Itifaki kwenye hotuba za Ramaphosa na Magufuli Ikulu Tanzania

Rais Magufuli sio mzungumzaji iwe kwa kiingereza au kiswahili. Wapo watu wapo hivyo tena mie nikimsikiliza akiwa anaongea pasipo kusoma naona ndiyo anafanya vizuri.

Akiwa anasoma anapooza saana.

Mwisho wa siku uongozi sio kuzungumza tu yapo mambo lukuki.
 
Nimesikiliza hotuba za viongozi hao nikaona aibu kidogo kwani badala ya rais mwenyeji kuanza hotuba yake na kuishia kwa kumkaribisha mgeni wake, nimeona kuwa mgeni ndiye aliambiwa atoe hotuba kwanza halafu mwenyeji amalize. Sijui hiyo ni protocol ya namna gani.

kwa vile Ramaphosa aliongea kiingereza, siyo kizulu, ilikuwa ni vyema Magufuli naye afanye ku-reciprocate kwa kuongea kiingereza pia, siyo kiswahili.
Tunaomba kujua Ilimu yako tafadhali
 
Uongo huo. Afrika ya Kusini ina lugha za Taifa 11, mojawapo ni Kizulu. Usilete propaganda usizojua, zungumza ukiwa na facts.
Hivi mkuu Kichuguu hakuna tofauti kati ya lugha ya taifa na lugha rasmi!

Nauliza maana navyojua/navyoskia hizo lugha tajwa ni lugha rasmi.

Official language/national language. Nadhani kwetu kiswahili ni lugha ya taifa/national language.

Asante.
 
Alikuwa mwl wa sec alikuwa anafubdisha jwa kiingereza. Akaenda chuo kikuu akapata Mastaz kisha Phd Kwa kiingereza hicho hicho. Yuko vizuli!
Mkuu acheni kufanya matani yasiyokuwa na huruma...
Yaani ulitegemea kabisa huyo mwenyeji aongee hicho ulichokiita Kiingereza?
Anaanzia wapi kwa mfano..??
 
Ingekuwa lafudhi tu mbona hapo hakuna tatizo. Huwa anakosea mpaka grammar. Ni vyema atumie tu kiswahili. Maana akikosea watu tutasahau hata SADC na kuanza kujadili hayo makosa. Ukweli sisi watanzania hatupo vizuri kwenye english pamoja na wengine kuwa wasomi wa anga za juu. Wala sishangai. Mtu unakulia kisukuma,shule kiswahili,secondary kiinglish darasani tu ila nje kiswahili.Chuo kikuu napo kiinglish ni mwalimu akiwa anafundisha tu. Nje ya hapo Kiswahili kwa kwenda mbele.

Victoire,
Ulishasikia Kiinglish cha Wana Afrika Kusini,Wanaigeria, Waarabu au Wahindi?
Tonations au lafudhi ya lugha ya mamako huwa haipotei lazima itasikika tu...!!Hata nshomile wa Kihaya akianza kubonga Kiinglish hapa utasikia lafudhi ya..''yiwe....yanishwera..'' kwa mbaali!!

Magufuli siyo kwamba anaogopa kuongea Kiinglish chenye lafudhi ya Kisukuma baali hana hata hicho chenye lafudhi ya Kisukuma...!!. Mbona tulikuwa na kina Balozi Paulo Bomani alikaa Marekani miaka lukuki lakini alikuwa anagonga English yenye lafudhi ya Kisukuma kwa English ilinyooka?
 
Hivi mkuu Kichuguu hakuna tofauti kati ya lugha ya taifa na lugha rasmi!

Nauliza maana navyojua/navyoskia hizo lugha tajwa ni lugha rasmi.

Official language/national language. Nadhani kwetu kiswahili ni lugha ya taifa/national language.

Asante.

Hiyo post umeikopi wakati bado naifanyia editing; uwongo ni dai kali sana, nilitakaka kusema kuwa post ile haikuwa kweli.

Kuhusu lugha za Africa ya kusini, Ramaphosa mwenyewe katika hotuba yake amesema atamfundisha lugha hizo akienda Afrika ya Kusini. Kule wana Federal system, kwa hiyo kila state ina uhuru wa kutumia lugha mojawapo kati ya hizo kumi na moja na zote zinatambulika kisheria.
 
Hiyo post umeikopi wakati bado naifanyia editing; uwongo ni dai kali sana, nilitakaka kusema kuwa post ile haikuwa kweli.

Kuhsu lugha za Africa yakusini, ramaphosa mwenyewe katika hotuba yake amesema atamfundisha lugha hizo akienda Afrika ya Kusini. Kule wa federal system, kwa hiyo kila state ina uhuru wa kutumia lugha mojawapo kaoi ya hizo kumi na moja na zote zinatambulika kisheria.
 
Victoire,
Ulishasikia Kiinglish cha Wana Afrika Kusini,Wanaigeria, Waarabu au Wahindi?
Tonations au lafudhi ya lugha ya mamako huwa haipotei lazima itasikika tu...!!Hata nshomile wa Kihaya akianza kubonga Kiinglish hapa utasikia lafudhi ya..''yiwe....yanishwera..'' kwa mbaali!!

Magufuli siyo kwamba anaogopa kuongea Kiinglish chenye lafudhi ya Kisukuma baali hana hata hicho chenye lafudhi ya Kisukuma...!!. Mbona tulikuwa na kina Balozi Paulo Bomani alikaa Marekani miaka lukuki lakini alikuwa anagonga English yenye lafudhi ya Kisukuma kwa English ilinyooka?
Mnigeria akiongea kiingereza unajua kabisa ni Mnija. Kidogo wakenya wengi hawana lafudhi. Akiongea kiingereza chake ni kama malkia Mwenyewe anaongea. Ila hapa Tanzania wengi kingereza kina lafudhi ya makabila yetu.
Magufuli Kinge cha kuongea ni mtihani. Ila ni asilimia kubwa ya watanzania.
 
Alikuwa mwl wa sec alikuwa anafubdisha jwa kiingereza. Akaenda chuo kikuu akapata Mastaz kisha Phd Kwa kiingereza hicho hicho. Yuko vizuli!

Tulimumu,
Acha kutetea ujinga wa homeboy wako!
Hivi umeshawahi kuingia darasani wakati wa somo la Sayansi au Hisabati ukamsikiliza Mwalimu? Unless uniambie hujawahi kuingia darasani. Waalimu wa Kibongo akifundisha darasani hata kama ni somo la Kiingereza ataongea Kiswahili 80%. Seuze somo la Sayansi kama Kemia, Bailojia au Fizikia? Hivi unajua kwamba Makampuni na Taaisisi nyingi za Kigeni huwa zina ajiri Wakenya na Waganda kwa sababu ya lugha ya Kiingereza? Leo hii kuna mapoyoyo fulani wanataka Mitaala yote kuanzia msingi mpaka Chuo Kikuu ifundishwe kwa Kiswahili...!!!Kwa jicho la 3, the reason behind ni lugha ya Malkia inawapiga..!!Tuache kutetea upuuzi jamani. Baba wa Taifa alisema:''WATANZANIA TUJIFUNZE KIINGEREZA MAANA NDO KISWAHILI CHA DUNIA''
 
Huu utawala kuna watu wameamua kujitoa ufahamu kwa kutetea kila namna ya upuuzi unaofanywa na Utawala wa Magufuli.
Kila jambo hata kama linaonekana limekosewa kabisa iwe KIITIFAKI au KISHERIA watu wanaona sawa tu...!!!Hiki nimekuwa ni kipimo kizuri sana cha kujua ujuha, ujinga, uzezeta na uelewa wa mambo kwa Wabongo wengi. Watu wanatakiwa waamke na wabadilike..!!!
Umeongea vizuri aisee ila sasa sidhani kama amekuelewa..
 
πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘πŸ½πŸ‘ŠπŸ½πŸ‘ŠπŸ½πŸ‘ŠπŸ½πŸ‘ŠπŸ½Pale mtu anataka kuhalalisha jambo kwa kutoa mfano FAKE wa USA bila kujua wewe unaishi huko kwa robo karne sasa.😎😎😎
πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚ πŸ˜‚
 
Subiri mataga ndio wanavaa mashati yao wanakuja kukuita mhujumu uchumi.

Watakubagaza mpaka ujute.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Jamaa anatupa mawe kwenye mzinga wa nyuki! Ngoja waje Sasa!πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Nimesikiliza hotuba za viongozi hao nikaona aibu kidogo kwani badala ya rais mwenyeji kuanza hotuba yake na kuishia kwa kumkaribisha mgeni wake, nimeona kuwa mgeni ndiye aliambiwa atoe hotuba kwanza halafu mwenyeji amalize. Sijui hiyo ni protocol ya namna gani.

kwa vile Ramaphosa aliongea kiingereza, siyo kizulu, ilikuwa ni vyema Magufuli naye afanye ku-reciprocate kwa kuongea kiingereza pia, siyo kiswahili.
Kutafuta Itifaki Ikulu ya Magufuli ni sawa na kutafuta sheria Mafia Mob.

Magufuli anajua kila kitu, anajua mpaka boiling point ya Silver kutoka kichwani mwake, habari za itifaki anaweza kutunga zake hapo hapo zikawa ndizo zinazokubalika!
 
Back
Top Bottom