ITV mmewakosea sana watanzania

Muongo wewe mbona kwenye gazeti la nipashe IPO..nunua gazeti usome kuonyesha speech za lema kwenye TV inahitaji editing za kutosha ili kituo kisiingie kwenye matatizo
Yan unanze kununua magazeti tena?
 
Lema kapwaya sana
Haikuwa na umuhimu na ulazima kwa ITV kuonyesha
 
Tujamaa twa ukawa bana! kwahiyo kwa kuwa nyie mnamwaminia huyo Lema wenu basi mkadhani kila mtanzania atamwona wa maana?
 
Wanamuogopa sizonje, kadikteta ketu
Hawa ujasiri wao uliishia pale mzee Warioba alipotandikwa makofi na Daud tangu hapo hawana ujasiri tena
 


Waache watajizika wenyewe! Wenzao TBC wanaishi kwa Kodi zetu. Wao wanahitaji wadau kujiendesha.
 
Sasa ni wakati wa sisi tunaotakia mema nchi hii kuanza kususia media kama hizi na makampuni mengine yanayotumika kisiasa .
 
ITV Siku Hizi wala siitazami kabisa Taharifa ya Habari Zake.

Siku hizi Naangalia Star Tv Habari. Napata habari zote, hawa jamaa siku hizi wamejirekebisha sana.

Hata habari ya mkutano wa jana wa Mh Leo wameonyesha Habari hiyo.

Amieni habari ya Star Tv unapata habari zote waacheni ITV.
 
Nadhani muhimu ni chama kuanzisha vyombo vya habari vyake, redio, tv na magazeti
kma gazeti lenye fikta mbadala kma mawio lafungiwa au lisu akiongea tu anaitwa mchochezi sembuse tv ianzishwe si itafungiwa baada ya siku moja tu
 

Kwa maoni yangu kituo ambacho kinarusha "balanced news" ni Azam TV peke yake...!
 
Damu nzito kuliko maji. Habari za vita dhidi ya madawa ya kulevya hazikuwa zikipewa muda wa hewani na ITV, lakini leo tunaambiwa kuwa Lema ni muhimu zaidi ya vita yenye lengo la kuokoa afya za maelfu ya vijana wa kitanzania.
 
Habari za mambo ya jela zinasaidia nini kwani mkuu?
 
Ukweli unaujua kuwa habari ya Lema, Mbunge na Waziri Kivuli, ilikuwa na maslahi kwa Waliomchagua na kwa Nchi hasa kwa nafasi yake kama kiongozi. Ila kwa sababu za kisiasa basi wajitoa ufahamu.
Walio mchagua walikua nae
Unataka iwe ya kitaifa kwani tulichagua wote. Acha ushambenga wewe
 
ITV IMETEKWA NA CCM MAANA JANA WAMETUONESHA UPUUZI WA CHIMWAGA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…