Ivi watanzania Nani katuroga?

ngulyavyangu

JF-Expert Member
Jan 9, 2019
203
266
Leo ndio nimeanza kumuelewa mh mkuu wa mkoa na dar es salaam ndugu Paul makonda.
Nimeanza kumuamini kwamba watz tunafurahia vitu vya hovyo na vitu vya msingi hatuvipi nafasi..

Leo katika zunguka zunguka yangu kwenye mtandao wa instagram nikabahatika kukutana na post ya mwanadada mwigizaji na mfanyabiashara, faiza ally.
Bidada huyu ameandika kwa uchungu jinsi Wakenya wanayo waaaminisha watu huko ughaibuni kwamba Mlima kilimanjaro upo Kenya,.
Sijashangazwa Sana na ili jambo Kwani kwa record nilizonazo ni kwamba Wakenya wanaonekana ni watu wa kutumia fursa na watz tumelala pono tukiwa hatuna Habari,
Kila kizuri cha tz Wakenya lazima wanufaike nacho mfano madini ya tanzanite dunia yanapatikana tz peke yake ila Wakenya ndio wafanyabiashara wakubwa wa madini Hayo, tena wao wananufaika zaidi yetu.

Nimejaribu kuingia kwenye page ya muheshimiwa waziri wa Maliasili na utalii post yake ya mwisho amempost Pierre na caption ndefu ya kumpatepate.
Apo ndipo nilipoamini Mh makonda Yupo sahihi, Yaani Wakenya wakiwa busy kuutangaza mount kilimanjaro kwamba upo sisi watanzania pamoja na viongozi wetu tuko busy kumtetetea mlevi Pierre liquid!!

Leo Hii Idadi kubwa ya wataliii wanaingia Kenya zaidi ya tz.. Sio kwamba Kenya wanausalama wa kutosha, La hasha! Sio km Kenya wanavivutio vizuri zaidi yetu, Yawezekana ivi ivi vya kwetu tunakula nao sahani Moja.
Wao wanachokifanya ni kuitangazia dunia kwamba kile kitu kizuri kipo Kenya,utalii ni matangazo, usitegemee upate wataliii Wakati autangazi vivutio vyako.

Mkenya anajua kutumia fursa, Sie Hawa wasanii wetu tunaona wanini ila wao wanavutia kwao, utasikia eti diamond ni mkenya, sijui professor Jay ni mkenya, AY n. k
Unajua Kwanini? Kwasababu wasanii wananafasi ya kuitangaza nchi kimataifa, ila sisi hatulijui ilo kazi yetu ni kuingia kwenye page zao na kuwatolea maneno machafu na yakukatisha tamaa, huyu diamond angekua mkenya angekua mbali Sana kimuziki coz Wenzetu wanasapotiana, ila sisi tupo tayari kumtetetea liquid kuliko kumtetetea diamond anayelitangaza taifa.

Tuamke watanzania majirani wataendelea kunufaika na rasilimali zetu hadi lini?

Muda sasa Umefika kuitangazia dunia kwamba Mlima kilimanjaro upo Tanzania.

Muda sasa wa kuwaambia Wakenya kwamba mmenufaika na lasilimali zetu kwa miaka mingi sasa inatosha.

Muda sasa umefika watanzania tuache kushabikia Ujinga,

Muda sasa Umefika watanzania tutumie mitandao ya kijamii kuitangaza mazuri ya nchi yetu

Nakupenda Tanzania
Nakupenda nchi yangu
2012896836861054647.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diamond angekua mkenya angekua mbali? Kisa wanasapotiana?

Wana wanamuziki na wasanii wangapi ambao wameshindwa kuwasapoti?

Kwenye swala la kutangaza Kilimanjaro ipo kwao sina la kusema.
 
kama umeanza kumuelewa makonda labda na wewe akili zako zitakuwa na mlengo huo,usichoke endelea kumuelewa!
 
Ndio angekua mbali, tukiachana na matatizo yao ya ukabila, Wakenya ni watu wanaoona fursa na kunitumia,
Wakati sisi tunamfungia diamond asifanye matamasha Humu ndani kisa wimbo wa nyegezi wakenya wanamkaribisha, anaperfom wanachukua kodi,
Ivi ushajiluiza washabiki wa music wa Kenya wanamakundi km sisi? Ndipo utaelewa Kwanini nakuambia diamond angekua mbali
Diamond angekua mkenya angekua mbali? Kisa wanasapotiana?

Wana wanamuziki na wasanii wangapi ambao wameshindwa kuwasapoti?

Kwenye swala la kutangaza Kilimanjaro ipo kwao sina la kusema.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio angekua mbali, tukiachana na matatizo yao ya ukabila, Wakenya ni watu wanaoona fursa na kunitumia,
Wakati sisi tunamfungia diamond asifanye matamasha Humu ndani kisa wimbo wa nyegezi wakenya wanamkaribisha, anaperfom wanachukua kodi,
Ivi ushajiluiza washabiki wa music wa Kenya wanamakundi km sisi? Ndipo utaelewa Kwanini nakuambia diamond angekua mbali

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwahiyo haujui kama Kenya umeufungia wimbo fulani wa Diamond ila pia wanamtuhumu kukwepa kodi?
 
Ndio angekua mbali, tukiachana na matatizo yao ya ukabila, Wakenya ni watu wanaoona fursa na kunitumia,
Wakati sisi tunamfungia diamond asifanye matamasha Humu ndani kisa wimbo wa nyegezi wakenya wanamkaribisha, anaperfom wanachukua kodi,
Ivi ushajiluiza washabiki wa music wa Kenya wanamakundi km sisi? Ndipo utaelewa Kwanini nakuambia diamond angekua mbali
Sent using Jamii Forums mobile app
hao hao ndio wamemfungia Diamond asifanye show kwao Kenya uwe unafanya research kabla uja post Watanzania unao tuzalau tunaishi vizuri kuliko Wakenya sisi ndio tunachota ela zao kuanzia kwenye sanaa chakula na gas n.k hao unao wasifia wana kufa na njaa..Kama ni fursa tumezitumia ipasavyo
 
Wewe hujaelewa kitu, watu walichukizwa na kitendo cha makonda kutoa maneno yasiyo mazuri kwa mualikwa mwenzake badala ya kuhamasisha michango, pale hapakuwa mahali sahihi kutoa maneno ya hovyo kwa mtu ambaye hajakuomba ushauri au kwa makampuni yaliyompa tenda za matangazo
 
Mkuu huwajui Wakenya vizuri embu jipe muda uwafanyie ushushu ndio utagundua ni kiasi gani walivyotuzidi katika hili swala la kuvipa kipaumbele vitu vya hovyo hovyo
 
Back
Top Bottom