baadhi ya wasaniii wametumia majina ya baadhi ya vijiji kisiwani humo Huku wakijibebesha nadharia za ubingwa katika matendo ya ushirikina.

Mfano: Kama umepata nafasi ya kuangalia filamu ya Kiswahili ambayo mhusika mkuu amebeba jina la Mkojani Ile ndo inatoa picha halisi ya hiki ambacho nakusudia kukizungumza.

Pia hata baadhi ya wasaniii wamuziki wameingiza mistari katika miziki yao inayojaribu kuihusisha Pemba Moja kwa Moja na Imani za kishirikina na kumaanisha kuwa Pemba ndio pekeee ina utaalam wa masuala haya ya Imani hizi .

Swali lakujiuliza: Ikiwa tamthilia na nyimbo hizi zinatazamwa na kusikilizwa na watu wa rika mbalimbali unahisi kunajengwa Imani gani kwa Rika la vijana na watoto ambao baadae ndio viongozi wa Tanzania ambapo Pemba pia ni sehemu ya Tanzania?

SI HALALI SI VIZURI TUKEMEEE KISIENDELEEE
PEMBA NI PAZURI WAPEMBA WANA USTAARABU PIA
WAPEMBA WANA IMANI YA DINI
PEMBA HAKUNA MATATA
 
Back
Top Bottom