GE2025 Itutu: Mafisadi jiandaeni kukimbia nchi tukiingia madarakani

GE2025 Itutu: Mafisadi jiandaeni kukimbia nchi tukiingia madarakani

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Just Pray

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,142
Reaction score
4,779
Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) kimesisitiza kuwa endapo kitapata ridhaa ya kuingia madarakani, kipaumbele chake kitakuwa kuwawajibisha wote walioiba mali za umma.

Kauli hiyo imetolewa Oktoba 3, 2024 katika Wilaya ya Ilemela, wakati wa mwendelezo wa kampeni za mtaa kwa mtaa zinazofanywa na Mwenyekiti wa ADC Taifa, Shabani Itutu ambaye pia ni mgombea ubonge wa Ilemela mkoani Mwanza.

Itutu, ameeleza kuwa tatizo la ufisadi ndilo limekuwa chanzo kikuu cha changamoto nyingi zinazowakabili wananchi ikiwemo upungufu wa madawa hospitalini.

Kwa mujibu wa maelezo yake, zaidi ya Sh30 trilioni zimepotea kutokana na matumizi mabaya na ubadhirifu ulioainishwa kwenye ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) tangu mwaka 2021.

Hata hivyo, licha ya wahusika kutajwa hadharani, Itutu amedai hakuna hatua za kisheria zilizochukuliwa dhidi yao.

 
Maigizo ni mengi sana, subirini tuandamane
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom