VIJANA WENZANGU MMENIANGUSHA BIG TIME!!
Mimi nikiwa Mzalendo wa nchi yangu niliteta mada hii baada ya kuambiwa na wenzangu kua humu kuna GREAT THINKERS..NASIKITIKA nilichoshuhudia humu ni tofauti kabisa na nilivyotegemea. Mimi nilieleza ni kwanini nadhani LOWASA HAFAI KABISA kua RASI wa nchi yangu niipendayo ya Tanzania. Sasa nilitegemea kwamba wale wote ambao wanaona anafaa basi wangejikita kueleza mazuri ya Lowasa ili baadae tuchambue kama pamoja na mabaya niliyoyataja lakini mambo mengine ya Lowasa ni mazuri.
Mimi sina kambi wala mtu yoyote ninayemuunga mkono. Nina uelewa na yale yaliyofanyika katika vikao vya CCM, NEC na Mkutano Mkuu maana kuna mmoja wa Vigogo ambae alihudhuria vikao vya 1995 na vya 2005 ingawa kwasasa hayumo tena. Mi naona ni vizuri kila mgombea anayetajwa kuutaka Urais basi AJADILIWE KWA MAPANA NA MAREFU ili hatimaye TUMPATE KIONGOZI BORA AJUAE MATATIZO YETU NA AMBAYE ANA UWEZO WA KUYATATUA NA SI YULE AMBAE NAPELEKA TUMBO LAKE MBELE.
Iwapo topic itamuhusu MIGIRO AU MEMBE AU SITA AU NCHIMBI AU MWAKYEMBE BASI WOTE TUJADILI UZURI NA UBAYA WA MTU HUYO BILA KUTAJA WENGINE .
TUSIKUBALI KUBURURWA NA WENYE MAKUNDI. NCHI HII INA WATU 45 000 000. JE HAKUNA WENGINE WANAOFAA ZAIDI YA HAWA TUNAOWASIKIA??? MAWAZIRI AU MABALOZI HAWAPO KWELI? KWELI? MKAPA ALIKUA HAJULIKANI 1995 LAKINI NDIYE ALIYEPATA..DID WE LEARN ANYTHING FROM THAT EXPERIENCE???
Mimi nina rafiki zangu kazini ambao wanampenda kwa dhati Lowasa na wanaamini ye ndio atawatia adabu waislamu, uamsho na wenye ukabila. Wao hawajalipwa chochote na wanachoongea kinatoka moyoni mwao na naheshimu mawazo yao. KINACHONIBOA NI MTU KUTUMIWA ILI AWE PUNDA WA KUMUINGIZA MWINGINE IKULU BAADA YA KUPEWA CHENJI!
Acha unafiki na kutuzuga hapa. Hakuna mzalendo nchi hii. Kungekuwa na wazalendo nchi isingeliwa kihivi. Mpaka wafagiaji wamekuwa mafisadi ndiyo sembuse Lowassa? Pia usidhani wote hapa ni vijana. Kuna vibabu humu pia. So, heshima mbele tafadhali.
Yes, humu kuna great thinkers. Lakini kwa taarifa yako, kama ulikuwa hujui, great thinkers huwa wanajadili hoja, siyo watu. Great thinkers huwa wana-argue objectively, siyo subjectively. Great thinkers use their brains and analyse issues critically, siyo kuokota habari za zamani na kuziweka hapa.
Great thinkers provide solutions to the issues being addressed, siyo kama wewe uliyesema Lowasa hafai bila kutoa alternative. Kama Lowassa hafai unampendekeza nani then and why? Great thinkers hawaandiki kwa hasira kama wewe inavyoandika kwa herufi kubwa. Calm down.
Unasema eti wewe huna kambi wala mtu yoyote unayemuunga mkono. Unatuchukulia for granted kuwa sisi tuna kambi na tunamuunga mkono Lowassa simply because tunapinga your recycled thread?
Unasema eti una uelewa na yale yaliyofanyika katika vikao vya CCM, NEC na Mkutano Mkuu. Hivi ni Mtanzania gani ambaye hayajui hayo? Kwa nini mnapenda kuwadharau Watanzania kiasi hiki? Yaani bado unadhani tuko dunia ya 47 ambapo mnaweza ku-hold information na kuzi-release pale mnapojisikia?
Kwako umeona umetoa inside information ya maana, kumbe ume-recycle tuu. Tena hata hiyo recycling uliyofanya ni hearsay maana unadai "kuna mmoja wa Vigogo ambae alihudhuria vikao vya 1995 na vya 2005." Ndiyo maana kwenye thread yako umeweka quotations za Nyerere ambazo hata hakuzisema kwenye hiyo mikutano. Watu watakuletea minutes zote za vile vikao hapa utashangaa na roho yako.
We don't believe on hearsay hapa. Kajipange upya.