ITV na Star Tv, mnachemsha kuzuia matangazo Azam

ITV na Star Tv, mnachemsha kuzuia matangazo Azam

Mlima meru

Senior Member
Joined
Dec 30, 2012
Posts
114
Reaction score
20
Nipo kanda ya ziwa kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka...
Jana majira ya jioni nilimtembelea rafiki yangu ambaye amejipatia kingamuzi cha AZAM TV ambacho ki ukweki kinaonesha vizuri sana, kwa pande zile nafikiri ni kwa kuwa kina tumia setelaiti.

Alichosema huyo rafiki yangu ni kuwa channeli za ndani ya nchi anapata TBC ila zingine kama ITV, Channel ten and Star Tv hazionekani eTi wenyewe wamekatalia...

Nashindwa kuelewa hii technologia kama watu wanailewa vizuri; Mengi unalifaham hili? au chuki binafsi?

Ninavyojua ni kuwa TV inavyo kuwa na coverage kubwa (kwa kuonekana na watu wengi) ndio inapata faida kubwa kwa matangazo; sasa hawa jamaa nafikiri kwa mawazo yao ya hapa karibu wanafikiri watalazimisha watu kukunua vingamuzi vyao ili waone TV zao?? kitu ambacho sio kweli kabisa.....
Watu hawapotayari tena kupanda juu ya miti kufunga antena ambazo hata hivyo zinaonesha kwa kukata kata....

Sitaki kuwataja majina ila kuna kampuni moja ya vingamuzi ....uki ingia ofisini kwao (head office) wenyewe hawapati network ya kuonesha hata Tv yao halafu eti wanauza...... sasa ukinunua ukienda nacho kijijini utegemee nini?
Ongezeni kwanza minara (au hamieni kwenye setelaiti) ndio mtangaze coverage...kumbuka; mkipoteza imani ya wateja wenu kuwarudisha ni ngumu sana....

Ushauri wangu:

Hela ya Tv ipo kwenye matangazo...na matangazo ni couverage.....

Kazi kwenu.. labda kama ni chuki binafsi..ambayo haitawafikisha mbali....

Nawakilisha!!!!!
 
We ndo mzigo namba moja yy mpaka anamilik tv station ulidhan aliota ndoto tu akawa vile?yeye kukataa kujiunga anajua n kipi anakitaka yy u never know je kama azam ndo kagoma warusha?
 
Mwambie Bilionea Mzee Mengi hata DSTv afanye maelewano nao kama Ch. 10 walivyofanya ili ITV na Ch. 5 zirushwe kwenye DSTv
 
tunakoelekea si ajabu hata Ku-post (kuandika hoja) hapa JF ukatakiwa kulipia
 
Nilikuwa nasoma kwenye mtandao wa Azam hapa wameandika kuwa hao kina ITV na STA TV ndio wamekataa kuunganisha...eti kwa kuwa AZAM wanarusha kwenye setelaiti na kuwa na international coverage....
Nafikiri Inaweza kuwa .... Chuki binafsi na kuoneshana ubabe ila kumbuka hawamkomoi Azam ila wanawakwaza wa TZ..kwa kuwaona hao wenye TV sio waungwana...
Bahresa anaendelea kula goodtime...you never know Azam akaunganishia ligi ya ulaya at no time...na kuifanya iwe chaguo la wote na hasa vijana

haihitaji kupigiwa magoti ili kuruhusu Tv yako irushwe...kama hawataki basi!!!
 
Nipo kanda ya ziwa kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka...
Jana majira ya jioni nilimtembelea rafiki yangu ambaye amejipatia kingamuzi cha AZAM TV ambacho ki ukweki kinaonesha vizuri sana, kwa pande zile nafikiri ni kwa kuwa kina tumia setelaiti.

Alichosema huyo rafiki yangu ni kuwa channeli za ndani ya nchi anapata TBC ila zingine kama ITV, Channel ten and Star Tv hazionekani eTi wenyewe wamekatalia...

Nashindwa kuelewa hii technologia kama watu wanailewa vizuri; Mengi unalifaham hili? au chuki binafsi?

Ninavyojua ni kuwa TV inavyo kuwa na coverage kubwa (kwa kuonekana na watu wengi) ndio inapata faida kubwa kwa matangazo; sasa hawa jamaa nafikiri kwa mawazo yao ya hapa karibu wanafikiri watalazimisha watu kukunua vingamuzi vyao ili waone TV zao?? kitu ambacho sio kweli kabisa.....
Watu hawapotayari tena kupanda juu ya miti kufunga antena ambazo hata hivyo zinaonesha kwa kukata kata....

Sitaki kuwataja majina ila kuna kampuni moja ya vingamuzi ....uki ingia ofisini kwao (head office) wenyewe hawapati network ya kuonesha hata Tv yao halafu eti wanauza...... sasa ukinunua ukienda nacho kijijini utegemee nini?
Ongezeni kwanza minara (au hamieni kwenye setelaiti) ndio mtangaze coverage...kumbuka; mkipoteza imani ya wateja wenu kuwarudisha ni ngumu sana....

ushauri wangu...
hela ya Tv ipo kwenye matangazo...na matangazo ni couverage.....

kazi kwenu...labda kama ni chuki binafsi..ambayo haitawafikisha mbali....

Nawakilisha!!!!!

Hold on.....,

Azam Tv ana Broadcasting Channel tu (kama Channel Ten), ni Muuza decorder tu (Kama Startimes) au Both (Kama ITV + Digitek au Start Tv + Continental)??

Kama ana Decorder zake na Channel Yake, je yeye Channel yake inapatikana kwenye Decorder za wenzake? Why?

Manake tusitake tu ITV ionekane kwenye Decorder za Azam, wakati yeye Azam TV haipo kwenye decorder za Digitek inayomilikiwa na ITV.
 
hawa ni wafuata mkumbo hawajui nini kinaendelea...leo huyu mtoa mada anamshauri MENGI 'eti matangazo ya tv ni coverage' really???do u think hawajui wanachofanya???
 
Nipo kanda ya ziwa kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka...
Jana majira ya jioni nilimtembelea rafiki yangu ambaye amejipatia kingamuzi cha AZAM TV ambacho ki ukweki kinaonesha vizuri sana, kwa pande zile nafikiri ni kwa kuwa kina tumia setelaiti.

Alichosema huyo rafiki yangu ni kuwa channeli za ndani ya nchi anapata TBC ila zingine kama ITV, Channel ten and Star Tv hazionekani eTi wenyewe wamekatalia...

Nashindwa kuelewa hii technologia kama watu wanailewa vizuri; Mengi unalifaham hili? au chuki binafsi?

Ninavyojua ni kuwa TV inavyo kuwa na coverage kubwa (kwa kuonekana na watu wengi) ndio inapata faida kubwa kwa matangazo; sasa hawa jamaa nafikiri kwa mawazo yao ya hapa karibu wanafikiri watalazimisha watu kukunua vingamuzi vyao ili waone TV zao?? kitu ambacho sio kweli kabisa.....
Watu hawapotayari tena kupanda juu ya miti kufunga antena ambazo hata hivyo zinaonesha kwa kukata kata....

Sitaki kuwataja majina ila kuna kampuni moja ya vingamuzi ....uki ingia ofisini kwao (head office) wenyewe hawapati network ya kuonesha hata Tv yao halafu eti wanauza...... sasa ukinunua ukienda nacho kijijini utegemee nini?
Ongezeni kwanza minara (au hamieni kwenye setelaiti) ndio mtangaze coverage...kumbuka; mkipoteza imani ya wateja wenu kuwarudisha ni ngumu sana....

ushauri wangu...
hela ya Tv ipo kwenye matangazo...na matangazo ni couverage.....

kazi kwenu...labda kama ni chuki binafsi..ambayo haitawafikisha mbali....

Nawakilisha!!!!!

wewe unaem-question MENGI ni nani na umefanya nini kama Mengi na IPP MEDIA YAKE???and for how long??? ulikuwa wapi wakati Mengi anaanzisha ippmedia???
 
TCRA nao MIZIGO!
Binafsi sioni sababu ya kuendelea kuwa na kitengo cha TCRA, ni woga sana - wanaogopa sana wafanya biashara - wawe wa makampuni ya simu au hawa wa makampuni ya TV na Radio, sheria ya mawasiliano inasema wazi wazi kwamba local channels zote zionyeshwe na makampuni yote nchini bila ya kujali kama ni ITV, EATV, clouds, Shibuka, DTV, Channel Ten, TBC1, TBC2, CTN, Mlimani na Tumaini.

Suala hilo alipashwi kuwa na mjadala - cha ajabu baadhi ya makampuni hayo yanavunja sheria bila ya kuchukuliwa hatua yoyote - wanafanya wapendalo as if they own this country. Ukosefu wa ubunifu wa baadhi ya makampuni haya ndio kunawafanya wawe selfish kupindukia, hawapendi ushirikiano hata kidogo, wanapoteza fedha nyingi kuweka mitambo ya kusambaza mawimbi kupitia usawa wa aridhini, mfumo huo una technical challenges chungu mzima kuhanzia kuweka repeaters karibu kila Mkoa si hilo tu sehemu nyingine unapashwa kuongezea gap fillers wakati mwingine juhudi zote hiyo uwezi kuwa na uhakika kama picha hazitaganda ganda ovyo ovyo!

Wanachosahau ni kwamba mawimbi ya digitali yako highly directional unlike analouge signal. Sina shaka tatizo hili mwenzao AZAM alifanya homework ya kutosha na kuja na mbinu za kumaliza matatizo niliyo taja hapo juu, AZAM hana haja ya kupoteza pesa za kununua mitambo ya kusambaza mawimbi kila mkoa - channels zake zinaoneka kwenye makontinent yanayo kuwa covered na footprint ya satellite anayo tumia, channels za AZAM zinaonekana bila matatizo - uwe Mlimani, baharini au porini mradi upunguze matawi ya miti, tatizo la Ku Band ni mvua ikinyesha kwa wingi hutapata matangazo.

All in all nampongeza sana AZAM kwa kutumia akili na kuwazidi wenzake kete, wenzake ambao kazi yao ni kulalama kila kukicha, sina shaka when the going gets tough na wao watamuhiga Mzalendo Mzee Bhakresa, hawana jinsi - wa kwanza kumuhiga AZAM watakuwa StarTimes sijui kwa nini hawakulifiria kutumia DVBS toka mwanzo!
 
Du kazi kweli kweli,naona jazba zimeanza kupanda kwa baadhi ya watu.
Ila naweza kusema kwamba AZAM tv wanalengo zuri sana.
Na ndio maana nimewahi kusema kwamba ndio Decorder peke yake East Africa mabazo zimeweza kufikia mikoa mingi kiasi hiki kwa wakati mmoja na Coverage ya hali ya juu namna hii.

Na inapotokea kwamba kuna biashara inayofanana basi matatizo kama haya hutokea.

Ila nasikitika tu hakuna mtu anaetaka ku challenge nao kwa Kujenga uwanja wa mpira na kumiliki timu au kuwa na academy ya kisasa.Hapo ndio ningeona kweli watu wameamua

Lakini hili la kuingiza baahdi ya Tv kwa maslahi ya kila mtu sidhani kama inasaidia.
Kwanza ningependa mfahamu kwamba hizi decorder ni kama line za simu,miaka ya 2001 ilikuwa line ya sime mpaka 20,000,lakini sasa ni bure,kwa mategemeo kwamba ukiisha nunua line unakuwa ni customer wa kampuni ya simu na wao watapata faidi kutoka kwako.

Sasa tunakoelekea kwenye Decorder ni kwamba itakuwa the same,zinatolewa buree,na makampuni yatatngeneza faida kwenye malipo ya mwezi.
Maana mpaka sasa kuna Decorder used za Nje ya nchi huku Zanzibar zinashika channel zote na wengine watundu wanavyonza mpaka supersports.

Muhim ni kukubaliana tu wao kwa wao.

Kwanza kuna habari za chini ya Carpet kwamba AZAM decorder zilitakiwa kuwa chini ya bei hiyo ila Mamlaka ya ushindani wa Bishara ikaingilia kati,maana kuna watu decorder zao zinge doda zaidi ya zilivyododa kwa sasa.
Hii Biashara sasa hivi ni kama fitna vile,na waofanyafitna wanafanyanamtu ambae hajui kama kuna fitan.

Mie naungana na jamaa hapo juu kwamba AZAM tv ndio mkombozi wa Upatikanaji wa Habari kwa Karne hii.
Kuna mikoa kama ya Kigoma,walikuwa wanashika TBC peke yake.We nchi gani mkoa mzima unashika TBC peke yake.
Sio kila mtu anaowezo wa Satelite dish.
Ila kwa sasa AZAM TV anafanya watu waikamate Dunia kwa mkupuo.Full raha.
Wao miaka yote wamekalia mikoa yenye maslahi nao tuu,halafu eti sasa ndio waanze kuleta maneno ya uzalendo.Uzalendo kwa vitendo.

Kwanza mie nwapongeza pia kwa kuwka mambo yao kimya kimya,maana wengine matangazo teleee,ila yeye alivojenga uwanja watu waliona,simba na yanga wao kila siku wanchukua wachina na wagirkiki wa karikakoo eti wanaita waandishi wa habari wapime uwanja,we nani anamjua mkandarasi wa Azam Complex ni nani kwa ghafla,ila muulize mtu wakandarasi wa uwanja wa Simba na yanga atakutajia hadi nchi walizotoka,uwanja je upo wapi?
Haya Azam Decorder,upembuzi yakinifu ulifanya kimya kimya bila porjo za waandishi wa habari leo hii Azam Decorder ndio Habari ya Mjini.

Halafu niegundu kitu kimoja,ukimchukia Bakhers na product zake basi ahifiki mwaka anakuja na jipya.
Sasa na shauri mudnelee kuchuku hii product ya azam decorder muone mwakani anavyowanyoa zaidi.
Azam weka Ligi ya Uingereza turejeshe madishi ya watu.tehetehe tehe

Jamani ni Mtizamo wangu tu,ila Mtakubali Azam Decorder hata kimya kimya
 
Tatizo La ITV na Star TV ni kubwa, Ubabe wao hauishi kwa AZAM TV pekee, Ila pia wamekatalia channel zao kwa Easy TV, DSTV, ZUKU.
Lakini baada ya Muda watangazaji wa bidhaa watapokea data na ndio wataanza kuumia kutokana na kuwa na coverage ndogo kwa vingamuzi.
Kama sio TCRA pia walikuwa na mpango wa kujitoa Startimes.

Msijali Local chaannel mpya - VIASAT 1- itawapiga bao woote
 
Binafsi sioni sababu ya kuendelea kuwa na kitengo cha TCRA, ni woga sana - wanaogopa sana wafanya biashara - wawe wa makampuni ya simu au hawa wa makampuni ya TV na Radio, sheria ya mawasiliano inasema wazi wazi kwamba local channels zote zionyeshwe na makampuni yote nchini bila ya kujali kama ni ITV, EATV, clouds, Shibuka, DTV, Channel Ten, TBC1, TBC2, CTN, Mlimani na Tumaini. Suala hilo alipashwi kuwa na mjadala - cha ajabu baadhi ya makampuni hayo yanavunja sheria bila ya kuchukuliwa hatua yoyote - wanafanya wapendalo as if they own this country. Ukosefu wa ubunifu wa baadhi ya makampuni haya ndio kunawafanya wawe selfish kupindukia, hawapendi ushirikiano hata kidogo, wanapoteza fedha nyingi kuweka mitambo ya kusambaza mawimbi kupitia usawa wa aridhini, mfumo huo una technical challenges chungu mzima kuhanzia kuweka repeaters karibu kila Mkoa si hilo tu sehemu nyingine unapashwa kuongezea gap fillers wakati mwingine juhudi zote hiyo uwezi kuwa na uhakika kama picha hazitaganda ganda ovyo ovyo! Wanacho sahau ni kwamba mawimbi ya digitali yako highly directional unlike analouge signal. Sina shaka tatizo hili mwenzao AZAM alifanya homework ya kutosha na kuja na mbinu za kumaliza matatizo niliyo taja hapo juu, AZAM hana haja ya kupoteza pesa za kununua mitambo ya kusambaza mawimbi kila mkoa - channels zake zinaoneka kwenye makontinent yanayo kuwa covered na footprint ya satellite anayo tumia, channels za AZAM zinaonekana bila matatizo - uwe Mlimani, baharini au porini mradi upunguze matawi ya miti, tatizo la Ku Band ni mvua ikinyesha kwa wingi hutapata matangazo. All in all nampongeza sana AZAM kwa kutumia akili na kuwazidi wenzake kete, wenzake ambao kazi yao ni kulalama kila kukicha, sina shaka when the going gets tough na wao watamuhiga Mzalendo Mzee Bhakresa, hawana jinsi - wa kwanza kumuhiga AZAM watakuwa StarTimes sijui kwa nini hawakulifiria kutumia DVBS toka mwanzo!

Startimes wanakuja na product mpya ya satellite- under umberella ya StarSat, mwezi Huu february
 
Nilifikiri Wingi wa makampuni ya ving'amuzi ungeondoa ukiritimmba na kuleta ushindani, kumbe wapi!!
Lakini muda si mrefu mambo yatakuwa sawa tu, na watazamaji tutafaidi sana.
 
Startimes wanakuja na product mpya ya satellite- under umberella ya StarSat, mwezi Huu february

Mkuu mimi nilikuwa nawashangaa sana hawa Wachina wa StarTimes sikuona mantiki ya kugangania kwenye terrestrial transmission ambayo ina matatizo ya kila chungu nzima na ni gharama kusambaza nchi nzima. Tatizo lao lilikuwa linatokana na TBC nadhani kug'ang'aniza mafundi wao au mainjinia wao kushirikishwa kwenye mradi huu wa Wachina - walijikuta wanaingia kwenye gharama zisizo za lazima kutokana na kukosa kuona mbali/ubunifu sasa sijui nani atawajibika kwa kuleta hasara zisizo na msingi - si ajabu Serikali yetu ika-foot blunder hii. Tangu mwanzo baada ya kuona wanatujulisha mradi unavyo kwenda na kuona wananchi wanavyo lalamika kuhusu upatikanaji wa matangazo nilijua mpaka waje kusambaza gap-fillers karibu nchi nzima kwenye matatatizo ya kupatikana mataganzo kirahisi hii ingechukuwa miaka!!! Nikawa najiuliza kwa nini hawatumii Satellite lakini? Walikuwa ill advised tangu mwanzo ukiwekea maanani kwamba uwezo wa waswahili wenzetu na vile vile ubunifu ni mdogo sana, siwasemi vibaya lakini hilo nilisha liona tangu mwanzo, sasa hivi ndio naona wanashtuka baada ya kuona mafanikio ya AZAM TV, mimi niliwahi kuwapa ushauri kupitia JF siku nyingi tu kuhusu changa moto za usambazaji watangazo kupitia njia ya terestila lakini wakapuuzia - ndio tulivyo.
 
TCRA pia walitaka makampuni DVB-T2 kwa ajili ya unafuu wa vifaa na wakati mwingine huhitaji Antenna.
Kingamuzi change satellite cha Startimes, unfortunately hakutakuwa na channel za ITV na StarTV
 
Q: Existing TV stations did not want to join and be part of Azam TV can you expand on the reasons why?

A: They are Star TV and Independent Television (ITV). We have spoken to both of them, but at the end of the day it is their decision. My door is always open if they want to talk.
It does look strange when every FTA TV in Kenya wants to be on our platform, but in Tanzania ITV and Star TV do not want to be.
There are TCRA rules stating that if you are a DTT operator there are five must carry channels which include Star TV and ITV. However since we are a satellite operator these rules do not apply. So they are not obligated to be on our platform
I would love it, if they joined us because it makes no sense that if a customer wants to watch their services and Azam TV they have to get a separate system.
We should not be competitors because if they come on to our platform more people will be watching their services and they will be earning more money.
I assume it is a commercial decision on their part they believe they would do better as our competitors. It is a competitive industry but not so competitive that we cannot work together.
 
kweli nimeamini azam wapo vzur ila naskia walitaka kuuza dishi lao kwa elfu 30 tu lakin wakashinikizwa wauze ghali
naomber pia washushe garama ya madishi ndugu
 
Nilikuwa nasoma kwenye mtandao wa Azam hapa wameandika kuwa hao kina ITV na STA TV ndio wamekataa kuunganisha...eti kwa kuwa AZAM wanarusha kwenye setelaiti na kuwa na international coverage....
Nafikiri Inaweza kuwa .... Chuki binafsi na kuoneshana ubabe ila kumbuka hawamkomoi Azam ila wanawakwaza wa TZ..kwa kuwaona hao wenye TV sio waungwana...
Bahresa anaendelea kula goodtime...you never know Azam akaunganishia ligi ya ulaya at no time...na kuifanya iwe chaguo la wote na hasa vijana

haihitaji kupigiwa magoti ili kuruhusu Tv yako irushwe...kama hawataki basi!!!

Mkuu upo sahihi kabisa, naweza nikasema hizo ni chuki dhahiri! huyu mshikaji katufanyia mambo makubwa mno especially kwa sisi wapenda news na soka live yatupasa tumpe sapoti nyingi kutoka kwetu,, so anahitaji pongezi kubwa mno kutoka kwetu. and another thing is that kwakuwa labda yeye ni mwalabu ndiomaana hapati sapoti za kutosha? na kumtakia mazuri? I don' know why, sisi watz ndivyo tulivyo na roho zetu za korosho...mimi ni mpenzi sana wa soka, hivyo nimefarijika sana bwana Azam kutuletea sports live big up kwake..na nitaendelea kuangalia azam na kuachana na akina ITV
 
Back
Top Bottom