ITV tunaomba kipindi cha kipimajoto kiahirishwe leo

ITV mmetuangusha sana leo. Mhavile kesho kaa na watu wako hii kitu isijirudie tena. Mmetia aibu sana
 
Kwani unadhani ni bahati mbaya Kafulila kuwa peke yake kwenye kipindi? Huo ni mkakati. ITV wanatumika tu.
Sasa wanamdanganya nani
Yani itafika sehemu wao kwa wao wataanza kulaumiana
Umeona mwenyekiti wa PAC wa bunge anavyo anza kishindwa kufunikafunika mambo
Itafika muda mawe yataongea hata kama watu wakinyamaza
 
Haileti maana ya kipindi cha leo kufanyika, tunaomba sana Kafulila hawezi kuzungumza peke yake kwa mantiki moja tu hatutawaelewa mkija kutuambia tahadhari ya kwamba mdahalo huu sio msimamo wa ITV......
..unadhani hao itv wamemualika kwa Bahati mbaya? hiyo tv kwa sasa ningumu kutofautisha Radio Uhuru na hiyo! Full ujinga!
 
ITV acheni kutumika Kafulila anajulikana msimamo wake kuhusu riport ya CAG,ili muwe fair Kwa nini msimualike Zito kabwe wapambane kwani Kafulila alijitokeza kuijibu hoja ya Zito.
Mzee Mengi ITV yako imeanza kuwa TBC,hizi siku za karibuni hasa baada ya vijana wako Godwin Gondwe na Emmauel kuteuliwa basi wengine wameanza kukutana faragha na akina polepole ili kupitisha agenda zao,ITV mjitathimini kama mnataka watanzania wailewe hiyo riport ya CAG mwiteni na Zito tupate mawazo kinzani
 
Back
Top Bottom