ITV vs Rais Magufuli na CCM

ITV vs Rais Magufuli na CCM

Status
Not open for further replies.

RJ-White

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2014
Posts
744
Reaction score
752
Habari JFGT,

Nimefuatilia kwa ukaribu nimeona ITV wana-report habari za Mkuu wa nchi na majeshi yake Rais JPM katika hali isiyompa umuhimu au uzito. Hii tafsiri yake ni nini?

Mfano, siku Mh Rais amelihutubia bunge na kutoa hotuba "ya kihistoria" iliyojaa uzalendo na kufufua matumaini, hotuba iliyogusa mambo nyeti kabisa yanayoisumbua nchi hii kama dawa za kulevya, ufisadi na ukwepaji kodi, taarifa ya habari saa mbili jioni habari ile ilisomwa kama ya tano au sita karibu na mwisho wa habari za kitaifa.

Nilikuwa bar muda huo watu waligeukia TV wakiamini habari hiyo itakuwa mwanzo kama ilivyozoeleka kipindi cha JK ambapo habari zake mara nyingi zilipewa kipaumbele kutangazwa mwanzo lakini walisubiri mpaka wakarudi kula maji tu. Hii ni nini??

Pia, juzi makamu wa Rais Mama Samia alikutana na Wanawake ofisini kwake kwa tukio la kikazi, habari hiyo ilisomwa mwisho-mwisho.

Anyway, siku Mh Rais au Makam au PM wakiwa na habari better niangalia TBC. Nahisi kuna element za mihemko na husuda.
Ila inabaki kuwa "uchaguzi umeisha, Rais ni JPJM".

Wanaisoma number tu sasa watu wa level ya kina Bade na bado!

Salute Mheshimiwa Rais!
 
Mimi sijawahi angalia tv yoyote zaidi ya ITV na mambo yote anayoyafanya nayaona kupitia ITV

Pole sana wa kuangalia ITV t. Ni jambo la hatari mno. Ukitaka upate ufahamu mkubwa wa mambo mbalimbali ya dunia ni lazima uwe na tabia ya kuangalia channel nyingi. Ukitaka kuwa na afya njema haiwezekani uwe unakula maharage tu kila siku.
 
Nina wasi wasi kama uwa unaangalia habari au vipindi vingine vya itv, hivyo maelezo yako yanaonyesha kwamba uangalii itv ila unamihemuko mingine ya chuki tena sio na itv bali na mmiliki wake, mie naomba nikushauri, hebu tafuta njia nyingine za kuungwa mkono na watu wenye mitizamo kama yako na sio kuja kutafuta sababu zisizo na pumzi au uhai, chuki na roho mbaya hazifai muda huu, tumepata serikali mpya sasa tufanye kazi.

Pole ndugu mie na waungwana wenzangu hatuko na wewe, pia nasikitika watu nyie mmekuja kwa kasi sana humu jf ili tu muihujumu na watu waone haifai, acha chuki.
 
Ikiwa ya kwanza au ya mwisho tatizo ni nini? Hata kama ITV inamapungufu lakini ndio kituo bora kabisa hapa TZ.
 
wachaga wameweka kinyongo.... mirija inazibwa ... majipu yanapasuliwa ...
 
Mihemko+chuki+ujinga uliokithiri=mada za kipuuzi kama hizi
 
Mpuuzi na mnafki tu wewe. Huna chakuandika acha, sio lazima uandike.

Watu wanaleta hoja zakujenga taifa wewe unaleta mipasho huku.
 
Fungua tv yako na wewe ili tuone uhodari wako kwenye utendaji
 
Habari JFGT,

Nimefuatilia kwa ukaribu nimeona ITV wana-report habari za Mkuu wa nchi na majeshi yake Rais JPM katika hali isiyompa umuhimu au uzito. Hii tafsiri yake ni nini?

Mfano, siku Mh Rais amelihutubia bunge na kutoa hotuba "ya kihistoria" iliyojaa uzalendo na kufufua matumaini, hotuba iliyogusa mambo nyeti kabisa yanayoisumbua nchi hii kama dawa za kulevya, ufisadi na ukwepaji kodi, taarifa ya habari saa mbili jioni habari ile ilisomwa kama ya tano au sita karibu na mwisho wa habari za kitaifa.

Nilikuwa bar muda huo watu waligeukia TV wakiamini habari hiyo itakuwa mwanzo kama ilivyozoeleka kipindi cha JK ambapo habari zake mara nyingi zilipewa kipaumbele kutangazwa mwanzo lakini walisubiri mpaka wakarudi kula maji tu. Hii ni nini??

Pia, juzi makamu wa Rais Mama Samia alikutana na Wanawake ofisini kwake kwa tukio la kikazi, habari hiyo ilisomwa mwisho-mwisho.

Anyway, siku Mh Rais au Makam au PM wakiwa na habari better niangalia TBC. Nahisi kuna element za mihemko na husuda.
Ila inabaki kuwa "uchaguzi umeisha, Rais ni JPJM".

Wanaisoma number tu sasa watu wa level ya kina Bade na bado!

Salute Mheshimiwa Rais!

Chema siku zote kinajiuza,kama wanajifanya bado hawajaisoma number ni swala la muda tu,ni lazima wataisoma na waisema number.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom