Ivi umeshawahi kujiuliza

Chauro

JF-Expert Member
Aug 20, 2010
2,968
1,476
ivi ni kwanini unapokuwa kwenye matatizo ndo usumbufu wa maisha huzidi

1. unapokuwa kwenye uhusiano mbovu watongozaji nao humiminika kama maji ya mvua

2.ukiwa huna hela ndo habari za matatizo hujaa kwa wingi.

na matatizo mengine mengi ivi hii husababishwa na nini au unapokuwa na shida huwa nyuso zetu huwa hazifichi yaliyomo ndani ya mioyo na wajanja hutafuta sehemu ya kuhemea

haya maswali yamekuwa yananisumbua sana ilo la kwanza kina kaka /baba naomba michango yenu kina dada pia embu toeni mauzoefu yenu
 
Wanakuwa wanasubiri pale kwenye matatizo ndo wanaposhikia.

Hata ukiwa kwenye ndoa kibao wanakufata ngoja uachike wanakucheka hawakutaki tena
 
dena ni kwamba ukiwa huna shida utawasikia kwa machale ngoja misongo ya mawazo ije mpaka utashangaa,mpka waliokuwa kwenye maboksi ivi wanaume nao hukutwa na hali hii au ni kina dada tu .
 
dena ni kwamba ukiwa huna shida utawasikia kwa machale ngoja misongo ya mawazo ije mpaka utashangaa,mpka waliokuwa kwenye maboksi ivi wanaume nao hukutwa na hali hii au ni kina dada tu .

Mie nadhani wanatumia ule msemo kuwa wenye afya hawamuhitaji dakitari au mweye shide haitaji chakula.

So unamatatizo ndo wanakujia kwa wingi wako hivyo
 
Yaani uliyosema ni kweli kabisa, ndio inakuwa nuksi kabisa, hata wale marafiki uliokuwa nao wanakukimbia, mbali na watu unaowadai hawalipi madeni, maadamu vurugu katika maisha.
cha msingi ni kujipa moyo na kutafuta suluhisho na sio kukurupuka unaweza kutoa maamuzi ambayo yataendelea kuleta shida zaidi.
 
naona kina baba wamekimbia kutoa maoni yao siwaoni
 
unaweza kuona dunia imekuinamia inahitaji utulivu wa hali ya juu kufanya maamuzi yoyote kipindi hiki lakini ndo ivo vurugu nazo zinapamba moto.

Yaani uliyosema ni kweli kabisa, ndio inakuwa nuksi kabisa, hata wale marafiki uliokuwa nao wanakukimbia, mbali na watu unaowadai hawalipi madeni, maadamu vurugu katika maisha.
cha msingi ni kujipa moyo na kutafuta suluhisho na sio kukurupuka unaweza kutoa maamuzi ambayo yataendelea kuleta shida zaidi.
 
Ibilisi aka shetani huwa anatenda kazi zake za ki intelijensia-penye udhia penyeza rupia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom