Ivii Umewai kujiuliza Internet Shutdown Inavyofanya Kazi Yaani kujiuliza Kwanini ghafla unakuta WhatsApp, Insta au net nzima Imekata Internet Shut

Ivii Umewai kujiuliza Internet Shutdown Inavyofanya Kazi Yaani kujiuliza Kwanini ghafla unakuta WhatsApp, Insta au net nzima Imekata Internet Shut

its MalekoGJ

Senior Member
Joined
Aug 27, 2020
Posts
135
Reaction score
285
Ivii Umewai kujiuliza Internet Shutdown Inavyofanya Kazi

Yaani kujiuliza Kwanini ghafla unakuta WhatsApp, Insta au net nzima Imekata

Internet Shutdowns ni moja ya silaha ya serikali nyingi za Afrika.

Hii siyo net tu kukatika, ni maamuzi ya makusudi kudhibiti taarifa au kukata mtiririko wa data kwa wananchi.

Mara nyingi hutokea kwenye uchaguzi, maandamano au wakati wa presha kisiasa.
Shutdown inaweza kuwa ya muda mfupi au mrefu, kulenga platform fulani (WhatsApp, Insta, X), au kuzima nchi nzima.

Lengo kubwa?

👉🏽 Kudhibiti taarifa zinazosambaa.
Lakini effect yake huumiza zaidi jamii na uchumi kuliko kusaidia kama Ambavyo Serikali ya Ccm Wakiongozwa Na Kijana wao

Sasa swali ni, wanazifanyaje shutdown hizi kiteknolojia?
Kuna njia mbili maarufu

1. Routing disruptions
2.Packet filtering

Routing disruptions
Kila kifaa chenye internet kina IP address. Ili mitandao icheze vizuri, kuna kitu kinaitwa Autonomous Systems (AS)
hizi ni networks kubwa (kama ISP zako).
Wanatumia Border Gateway Protocols (BGP) ili kuoneshana njia za kufika websites na servers mbalimbali.

Hapa fikiria internet kama barabara kubwa zinazounganisha miji tofauti.

1.Mji hapa ni ISP (makampuni ya internet kama Airtel, TTCL, Vodacom).

2.Barabara kuu ni Border Gateway Protocol (BGP) – ndiyo ramani inayoonesha magari (data) zipite njia gani.

Kila kifaa chako (simu, laptop) kina anwani yake (IP address). Ili kufika WhatsApp au Google, inahitaji kupitia kwenye barabara (routes) zilizo kwenye ramani ya BGP.

Sasa, serikali ikiamuru ISP

“Ondoeni hizi barabara kwenye ramani ya dunia ya internet,” mara moja, hakuna gari (data) litakalofika popote.
Watumiaji wa ISP hiyo hawataweza kuingia WhatsApp, Google, au website yoyote kwa sababu ramani yao imefutwa.
Njia Hii Imetumika sanaa nchini Misri na ata hapo Nepali Juzi thats

Blackout ya Misri 2011 ilijulikana, ilitoka kwa manipulation ya BGP na ilitrace moja kwa moja kwa providers.

Lakini hii style ya routing disruption ni too loud. Ni rahisi kugundulika na inaweza kuharibu uchumi mzima. Hivyo, mara nyingi hutumika wakati serikali inataka blackout kubwa, bila kujali loss.

Packet Filtering
Hapa ndo mambo yanakuwa selective. Serikali haitazimi net nzima, bali inalenga apps au sites fulani.

Mfano: ISP wakiblock IP ya WhatsApp (mfano 15.197.206.217), basi app nzima inakuwa unreachable............kama Walivyotufanyia Bongo hapa

Piaa kuna Deep Packet Inspection (DPI).
Hii inachambua data packets zako moja kwa moja siyo tu IP.
Inatumika kwa
1. surveillance,
2.kuchuja keywords,
3.kublock platforms kama

Senegal 2023 walitumia hii kusimamisha WhatsApp, Telegram, Insta n.k.

Tofauti na routing disruptions, packet filtering ni stealthy Yaaani mtu anayeumia ndani ya network ndio atagundua. Ndio maana researchers hutumia active probing kuverify shutdowns.

Zaidi ya hizi njia mbili
Serikali pia hucheza na:
•DNS manipulation (kubadilisha anwani za websites),
•Denial of Service (DoS),
•hata physical sabotage (kukata fiber cables).

Kiini cha yote: Internet shutdowns ni uvunjifu wa haki za msingi uhuru wa kujieleza na kupata habari na ata Uhuru wa kiuchumi kwa Vijana walio amua kujiajiri kupitia Mitandao

Ni njia ya kuficha tatizo badala ya kulitatua.

Na kiuchumi? Ni hasara kubwa sana kwa biashara, innovation, na trust ya kimataifa

Dear Ccm
Keep It On.
Kama kuna challenge kisiasa au kijamii, solution siyo kukata intaneti. Kuzimwa kwa mitandao kama X kunaua demokrasia, kunavuruga jamii, na kunaharibu future ya kiuchumi

Internet shutdown ni silaha ya karne hii. Lakini kila mtu anatakiwa kufahamu mechanics zake ili tujue jinsi ya:
1.Kuzipinga,
2.Kuzipita (circumvent),
3.Kuwawajibisha wanaozifanya.

👉🏽 Internet ni haki ya msingi, sio favour au Huruma ya serikali

Jobless Muuza laptop Check hapo Chini
 
Hicho ni kitufe tu flani kidogo, mtu akimka kwao amevimbiwa makande tumbo linamsumbua, anaamua kufyatua tu paaa! Karaha na tabu za kitambi chake mzipate wote...
 
Back
Top Bottom