Itapendeza sana Simba SC ikifuzu kucheza FIFA Club World Cup 2025

Hapa yabidi tushinde mechi 12 au tuchukue kombe
Tukienda kimahesabu tu, Simba inaweza kufuzu bila kuchukua kombe ila kama mambo 4 yatatimia:
1. Bingwa msimu huu awe Al Ahly au Mamelodi
2. Esperance apoteze mechi mbili zilizobaki za makundi na atolewe katika mashindano ya klabu bingwa
3. CRB na Petro de Luanda hata wakiendelea kuongeza point zao, wasije kufikia za Esperance
4. Simba ashinde mechi 2 zilizobaki za Makundi halafu ashinde mechi zote mbili za robo fainali, halafu ashinde zote mbili za nusu fainali na aingie fainali. Akiwa katika fainali, Simba haihaji kushinda mechi hata moja ingawa akitoka sare hata mechi moja itakuwa nzuri zaidi

Haya mambo yote manne yakitimia, Simba atafikisha point 75 sawa na Esperance. Sijajua FIFA watatumia kigezo gani iwapo hali hii itatokea ya timu mbili kulingana point katika rank.

Ingawa kama nilivyosema, tayari kuna timu mbili za kaskazini zilizofuzu, Simba inabidi ajisogeze angalau nafasi ya 5 chini ya Esperance, ili kama vigezo vingine vitatumika kama vya ukanda Simba iwe chaguo linalofuata. Hatujui vigezo vyoote.
 
Kama unajua ni sahihi kwanini ulisema kuwa Yanga haina vigezo vya kucheza FIFA club world cup? Timu zote 16 zilizofuzu katika hatua ya makundi zina nafasi ya kufuzu kasooro Wydad na Al Ahly pekee ambao wameshafuzu kwasababu ya kuwa bingwa wa misimu iliyopita. Kuna nafas moja ya bingwa mpya na kuna nafasi moja pekee ya upande wa rank.
Yanga wameshafuzu hata hiyo robo? Utazungumzia vip kuchukua kombe wakati hata robo fainali yenyewe ni mtihani mkubwa?
 
SALEH JEMBE: HIZI NDIO TAKWIMU SIO ZILE PROPAGANDA

"Simba itawania kucheza Kombe la Dunia la klabu...TUNAPASWA KUJIVUNIA kama nchi Tanzania 🇹🇿

♦️Niwakumbushe rank sahihi si zile za propaganda
♦️Hatua walizopiga Simba muda mrefu ZINAWALIPA SASA
♦️Hii maana yake wanapaswa wazilinde kwa kufanya vema kimataifa
♦️Timu nyingine zilichukulie hili jambo la KUJIFUNZA na si kukandia KIPROPAGANDA
♦️Nafasi ya timu nyingine za Tanzania kupiga hatua zaidi na inawezekana.."

#iamsalehjembe🇹🇿
 
Tukienda kimahesabu tu, Simba inaweza kufuzu bila kuchukua kombe ila kama mambo 4 yatatimia:
1. Bingwa msimu huu awe Al Ahly au Mamelodi
2. Esperance apoteze mechi mbili zilizobaki za makundi na atolewe katika CL
3. CRB na Petro de Luanda wasije kumzidi point Esperance
4. Simba ashinde mechi 2 zilizobaki za Makundi halafu ashinde mechi zote mbili za robo fainali, zote mbili za nusu fainali na moja ya fainali

Ingawa kama nilivyosema, tayari kuna timu mbili za kaskazini zilizofuzu, Simba inabidi ajisogeze angalau nafasi ya 5 chini ya Esperance, ili kama vigezo vingine vitatumika kama vya ukanda Simba iwe chaguo linalofuata. Hatujui vigezo vyoote.
Hizi ndio hesabu hua unakitakaa za tuki waki ,nashangaa unazitumia hapa
 
Mungu hakupi unachotaka anakupa unachostahili. Kama mmekaa kwenye keyboard mkiomba mfuzu kushiriki huku wachezaji wanashinda Juliana wakifika uwanjani ni hovyo kabisa halafu unaomba mkashiriki CWC, badala viongozi wafanye usajili wao wanakomaa na 10% huku nyie mnaendelea kuota tu
 
Tunajua inakuuma kuona mwakarobo anaenda mirikani
 
Mashindano tunayoyazungumza hayafanani.

Maana Yanga imeipiga 5-1 Simba Lakini kwenye orodha ya vilabu vinavyoshindania kucheza Mashindano ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA 2025 HAIMO!!
Nenda kafuatilie tena. Inaonekana huelewi kitu kuhusu hayo mashindano.
 
Back
Top Bottom