ITV-Juma Kapalatu Hafai kipindi cha Malumbano Ya Hoja

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
15,303
23,055
Wakuu!!

Kwa muda mrefu hiki kipindi kinapoteza hadhi yake. Msimamizi wa kipindi hikiJuma Kapalatu ambaye kwa muda mrefu amekuwa akikandamiza hoja ya mtu ambaye anaikosoa serikali.

Kapalatu hataki kabisa kusikia mtu ukiikosoa serikali, anataka kusikia kile anachoona yeye kinafaa ndio ukiseme.

Leo kuna hoja ya nini matarajio ya serikali ya awamu ya tano mwaka 2016.

Siku zote unapochangia mada, lazima uanze na utangulizi ambao utampa msikilizaji uelewa na usikilizaji mzuri.

Inasikitisha sana Kapalatu kukandamiza hoja ya mtu hasa pale anapoikosoa serikali kwa aliyofanyika huko nyuma au kipindi hiki.

Ukishaikandamiza hoja ya mtu ambayo watazamaji wanaona yupo sahihi, lkn mtangazaji ukaikosoa kwa namna unavyotaka wewe, basi hoja ya mchangiaji inakuwa haina nguvu, inakosa mashiko.

Tunaomba mkurugenzi wa ITV ambadilishe mtangazaji huyu, hafai kuongoza kipindi.

Alamsiki
 
Hiki kipindi kimepoteza mvuto, afadhari ya Kambaya kuliko Kapalatu au Ufo Salo.

Nyangasa na Magret Cosmas walikiweza hiki kipindi.
 
wamekusikia mlianza na mfo saro kabadilishwa sasa tena mnataka na huyu achomoke
 
Bora kama wanaogopa Serikali waache kuja na mada kama Hizo waandae mada za kuifagilia Serikali tu maana huyo Bonge hawezi kitu ni bora wengine wote kuliko huyo bonge anayefanana na Le- Mutuz, Ujue unene ukizidi Mafuta hupanda kwenye Ubongo na kupunguza uwezo wa kufikiri ndiyo maana wazungu wanaupiga vita sana Unene wanasisitiza watu wafanye mazoezi wapunguze mafuta mwilini.
 
Bor
wamekusikia mlianza na mfo saro kabadilishwa sasa tena mnataka na huyu achomoke[/QUOTE bora ufa Saro japo ni mtemi sana lakini yeye mada za kukosoana anazipenda sana na hawezi kumzuia mtu anayekosoa kwa uchungu.
 
Mkiropoka mtadhibitiwa tuu! Hivi mnafikiri msizuiwa kuropoka madhara yatakuwa kwa nani kama si ITV? Ukiongea point bila kuvuka mipaka hutowezwa kuzuiwa!

Tatizo mnakwenda pale kuwashambulia watu sasa mnataka muachwe halafu wenzenu wafungiwe ili mpate mtaji wa kisiasa kuwa serikali inaonea vyombo vya habari?

Nawapongeza ITV kwa kuweka waongozaji wanao wadhibiti waropokaji!

Kama unataka kuropoka jifungie bafuni ufanye hivyo si kwenye media za watu...!

Hongera Kapalatu na Ufo saro.
 
Back
Top Bottom