J. K Nyerere: 'Malecela na Lowassa hawafai urais Tanzania'

EMT unaongoza KWA PUMBA. kiukweli kabisa kwa namna hii TZ ITAENDELEA KUJENGWA NA WENYE NCHI NA KULIWA NA WENYE MENO NA MITUMBO MIKUBWA. I REST MY CASE

Kama hupendi pumba acha kuandika pumba.

You better rest your pumbas.

And rest in peace too.
 
HONGERA LOWASA MAANA INAONYESHA CHENJI ZAKO SI TU SIMEWACHANGANYA WANACHAMA WA CCM AMBAZO ZILIKUA ZIKIGAWIWA VYOONI BALI PIA HATA WANACHADEMA HUMU JAMVINI WAMEONA CHADEMA TUPA KULE...CHEZEA HELA WEWE...LOL..DUU TZ tumefikia kudhalilishwa utu wetu namna hii!!! LEO NGOYAI KAGAWA MBUZI KWA KUTUMIA MAFUSO ARUSHA..MASKINI BVIZEE VYA KIMASAI HAVINA LA KUFANYA ZAIDI KUKUBALI KILA CHA LOWASA...

WENGI WANASHANGAA MBONA CHADEMA IMEFANYA HARAKATI KUBWA SANA WHY IMEAMBULIA KATA 5 TU..SASA MNATEGEMEA NINI IWAPO HATA WALE WAFURUKUTWA WALIOKUA MSTARI WA MBELE KULAANI RUSHWA NA KUISEMA CCM NA UFISADI SASA WAKO MSTARI WA MBELE KUMSAFISHA LOWASA KWA JIKI!!

NDO MAANA TUNASEMA CHADEMA NYIE NJAA TU MKIONYESHWA KIMKWANJA KIDOGO TU MNAPEPESUKA KAMA WALEVI...HA HA HA HA
 
NDO MAANA TUNASEMA CHADEMA NYIE NJAA TU MKIONYESHWA KIMKWANJA KIDOGO TU MNAPEPESUKA KAMA WALEVI...HA HA HA HA.......[/QUOTE]

Utatoa povu sana humu ndani huku ukitijitahidi kugawa watu kwenye makundi ya kisiasa but that will not justify ulichoandika. Hata ku-reason huwezi wewe. Hivi rushwa inayogawiwa chooni ni mbaya zaidi ya ile inayogawiwa uani?

Halafu kuonyesha mlivyo ovyo sana mlimuona anagawa rushwa mpaka chooni lakini mkamwacha tuu? Kwa nini msingemkamata mumpeleke kwa Nape?

Nenda kajipange upya. Don't thnk you can log in your first day (if is in deed true) and take people for granted. Kadanganye huko huko ulipotoka.
 
Tanzania sasa hvi tumeambukizwa na ugonjwa wa rushwa,yaani kwenye uchaguzi bila kutoa rushwa unaonekana hufai wakati wa Nyerere rushwa ilikuwa kigezo cha kukufanya ushindwe kuwa kiongozi wa umma,lakini sasa hivi mtoa rushwa anasifiwa tena kufagiliwa kama unavyoona wapambe wake wanavyohangaika kumtetea.

INABIDI CCM Lowassa waje na itikadi yao tuisikie,ccm dhaifu tumeishaijua ufisadi na kulalamika,ukiwaletea hoja ambayo hawawezi kuijibu unapelekwa mabwepande ukiwa na bahati(ULIMBOKA) au vitu vizito vyenye ncha kali kam kwa mzee Kamuhanda rpc wa Iringa.

Kama ingekuwa si sera yao leo hii asingekuwa ofisini baada ya kushuhudia na kusimamia mauaji ya mwandishi wa habari pale Nyororo.
 
Nafikiri wafuasi wako na kundi lako watakuelewa na kukupongeza kwa uliyoandika bila kuwa na ushahidi wowote. Nashangaa mbona hakufunguliwa kesi ya rushwa, kutumia vibaya madaraka, na huyo J. K. wako ambaye Mwalimu alimkubali kwamba hana doa mboa katuleta kwenye matatizo kiasi hiki. Mimi ni vigumu sana kukubaliana na mambo ya kusema Nyerere alisema, Nyerere hakuwa Mungu, mwenyewe alituletea umaskini wa kutisha mpaka tulipompata Mwinyi. Bora kumpata Rais mwenye pesa na maendeleo kuliko maskini atakayeanza kutafuta pesa akiupata urais atatupa shida sana huyo.
bora ya nyerere alikuwa na uzalendo na aliweza kuweka na kutetea miiko ya uongozi.sasa hivi ccm wanadai wanafuata siasa ya ujamaa na kujitegemea lakini kwa vitendo wanadhihirisha hilo?
Inabidi watanzania tuwe na value ambazo tunazienzi bora kumpata raisi mwenye pesa na maendeleo,sick.Hutaki hata kujua hizo pesa amezipataje?maendeleo unayoyasema hapa ni ya kwake na familia yake au ya watanzania?HATA UKIMCHUKIA LAKINI KWA UJINGA WA VIONGOZI WA CCM WALIOPO SASA WANAMFANYA AENDELEE KUWA BORA "MKE WA KAISARI HATAKIWI KUTUHUMIWA"hii ni kwa watanzania wenye uzalendo na nchi yao si mambumbumbu
 
Lowassa ni mrithi wa Kiukweli na sio maneno tu wa Hayati Sokoine, alimuuwa Sokoine kwa amri yake ni Nyerere kwani hakupenda watu wenye fikra za kimapinduzi dhidi ya siasa zake.

Sasa je wewe ungedhani Nyerere angemkubali Lowassa aka Sokoine aliemuua arudi haraka hivyo yeye akiwa hai? Akiulizwa mambo yake ya kuua au kuzamisha wenzake kama kikwete alivyotaka kumtosa Lowassa?

Sasa Nyerere keshakufa kwa hiyo Lowassa sio tishio kwake na siasa zake, na aje kutukomboa!
 
Lowassa ni mrithi wa Kiukweli na sio maneno tu wa Hayati Sokoine, alimuuwa Sokoine kwa amri yake ni Nyerere kwani hakupenda watu wenye fikra za kimapinduzi dhidi ya siasa zake, Sasa je wewe ungedhani Nyerere angemkubali Lowassa aka Sokoine aliemuua arudi haraka hivyo yeye akiwa hai? Akiulizwa mambo yake ya kuua au kuzamisha wenzake kama kikwete alivyotaka kumtosa Lowassa? Sasa Nyerere keshakufa kwa hiyo Lowassa sio tishio kwake na siasa zake, na aje kutukomboa!
 
ENZI ZA MWALIMU

MTU ukiwa mla rushwa unakula mboko 24. Mboko 12 wakati wa kuingia jela na mboko 12 wakati wa kutoka ukamwonyeshe mkeo. BUT SASA kua MTOA RUSHWA NDIO KIGEZO.... HA HA HA

ENZI ZA MWALIMU LOWASA ANGEKULA MBPOKO 1,240,000 Maana jinsi alivyo mla rushwa..Teh Teh
 
Hakuna wa kumzuia Lowasa ndani ya CCM iliyoja tamaa,fitna na ulafi,yeye ndio mtu pekee anayefit hali halisi ya chama,

nakuhakikishia kwa hela alizonazo lowasa atamhonga hata jk ampitishe na atapita ila swali la kujiuliza ni je ataweza kueleweka kwa watanzania??anauziaka???
 
Mimi nina rafiki zangu kazini ambao wanampenda kwa dhati Lowasa na wanaamini ye ndio atawatia adabu waislamu, uamsho na wenye ukabila. Wao hawajalipwa chochote na wanachoongea kinatoka moyoni mwao na naheshimu mawazo yao. KINACHONIBOA NI MTU KUTUMIWA ILI AWE PUNDA WA KUMUINGIZA MWINGINE IKULU BAADA YA KUPEWA CHENJI!....[/QUOTE]

Kujibu hoja unakimbia! Huna lolote zaidi ya kulinda kibarua!

Nenda hoja kwa hoja na remain objectively. Unaita wenzio wana njaa. LOL

Kajipange tena. Lete story mpya.

Vijana vijana. Wazee hatuna chetu? Hata kutafakari huwezi!

Hata e- ettiquettes hujui! Una shout tu! Pumba kibao

Kajipange
 
But hata 2005 Nyrere hakuwepo bali Malecela aligombea na akapigwa chini maana MAWAAZO YA NYERERE 1995 NDIO DIRA NA NI PRECEDENT!!!.....[/QUOTE]

Mkuu nimekubali. precedent iliyotumika kwa cigwiyemisi ndo itatumika kwa laigwanani. wamlete yoyote njia whiteee kwa CDM.
 
inawezekana akapita,maana mitandao ya hao jamaa balaaa..nyerere alikuwa na nguvu sana huwezi fananisha na kauli akitoa kikwete leo..nani ataongea jambo leo watanzania walisikie na walitilie manani kama nyerere?na hiyo kamati kuu inatoka wapi?si hapa2,sasa kwanini ashindwe kuwalubuni?
 
Nafikiri wafuasi wako na kundi lako watakuelewa na kukupongeza kwa uliyoandika bila kuwa na ushahidi wowote. Nashangaa mbona hakufunguliwa kesi ya rushwa, kutumia vibaya madaraka, na huyo J. K. wako ambaye Mwalimu alimkubali kwamba hana doa mboa katuleta kwenye matatizo kiasi hiki. Mimi ni vigumu sana kukubaliana na mambo ya kusema Nyerere alisema, Nyerere hakuwa Mungu, mwenyewe alituletea umaskini wa kutisha mpaka tulipompata Mwinyi. Bora kumpata Rais mwenye pesa na maendeleo kuliko maskini atakayeanza kutafuta pesa akiupata urais atatupa shida sana huyo.

Mko wengi humu,bado Pasco nae atachangia kama wewe!Ni ukweli usiokuwa na shaka kuwa JK hakuwa na doa mwaka 1995, lkn mwalimu alijua hatoshi ndio maana alisema huyu bado!Mkapa ndio alidhani ile bado imekuwa tayari, maana alipopewa nafasi mwaka 2005 (Hatujui mwalimu kama angesema huyu tayari) alishinda kwa asilimia 85 kiwango kikubwa kuwahi kufikiwa na rais yeyote TZ tangu uanze mfumo wa vyama vingi! Hata sie wengi wetu tulifurahi na kurukaruka na kwenda kupiga kura kwa mbwembwe, akatugeuka maisha bora hatukuyaona tukapata bora maisha mpk sasa hatujamsamehe!Lkn EL hata hajapewa nafasi tayari hatumtaki,jina lake ni kero kwa wengi wetu!Hakuna muujiza wa CCM kumpitisha labda kama wamechoka kutawala nchi!
 
MKUU UKO JUU... Huyo mgombea wao mwenyewe Laighwanan afya yenyewe mgogoro...hivi mmemuona anavyotembea???? ataweza kweli mikikimikiki ya uchaguzi???
Pia mjue tunachagua mtu ambae atakua Rais wa 2015-2025.....

Yani kila hoja inaenda against LAIGHWANAN~~~!!!
 
WAGOMBEA 17 WA CCM 1995


HARAKATI ZA E. LOWASA UCHAGUZI 2015


MKUTANO WA KAMATI KUU 2015
Kwa maoni yangu, huu ndio mkutano utakaomchinjia baharini Lowasa na rundo lake la wapambe nuksi. Lowasa na Malecela wanafanana sana (1. wote wana uchu SANA wa kwenda ikulu, wote wana rundo la wapambe, wote watakua wamegombea mara 2)Mwenyekiti JK atakua na kazi ndogo tu. Kwanza atawaonyesha mkanda wa Nyerere 1995 aliposema
1. Lowasa ni kijana mdogo mwenye utajiri wa kutisha
2. Mtu anaekimbilia Ikulu ni wa kuogopwa kama ukoma
3. Mke wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa.
4. JK ataonyesha video na minutes za kikao cha CC cha 2005 ambapo Mkapa alitumia hoja za Nyerere za 1995 kumchinjia baharini Malecela.

Hivyo wote mnaotumia JIKI kumsafisha Lowasa na njaa zenu mjue fika mgombea wenu hauziki. Hivi CCM ikimteua Lowasa kuwa mgombea je itakua imetoa picha gani kwa wanachama wake? Je wanachama wataweza tena kusema mbele ya watu kua CCM ni chama CHA WAFANYAKZANI NA WANYONGE??

Mtu pekee ambae angeweza kumsafisha Lowasa ni Nyerere tu vinginevyo sioni mwingine. Tukumbuke kua nchi imegundua uwepo wa Uranium, gas na oil hivyo kumpa mtu mwenye hurka na uroho wa mali kama Lowasa ni kuipeleka nchi pabaya.

Ni imani yangu watu wengi watachangia na kutoa maoni yao ili nchi ipate Rais anayefaa na sio mtu anayetumia hela kwa namna ambayo haijapata kutokea hapa nchini.

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!

Ndugu yangu GALIYA umeongea ukweli kabisa na ukweli mtupu. Lakini kama ulivyosema haya ni maoni yako. Na nadhani yataendelea kuwa maoni yako na wala si JK na wana CCM wake.

Mimi si mwana CCM lakini hata ningekuwa mwana CCM ningekiri wazi kuwa EL hafai kuwa rais wa nchi hii hata kwa siku moja! huyu jamaa ni mtu hatari sana; ni mtu anayeamini pesa kununua kila kitu! kununua utu, kumnunua kila mtu na kununua uongozi. Kama ulivyosema ni mtu anayeitafuta ikulu kwa hali na mali-sijui kwa lengo gani! Lakini Ni mtu aliyeonja tamu ya ufisadi ambayo sasa inamfanya awe na uwezo wa ku control watu kwa remote. Akipata madaraka ya urais atachonga mzinga.

EL Ni mmoja wa waasisi wa rushwa 'ya kitaifa na kimataifa' na ufisaidi wa hali ya juu akishirikiana na mapacha wake wawili- RA & Mzee wa vijisenti. Leo hii rushwa na ufisadi imekuwa culture na sera ya CCM. Rushwa na ufisadi vimeingia ndani ya mishipa ya damu ya CCM na kumuambukiza kila mwana CCM hadi ngazi ya chini, hadi mwanachama wa kawaida wa CCM anawaza kupata hongo ili atoe haki au kutoa hongo ili apewe haki yake. Marais karibu wote wa CCM wameingia madarakani kwa njia hii ya rushwa.

Kwenye hoja zako napingana na wewe kwa hoja moja tu; nataka kukuhakikishia kuwa ndani ya CCM EL is unstoppable for presidency. Ndani ya CCM hakuna mwenye uwezo wa kumzuia EL asipeperushe bendera ya CCM kugombea urais, not even JK! Kwa taarifa yako hata JK amepita kwa rushwa, na kwa bahati mbaya JK si mpambanaji dhidi ya rushwa au ufisadi. Kama si kwa ugonjwa, EL atakuwa ndie mgombea wa urais CCM. Kama nilivyowahi kusema hata wangekata vipi mtandao wake, anao uwezo mkubwa sana wa kujenga mtandao wake within no time. EL hamhitaji JK ili kuwa rais, na kwa bahati mbaya JK hana maamuzi au msimamo wa veto kama walivyokuwa watangulizi wake. Kama JK ana nia ya kumuengua asigombee urais, he is too late! Pale ambapo JK angeweza kumzuia EL asisonge mbele ilikuwa ni kutopendekeza jina lake kupita kugombea NEC.

Kitu nilicho na uhakika nacho wananchi wengi ambao si wana CCM, of course na baadhi ya wana CCM wachache, hawataki kumsikia EL.
 
Amini usiamini mawazo ya nyerere yanadumu vichwani mwa wajumbe wa nec. Na ni kama mizimu..................sio kosa sababu mi-afrika ndivyo tulivyo........cdm4legitimization of power 2015
 
Nafikiri si vibaya Lowassa kuwa Rais Kama Tanzania ina "Leadership Vacuum"! Nafikiri Tanzania haihitaji watu wakusafisha kwani walio safi wapo pia.
 
Kikao kitakacho mchinjia mbali Lowasa kitaongozwa na nani?au ni jk ambae alishawahi kusema kuwa urafiki wake na Lowasa si wakukutana barabarani.au ni akina Nape walioshindwa kumvuwa magamba baada ya Lowasa kuwa koromea kuwa yeye haondoki vinginevyo wakwanza kuondoka awe ni mwenyekiti wa chama kwa vile hakuna alicho kifanya bila mwenyekiti wachama kuhusika.baada ya kuambiwa hivyo na Lowasa jk na safu yake yote waliufyata na hakuna mtu anaethubutu kumnyoshea kidole Lowasa kuhusu kujivuwa gamba.kama walishindwa kumvuwa magamba Lowasa kutokana na udhaifu walionao ndani ya ccm huo ujasiri watautowa wapi?ili waweze kumchinjilia mbali Lowasa.hawa ccm naona hakuna msafi hata mmoja ndiyo maana wanamwona Lowasa ndie mwenye unafuu kiasi cha kuonekana kuwa ndie mtu pekee wakuweza kupeperusha bendera ya ccm pamoja na tuhuma kibao alizonazo.mwenye nguvu pekee ninaemwona kuwa anaweza kumdhibiti Lowasa ni mpiga kura na siyo ccm ambayo imejaa viongozi dhaifu kiasi cha kugeuzwa na Lowasa jinsi apendavyo.wapiga kura tusipoangalia tutajikuta tunampa urais Lowasa na baadae tukaambiwa kuwa sisi ni wajinga km Lowasa na Nyerere kama akifufuka kama alivyo ambiwa Kawawa kuwa asiwe mjinga kama Lowasa.
 
Galiya,

Umejitahidi? Nami nilisikia siku moja watu wanasema haya. Kama ni kweli kwa nini mshikaji ajisumbue? au CC ya sasa haitatumia usia wa baba wa Taifa?

WAGOMBEA 17 WA CCM 1995

Mwaka 1995, walijitokeza wagombea wanaccm 17 kuomba kuteuliwa kuipeperusha bendera ya ccm. Majina hayo yalipaswa kujadiliwa na vikao 3 ie CC, NEC na Mkutano Mkuu. Kikao cha kwanza kilikua ni CC. Mwenyekiti wa kikao alikua Mwenyekiti wa ccm A.H. Mwinyi. Baba wa Taifa Mwl Nyerere alialikwa ili asaidie shughuli hii pevu.

Nyerere bila kumungunya maneno wala kupepesa macho, kama ilivyo kawaida yake kwenye masuala ya kitaifa alisema wazi kuwa MALECELA NA LOWASA HAWAFAI KABISA KUONGOZA NCHI HII. Nyerere alisema Malecela ana madhambi mengi na ameyaweka wazi katika kitabu ambacho pia alielezea udhaifu wa Kolimba. Kuhusu Lowasa, Nyerere alisema baada ya kua amepewa file confidential na watu wa usalama-"Huyu kijana wa miaka 42 tu amepata wapi utajiri wote huu?? S. Sita ambaye alikua Compaign Manager wa J. Kikwete na E. Lowasa kwa pamoja aliinuka na kumtetea sana Lowasa hadi kufikia kusema hizo ni tuhuma tu hazijathibitishwa na pia kua Lowasa ana mvuto mkubwa kwa wananchi na anakubalika sana.

Baada ya kusikia "upuuzi" huu Nyerere hakusubiri Sita amalize hadithi zake alimkatisha na kumwambia "Mke wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa, na kama ni mzuri kanywe nae chai". Wana-CC wengine wajitahidi kuwatetea Lowasa na Malecela kwa nguvu kubwa maana tayari walikua na makundi. Kutokana na hilo Nyerere alisema "Niko tayari kurudisha kadi yangu ya chama, CCM sio baba yangu wala mama yangu. Kuna wagombea wana uchu sana wa kwenda Ikulu. Mimi nimekaa pale ikulu kwa miaka 25. Ikulu si mahali pa kupakimbilia, ni mzigo. Ukiona mtu anakimbilia ikulu ujue huyo ni wa kuogopwa kama ukoma hasa anapotumia pesa. Je amepata wapi hizo pesa na atazirudishaje??". Kutokana na tishio hilo pamoja na nguvu kubwa aliyokua nayo A. Mrema wa Nccr ilibidi wana-CC hao kunywea hivyo Malecela na Lowasa wakachinjiwa baharini. Majina 5 yakapelekwa NEC na hatimaye majina ma3 yakapelekwa Mkutano Mkuu (Mkapa, Kikwete na Msuya) na mwishowe Mkapa akachaguliwa kuwa mgombea wa CCM

UCHAGUZI WA 2005

Kama ilivyokawaida kikao cha kwanza cha kuchuja wagombea kilikua ni CC. Malecela, kwa mshangao wa wengi, naye pia aligombea na wakati huo alikua M/Mwenyekiti wa CCM. Kwa kutumia wadhifa huo, toka 1995 Malecela alizunguka nchi nzima na kufajhamiana na wajumbe wote wa vikao vyote muhimu hivyo wkt wa kuchukua na kujaza na kurudisha fomu yeye alikua wa kwanza kumaliza mchakato wote huo na takriban asilimia 85 ya wajumbe wa vikao vyote 3 walikua wanamkubali na Malecela mwenyewe na wapambe wake waliamini baada ya kifo cha Nyerere kusingekua na kikwazo tena. Mkapa,Mwenyekiti wa CCM alifungua kikao na kuwaonyesha alichosema Nyerere kuhusu Malecela. Wana-CC wengi walikumjegea hoja Malecela lakini hoja za msingi zilizojengwa na Mkapa na wengine kua chama kitashindwa kuonekana kinamuenzi Nyerere na pia itakua vigumu kumnadi MALECELA ambaye tayari alikua amechafuka. Hatimaye, kwa mara nyingine, Malecela akachinjiwa baharini. J. Kikwete ndiye akapererusha bendera ya ccm.

HARAKATI ZA E. LOWASA UCHAGUZI 2015

Licha ya Nyerere kusema Lowasa hafai na kwamba ni kijana mdogo mwenye utajiri mkubwa na mwenye uchu mkubwa wa kwenda Ikulu, Lowasa baada ya kujiuzuru uPM alianza jitihada kubwa mno za kutaka kuwa Rais wa TZ 2015. Katika jitihada hizo amefanya mambo mengi miongoni mwake ikiwa ni pamoja na 1. Kuweka mtandao mkubwa wa wapambe wake wakiwamo mawaziri lukuki waliomo kwenye Barza la mawaziri la sasa 2. Kuhakikisha kundi lake linaingiza watu wengi kwenye NEC 3. Kuhakikisha waCC na Wajumbe wengi wa mkutano mkuu nao wanakua upande wake 4. kugawa vyakula, kuku, ngombe mbuzi kama hana akili nzuri kwa watu na taasiis mbali mbali 5. kugawa na kuchangisha fedha kwa dini zote mbili ili asionekane mbaguzi 6. kutumia vyombo vya habari kumsafisha 6. kutumia wabunge mbalimbali kumsafisha na ikiwezekana mjadala wa Richmonduli urudishwe upya na pia amekua akiwalipa wetu wengi na vijana wake ili kumsafisha katika mitansao mingi ya jamii.

Lowasa amedaiwa kuwa ni fisadi mkubwa na kumekua na tuhumu kibao dhidi yake kama ifuatavyo
1. Amedaiwa kua ni mla rushwa mkubwa na kamwe hana moral authority kukemea rushwa
2. Amedaiwa alipokua AICC alitumia vibaya madaraka yake
3. Amedaiwa kua ni mgonjwa hivyo hawezi mikikimikiki ya uchaguzi na ya kuongoza nchi
4. Amedaiwa kutumia hela nyingi sana kuwaweka watu wake NEC hadi hela zilikua zikigawiwa vyooni, kwenye vibanda vya simu na kwa mama ntilie na vocha za simu
5. Anadaiwa akiwa Waziri wa Ardhi alitumia vibaya madaraka na kuuza viwanja hovyo hasa open spaces kwa wahindi
6. Ingawa alikua mtumishi wa serikali ana mahoteli mengi, majumba pamoja na jumba la ubalozi wa Africa Kusini.
7. Richmonduli
8. Ana utitiri wa vitega uchumi eg Alpha
9. Ni shareholder wa Vodacom analipwa 900M KWA MWEZI
10. Amekorofishana na swahiba wake JK

Hizi ni tuhuma ambazo ameshindwa kabisa kuzikanusha


MKUTANO WA KAMATI KUU 2015
Kwa maoni yangu, huu ndio mkutano utakaomchinjia baharini Lowasa na rundo lake la wapambe nuksi. Lowasa na Malecela wanafanana sana (1. wote wana uchu SANA wa kwenda ikulu, wote wana rundo la wapambe, wote watakua wamegombea mara 2)Mwenyekiti JK atakua na kazi ndogo tu. Kwanza atawaonyesha mkanda wa Nyerere 1995 aliposema
1. Lowasa ni kijana mdogo mwenye utajiri wa kutisha
2. Mtu anaekimbilia Ikulu ni wa kuogopwa kama ukoma
3. Mke wa Kaisari hapaswi kutuhumiwa.
4. JK ataonyesha video na minutes za kikao cha CC cha 2005 ambapo Mkapa alitumia hoja za Nyerere za 1995 kumchinjia baharini Malecela.

Hivyo wote mnaotumia JIKI kumsafisha Lowasa na njaa zenu mjue fika mgombea wenu hauziki. Hivi CCM ikimteua Lowasa kuwa mgombea je itakua imetoa picha gani kwa wanachama wake? Je wanachama wataweza tena kusema mbele ya watu kua CCM ni chama CHA WAFANYAKZANI NA WANYONGE??

Mtu pekee ambae angeweza kumsafisha Lowasa ni Nyerere tu vinginevyo sioni mwingine. Tukumbuke kua nchi imegundua uwepo wa Uranium, gas na oil hivyo kumpa mtu mwenye hurka na uroho wa mali kama Lowasa ni kuipeleka nchi pabaya.

Ni imani yangu watu wengi watachangia na kutoa maoni yao ili nchi ipate Rais anayefaa na sio mtu anayetumia hela kwa namna ambayo haijapata kutokea hapa nchini.

MUNGU IBARIKI TANZANIA!!!
 
Back
Top Bottom