J J Mnyika alikuwa Waziri kivuli wa Nishati katika Serikali ya awamu ya 5. Je, anasemaje kuhusu mgao wa Umeme?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,968
141,979
Katibu mkuu wa Chadema mh J J Mnyika alikuwa waziri kivuli wa Nishati katika serikali ya awamu ya 5.

Labda atueleze uzoefu wake katika kulisimamia na kulishauri shirika letu la umeme wakati akihudumu kama waziri kivuli.

Mnyika ni mtu anayeheshimika hivyo tunasubiri ufafanuzi wake tukizingatia wakati wake hapakuwa na mgao wa umeme.

Maendeleo hayana vyama!

cc: bwashee Tindo
 
Samahan hiv kaz ya waziri kivuli huwa ni nini? Maana hii kitu naisikia tu
 
Jambo la msingi ni kuwa tatizo linatengenezwa ili baadae lije suluhisho. Suluhisho ambalo ninaamini linaweza kuambatana na vilio vya walio wengi.
Service charge unit kupanda gharama n.k

Au tuite wataalamu kutoka nje walete mvua ya kubumba
 
Katibu mkuu wa Chadema mh J J Mnyika alikuwa waziri kivuli wa Nishati katika serikali ya awamu ya 5.

Labda atueleze uzoefu wake katika kulisimamia na kulishauri shirika letu la umeme wakati akihudumu kama waziri kivuli.
Mnyika ni mtu anayeheshimika hivyo tunasubiri ufafanuzi wake tukizingatia wakati wake hapakuwa na mgao wa umeme.

Maendeleo hayana vyama!

cc: bwashee Tindo
Mlivyowaondoa kwa hila si mlitaka wasiseme? Sasa unataka asemeje? Mtajijua wenyewe
 
Mnyika ni Katibu Mkuu asie na meno,kama ni mbwa basi asiebweka,kama ni nyoka basi LA kibisaa.

Mnyika wa Chuo kikuu kabla ya ubunge na mnyika wa enzi za spika Makinda ukilinganisha na wasasa ni watu wawili tofauti kabisa.
Labda kaamua kutulia kula mema ya nchi sio mbaya lakini unafanya kazi kwa malengo sio ili mradi tu.
 
Awamu ya 5 walikuwepo Bungeni. Je umeme ulikuwa ukikatika hovyo kama awamu hii?? Mlikuwa mkifikiri mnawakomoa Upinzani hasa Chadema. Pambaneni wenyewe huko.

Choko choko za nn wakati watumiaji wa umeme ni Chadema??

Nchi hii imeharibiwa vya kutosha na CCM. M/Kiti wake Taifa aliwaambia vijana na kina Mama wajiajiri kama Wamachinga. Akawapa na vitambulisho ili wasibugudhiwe na yeyote. Alikusanya Fedha za kutosha toka kwao. Baadae M/Kiti Taifa wa Chama kile kile kawaona hawafai kufanya biashara mijini kwani ni kero kwa walipa Kodi wengine, wakasahau Ile tozo ya 20k kwa kila machinga.

Baadhi ya vijana waliamua kutimkia nje ya miji/vijijini. Wakaanzisha kilimo cha umwagiliaji. M/Kiti Taifa wa Chama kile kile akajitokeza na kusema waondolewe mara moja kwani wanaharibu vyanzo vya maji. Na wale ndugu zetu wa mikoa ya kanda ya ziwa waliowekeza kwenye ufugaji wa ng'ombe wakaambiwa eti kwakuwa ng'ombe mmoja hunywa Lita 40 za maji kwa siku hawafai tena kwani watakauasha maji yanayototiririka kwenye mabwawa ya kuzalishia umeme. Kwa tafsiri nyingine ng'ombe wale wanaweza kukausha maji ya Ziwa Victoria.

Sasa wewe nikuulize: Awamu zilizopita kulikuwa hakuna wafugaji na wakulima?? Tukiwaambia mmechoka hamsikii. CCM haina mbinu tena ya kuwasadia raia wa nchi hii. Kila siku matamko yanayoambatana na vitisho toka kwenye vyombo vya dola.
 
Awamu ya 5 walikuwepo Bungeni. Je umeme ulikuwa ukikatika hovyo kama awamu hii?? Mlikuwa mkifikiri mnawakomoa Upinzani hasa Chadema. Pambaneni wenyewe huko.

Choko choko za nn wakati watumiaji wa umeme ni Chadema??
Wewe hutaki mwanga?
 
Katibu mkuu wa Chadema mh J J Mnyika alikuwa waziri kivuli wa Nishati katika serikali ya awamu ya 5.

Labda atueleze uzoefu wake katika kulisimamia na kulishauri shirika letu la umeme wakati akihudumu kama waziri kivuli.

Mnyika ni mtu anayeheshimika hivyo tunasubiri ufafanuzi wake tukizingatia wakati wake hapakuwa na mgao wa umeme.

Maendeleo hayana vyama!

cc: bwashee Tindo
Hata akisema hawatasikiliza
 
Back
Top Bottom